Tetesi za soka Ulaya Jumapili 06.10.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Al-Nassr na Ureno Cristiano Ronaldo, 39, anahimiza klabu hiyo ya Saudi Arabia kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne wakati mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 33 na Manchester City utakapokamilika msimu ujao. (Mundo Deportivo)
Manchester United wana nia ya kumteua kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso kuchukua nafasi ya Erik ten Hag na wako tayari kumsubiri hadi msimu wa joto kiungo huyo wa zamani wa Liverpool. (Todofichajes )
Mlinzi wa Aston Villa Pau Torres analengwa na Manchester United, ambao wako tayari kutoa karibu pauni milioni 42 kwa mlinzi huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 27. (Fichajes)

Chanzo cha picha, Getty Images
Klabu ya Saudi Pro League, Al-Ahli inataka kumsajili mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 32, na mwenzake wa Liverpool, Virgil van Dijk, 33, wakati kandarasi zao na The Reds zitakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (Caught Offside)
Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 36, ana chaguo la kuongeza kandarasi yake Barcelona hadi msimu ujao wa joto ikiwa atafikia vigezo fulani. (Sport)

Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona wanafikiria kumtoa kwa mkopo mwezi Januari mshambuliaji wa Uhispania Ansu Fati, 21, ambaye alikuwa na Brighton msimu uliopita. (Sport)
Mshambuliaji wa Uingereza Eddie Nketiah, 25, anasema aliondoka Arsenal na kujiunga na Crystal Palace msimu wa joto ili kupata "fursa ya kuwa uwanjani na kuimarika". (Independent)














