Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vita vya Ukraine: Mwanafunzi wa Nigeria 'hana chaguo jingine zaidi kurudi kusoma'
Akiwa katika msongamano wa magari wa jiji kuu la Nigeria, Lagos, Oyewumi Azeez Olawale anaelekea kwenye miadi ya visa.
Mwaka mmoja uliopita, mwanafunzi huyo wa udaktari wa Nigeria alikuwa akihangaika kutafuta njia salama ya kutoka Ukraine baada ya mashambulizi ya Urusi kuanza tarehe 24 Februari.
Lakini chaguzi zingine za kusoma zikiwa zimefungwa, alirudi Ukraine baadaye mwakani kwa muhula mwingine. Sasa, anataka kusafiri tena kwenda huko.
"Ninarudi Ukraine kwa sababu ninahitaji kumaliza mwaka wangu wa mwisho, kufanya mitihani yangu na kuchukua cheti changu," alisema kijana huyo wa miaka 28.
"Hakuna chaguo kwangu mimi nchini Nigeria," aliongeza.
Ukraine ilikuwa nyumbani kwa zaidi ya wanafunzi 80,000 wa kigeni
Wengine wanafikiria kurejea Ukraine huku wakihangaika kutafuta mahali pa kumalizia masomo yao.
Kwa Bw Olawale, chaguo lilikuwa rahisi.
Mnamo Julai 2022, Baraza la Matibabu na Meno la Nigeria lilisema halitakubali tena digrii kutoka vyuo vikuu vya Ukraine zinazotolewa mtandaoni.
Ilikuwa ni hatua ambayo baraza la matibabu la Ghana lilinakili miezi miwili baadaye.
"Nilihitaji kumaliza shahada yangu nikiwa nahudhuria masomo moja kwa moja," Bw Olawale alisema.
Alibahatika kuwa mahali alipokuwa akisoma palikuwa mbali sana na eneo la mapigano.
Bw Olawale yuko katika mwaka wake wa mwisho katika Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Uzhgorod, ambacho kimekingwa kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa vita kama ilivyo magharibi mwa Ukraine karibu na mpaka na Slovakia.
"Jiji langu liko salama na ndilo chaguo bora kwangu," Bw Olawale aliambia BBC.
Wengine hawakuwa na bahati kama hiyo.
Ukraine ilikuwa kitovu cha wale wanaotafuta elimu ya bei nafuu huko Ulaya, inayojulikana kwa michakato yake ya moja kwa moja ya visa, ada ya chini ya masomo na kiwango cha juu cha masomo.
Baada ya kutumia miaka mingi kuweka akiba ya digrii zao, kurudi nyumbani mikono mitupu haikuwa chaguo kwa wanafunzi wengi.
Baada ya kutumia miaka mingi wakisomea digrii zao, kurudi nyumbani mikono mitupu haikuwa chaguo kwa wanafunzi wengi.
Lakini pia kupata nchi mpya ya kumaliza masomo yao imekuwa si rahisi.
Jessica Orakpo, mwanafunzi anayesomea udaktari wa Nigeria ambaye alipitia ubaguzi wa rangi wakati akijaribu kutoroka Ukraine mwaka jana na taarifa zake kusambaa kwenye mitandao mingi, ni miongoni mwa wale wanaofikiria kurejea.
Hapo awali alikimbilia Hungaria na kisha akahamia Uholanzi ambako sasa anaishi na familia mwenyeji.
Visa yake ya muda inaisha baada ya mwezi mmoja labda apate kazi stadi.
Baada ya kuhitimu mwaka wa 2022, sasa ni daktari aliyehitimu, lakini anasema kutafuta kazi bila ujuzi wa lugha ya Kiholanzi imekuwa changamoto.
"Chaguo langu pekee ni kubaki hapa au kurudi Ukraine.
"Baadhi ya watu wanasema kwa nini usirudi tu Nigeria? Lakini hawaelewi, hilo ni rahisi kusema kuliko kufanya," Dk Orakpo alisema, akitoa mfano wa mifumo ya uchumi na afya inayozidi kuwa mbaya nchini humo.
"Nina malengo maishani, nataka kuwa daktari," alisema, akiongeza kuwa hali ya usalama nchini Nigeria inafanya hilo kuwa changamoto.
Kupata visa ya kurejea Ulaya itakuwa jambo lisilowezekana ikiwa atarudi Nigeria kwa kuwa ameishi nje ya nchi tangu 2016 hana anwani ya kudumu au akaunti ya benki, alisema.
Sawa na wanafunzi wengi wanaosemea udaktari Nigeria, Fehintola "Moses" Damilola, ambaye alikuwa akisoma huko Sumy karibu na mpaka wa Urusi, alitatizika kuendelea na masomo yake mtandaoni, hasa baada ya mamlaka kusema shahada ya mtandaoni haitatambuliwa.
"Sote tumekuwa tukitafuta mbinu mbadala tangu wakati huo," Bw Damilola alisema.
"Sitaki kurejea Ukraine hivi sasa," alieleza. Nilichopitia nilipokwama huko Sumy wakati mashambulizi ya mabomu yalipoanza na ugumu wa kwenda kwenye eneo salama ilikuwa tukio la kuumiza akili sana," aliongeza.
Hata hivyo, Bw Damilola anajua kuhusu wanafunzi wa Kihindi ambao wamerejea kwasababu mitihani ya mwisho inapokaribia.
Mitihani ya mwaka jana iliondolewa kwa sababu ya vita.
Lakini mwaka huu, mamlaka ya mtihani Ukraine imesema kuwa mtihani huo utafanywa na mtu binafsi mwenyewe huko Kyiv mnamo Machi 14.
Kuhudhuria kunamaanisha kutia sahihi hati ya "kukubali hatari zote za usalama", soma barua pepe kwa wanafunzi.
"Realistically, we don't have many options," Mr Damilola said.
Chaguo mbadala linapatikana kwa wale "wasiotaka kurudi Ukraine" kwa njia ya kupatikana kwa "vituo 140 vya kufanya mitihani kupitia kompyuta kote ulimwenguni", ingawa muda wa kufanya hivyo bado hauko wazi.
"Ukweli ni kwamba, hatuna chaguzi nyingi," Bw Damilola alisema.
"Vituo hivyo vya kufanya mitihani katika nchi zingine havionekani kuwezekana hivi sasa, kwa hivyo wengi wetu tunafikiria kurejea."
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, linasema karibu watu milioni nane wametoroka Ukraine na kuelekea nchi jirani za Ulaya.
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) liliripoti watu 625,000 wasio raia wa Ukraine walikuwa miongoni mwao, lakini likaonya kuwa baadhi ya watu huenda wamehesabiwa mara mbili.
Wanafunzi wengi sana wametumia miezi kadhaa kuhama sehemu moja hadi nyingine barani humo kutafuta nchi salama ili kukamilisha digrii zao.
Wengi wamejiingiza katika urasimu tata.
Kujiandikisha katika chuo kikuu kingine mara nyingi kunamaanisha mchakato wa visa kuanza upya, mahitaji ya lugha na ada ya juu ya masomo kwani ufadhili mkubwa wa masomo sasa unatengwa kwa ajili ya raia wa Ukraine.
"Serikali za Ulaya zimewakaribisha Waukraine kwa mikono miwili," alisema Tisa Fumi Yamamoto wa BIPoC Ukraine, shirika lenye makao yake makuu mjini Berlin linalosaidia watu wa asili mbalimbali wanaokimbia vita.
"Lakini raia wa nchi nyingine wanaokimbia vita hivyo hawakuwa na bahati," alisema.
Sheria inapendelea wale wenye kibali cha kuishi, wanaweza kufikia elimu na soko la ajira.
'Hakuna pa kwenda'
EU inasema hii inajumuisha raia wa nchi nyingine ambao "hawawezi kurejea katika hali salama na ya kudumu nchini mwao".
Inasema visa zile za muda zimetolewa kwa watu milioni nne wanaokimbia vita, 200,000 kati yao wakiwa wasio raia wa Ukrainian.
Lakini mashirika mengi ya kutoa misaada na mashiŕika ya mashinani yanasema hali halisi ni tofauti.
"Tumeona watu ambao wamekuwa wakiishi Ukraine kwa miaka 10 wakikataliwa. Wengine hawawezi kurudi katika nchi zao na hawana pa kwenda. Waliacha karatasi zao wakati wa vita," Bi Yamamoto alisema.
"Wanafunzi wengi hawawezi kurudi nyumbani na wanataka tu mahali salama pa kumaliza shule."
Andrew Awuah, mwanafunzi wa mwaka wa mwisho wa udaktari kutoka Ghana, amekuwa akifanya kazi siku nzima ili kumaliza shahada yake barani Ulaya.
"Mimi hufanya masomo yangu mtandaoni, siku zangu za kupumzika nafanya kazi na kusoma lugha ya Kijerumani jioni," alisema.
"Nimebakisha miezi mitano tu nimalize na sitaki shahada yangu ipotee," alisema, alipoulizwa kuhusu kurejea Ghana.
Akiwa nje ya mpango wa visa za muda huku mamlaka ikisema anaweza kurejea Ghana, Andrew alikosa programu ya wiki sita ya ufadhili wa masomo Harvard. Inabidi abaki Ujerumani kama sehemu ya masharti yake ya viza ya muda.
"Najiona mwenye bahati," alisema, kwani amepata kazi ya muda katika chuo kikuu cha Ujerumani.
Wakati wanafunzi wengine wanapofikiria kurudi Ukraine, wengine, kama Victoria Osseme, hawakuondoka kamwe.
Raia huyo wa Nigeria anajiita "mwanamke pekee mweusi huko Kharvkiv, Ukraine".
Baada ya kufanya digrii mbili, na kukaa miaka tisa nchini humo, alisema "aligeuka na kuwa Mkraine."
"Singeweza kuziacha katika hali ngumu kama hii," aliongeza. "Ilinibidi kuwaunga mkono na njia bora ya kufanya hivyo ilikuwa kubaki, kushiriki katika maumivu yao."
Amekuwa akishirikisha wengine uzoefu wake kwenye mitandao ya kijamii tangu Aprili 2022 na anasema amekuwa akipata majibu chanya kutoka kwa Waukraine kwa mshikamano wake.
"Familia yangu na marafiki pia wanajivunia mimi kwa kubaki nyuma na kuiwakilisha Nigeria."
Lakini ingawa wanafunzi wengi wanaweza kutokuwa waaminifu sana kwa Ukraine baadhi, ambao hawajaweza kupata visa kuwawezesha kukaa mahali pengine, wanaanza kuona kuwa licha ya vita, kurejea ndio chaguo pekee lililosalia.