Je, majengo ya mbao yanaweza kuwa suluhisho la athari za mabadiliko ya tabia nchi?

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Frank Mavura
- Nafasi, Bbc Swahili
- Iliyochapishwa
Utegemezi wetu wa saruji na chuma kujenga kila kitu kuanzia nyumba hadi viwanja vya michezo, unakuja kwa gharama kubwa ya mazingira. Zege inawajibika kwa 4-8% ya uzalishaji wa kaboni dioksidi (CO2) duniani. Ikiwa ya Pili tu kwa matumizi zaidi Duniani baada ya maji, ikichukua karibu 85% ya uchimbaji wote wa madini na kuhusishwa na upungufu wa kutisha wa mchanga ulimwengu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Athari za Mabadiliko ya tabia ya nchi umekua mjadala mkali katika maeneo mbalimbali Duniani. Na hatua kadhaa zimekua zikichukulia katika kupambana na athari hizo ambazo kwa mujibu wa wataalamu inahitajika hatua kuchukuliwa.
Kampuni moja huko visiwani Zanzibar kushirikiana na serikali ya Zanzibar imezindua nyumba Zaidi ya 300 zilizojengwa kwa mbao.
Mradio huo unahusisha ujenzi wa nyumba za mbao kwa ajili ya makazi visiwani Zanzibar ukihusisha nyumba za chini Pamoja na ghorofa.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa kampuni ya CPS Sebastian Dietzold anasema kuwa ujenzi wa nyumba hizi za mbao ni mkombozi wa mazingira na ni hatua nzuri kutokana na kukua kwa kasi kwa wakazi hasa maeneo ya mijini.
‘’Tunatengeneza nyumba za mbao kwasababu hapa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla idadi ya watu inaongezeka sana, na tukaona namna pekee ya kutunza mazingira na kupatia watu makazi, ni kujenga nyumba za mbao ili kuepuka matumizi ya saruji na chuma…’’ anasema bw Sebastian.
Mbao zinatoka wapi?
Ujenzi wa nyumba za mbao, hutegema mali ghali ya mbao zilizotengenezwa vizuri na zilizokomaa. Mbao nyingi huvunwa katika misuti iliyohifadhiwa ama mashamba rasmi.
Katika mradi huu mbao hizo hutolewa ndani ya Tanzania, katika hifadhi na mashamba mbalimbali.
‘’Tuna misuti iliyohifadhiwa vizuri Pamoja na mashamba ya miti huko nyanda za juu kusini mwa Tanzania, Tanzania ina bahati sana kuwa na eneo kubwa la misuti, tuna mashamba makubwa huko mafinga Iringa, tuna heka Zaidi ya 300 ya miti na tunajua wakati gani wa kukatwa’’ anasema Sebastian.

‘’Miti ikukua sana hutoa kaboni nyingi’’
Misonobari mingi katika misitu inayosimamiwa, kama vile spruce ya Ulaya, huchukua takriban miaka 80 kufikia ukomavu, ikiwa ni vifyonzaji wavu wa kaboni katika miaka hiyo ya ukuaji - lakini inapofikia ukomavu, humwaga takribani kaboni nyingi kupitia mtengano wa matawi yaliyoanguka na yanaponyonya.
Kama ilivyokuwa huko Austria katika miaka ya 1990, kupungua kwa mahitaji ya karatasi na kuni kulisababisha misitu mikubwa inayosimamiwa ulimwenguni kutotumika.
Badala ya kurudi kwenye nyika asilia, mimea hii moja hufunika sakafu ya misitu kwa sindano zenye tindikali ya misonobari na matawi yaliyokufa.
Misitu mikubwa ya Canada kwa mfano imetoa kaboni zaidi kuliko inavyofyonza tangu 2001, kutokana na miti iliyokomaa kutokatwa tena kikamilifu.
Nyumba za mbao ndio suluhisho la athari za mabadiliko ya Tabia nchi?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
kulingana na nakala ya Taasisi ya Potsdam ya Utafiti wa Athari za Tabianchi (PIK) , Asilimia 90 ya Makaazi ya watu wa mijini inayoongezeka ulimwenguni katika majengo ya mbao yenye urefu wa kati inaweza kuzuia tani 106bn za uzalishaji wa kaboni ifikapo 2100, unasema utafiti wao.
Lakini hili linaweza kutekeleka katika maeneo mengine barani Afrika? Bado ni swali linalohitaji majibu
Mkurugenzi wataasisi ya misitu Tanzania TAFORI Dokta Revocatus Mushumbusi anasema kuwa matumizi ya mbao huweza kusaidia kupunguza kaboni lakini kuna msingin ya kufuatwa katika kufanikisha hilo.
‘’Ujenzi wa nyumba hizi kwa kutumia mbao, kwa njia moja inaweza kupunguza kwasababu malighali zinazotumika zinaweza kupunguza kaboni, lakini ni lazima kufanya utafiti wa kuona kuwa ni mbao gani ni sahihi na kuhakikisha kuwa miti hiyo imekomaa na lazima iwekwe dawa ili kuzuia ushambuliaji wa wadudu ambao inaweza kupunguza uhai wake wa hizi mbao’’ anasema Dokta Mushumbuzi.
Nyumba za mbao zina utofauti gani na nyumba za saruji?
Kuna tofauti kadhaa wa nyumba za mbao na nyumba za Saruji na chuma, ikiwemo hatua za ujenzi pamoja na vifaa vinayotumika.
Kwa mujibu wa mhandisi ujenzi Bi Debora Baruta kutoka kampuni ya CPS nyumba za mbao huchukua muda mfupi zaidi kulinganisha na nyumba za kawaida katika hatua za ujenzi wake.
‘’Nyumba za mbao hujengwa kwa muda mfupi zaidi kwasababu sehemu kama ukuta wake kujengwa pembeni kisha kupachikwa baadae hivyo zoezi hilo kuchukua muda mfupi kulinganisha na nyumba za kawaida.
Kwa upande wa mkazi wa nyumba hizi, Bi Sharmini Esmail aliamua kununua nyumba ya mbao kutoka katika mradi wa nyumba hizo eneo la Fumba visiwani Zanzibar kutokana na faida kama vile hali ya ubaridi katika nyumba ukilinganisha na nyumba za saruji.
‘’Nyumba yangu hii ya mbao ukiingia ndani hapa unaona kabisa hakuna joto kali licha ya kuwa nje jua ni kali, ukilinganisha na majengo ya kawaida ya saruji, nilivyoona hali ya ujoto haipo nikaona ni fursa nzuri kumiliki nyumba ya mbao’’ anasema Sharmin.

Majengo ya mbao Afrika
Kabla ya kuangazia maeneo mengine barani Afrika katika ujenzi wa nyumba za mbao, Visiwani Zanzibar inatarajia kujengwa jengo refu zaidi barani Afrika litakalohusisha ujenzi mchanganyiko wa mbao.
Maarufu kama ‘BURJ zanzibar’ litakuwa jengo refu zaidi la mbao za mseto barani Afrika.
Wasanifu majengo tayari wanapanga majengo makubwa kwa kutumia mbao nyingi barani Afrika. Mnara wa Utajiri Mkuu wa Gabon, unaotazamiwa kuwa karibu mita za mraba 9,000 za nafasi ya sakafu juu ya zaidi ya ghorofa sita, utajengwa huko Marina, eneo la hekta 13 lililo kwenye ncha ya Libreville.
Mradi huo mkuu unalenga kuhifadhi uwepo wa Umoja wa Mataifa nchini pamoja na wateja wengine mbalimbali wa makazi na reja reja, wakiwemo Mfuko wa Utajiri wa Kifalme.
Kampuni ya kubuni na ujenzi ya BuildX ya Kenya inashughulikia mradi wake wa Makazi ya bei nafuu wa Circular Cooperative Cooperative ambao unalenga kujenga nyumba za bei nafuu zilizotengenezwa kwa mbao.












