Tetesi za Soka Ulaya: Chelsea na Man Utd 'zateta' na Delap wa Ipswich

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Ipswich Town mwenye umri wa miaka 22, Liam Delap amefanya mazungumzo na Chelsea na Manchester United kuhusu uwezekano wa kuhamia mojawapo wa klabu hizo msimu wa kiangazi. (Fabrizio Romano via CaughtOffside)
Licha ya kukosa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa, Manchester United haitapokea ofa zozote kwa ajili ya nahodha Bruno Fernandes, huku Al-Hilal ya Saudi Arabia ikiwa na hamu ya kumsajili kiungo huyo wa kati wa Ureno, 30, kabla ya Kombe la Dunia la Vilabu la Fifa. (GiveMeSport)
Manchester United pia imeridhia klabu ya PSV Eindhoven kumsajili mlinzi wa Uholanzi Tyrell Malacia, 25, ambaye alishinda taji la Eredivisie (Manchester Evening News)
Ruben Amorim ana bajeti ya uhamisho wa majira ya kiangazi ya karibu pauni milioni 100 anaendelea kuungwa mkono na Manchester United licha ya kushindwa kwa fainali ya Ligi ya Europa na Tottenham Jumatano. (Guardian)
Mshambuliaji nyota wa Leicester City Jamie Vardy, 38, ananyatiwa na klabu ya Valencia nchini Uhispania. (Sun)
Newcastle United imezipiku klabu za Barcelona na Real Madrid katika mbio za kumsajili winga wa Uhispania Antonio Cordero mwenye umri wa miaka 18 kutoka Malaga. (Chronicle)
Manchester United imetanguliza mauzo ya mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, na Jadon Sancho, 25, pamoja na winga wa Brazil Antony, 25, kama sehemu ya kuimarisha kikosi chao. (Manchester Evening News)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mjomba wa Viktor Gyokeres anasema mshambuliaji huyo wa Uswidi mwenye umri wa miaka 26 alifanya uamuzi kuzipiga Manchester United na Arsenal msimu huu ili kusalia Sporting. (Sun)
Tottenham wanatumai ushindi wao wa Ligi ya Europa utasaidia kumshawishi beki wa Crystal Palace Muingereza Marc Guehi kujiunge nao msimu huu wa kiangazi. (GiveMeSport)
Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy amshukuru kocha Ange Postecoglou katika hotuba baada ya ushindi wa klabu hiyo ya Ligi ya Europa na anaamini kuwa kombe hilo linaweza kuiweka Spurs 'kileleni'. (Metro)
Nottingham Forest inamfuatilia mshambuliaji chipukizi wa Leicester City, Lorenz Hutchinson, 17. (Mail)
Winga wa zamani wa Liverpool Albert Riera, 43, anayeongoza katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya kocha ajaye wa Hull City. (Talk Sport)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












