Jinsi pikipiki za umeme zitakavyokuwa suluhisho la uchafuzi wa hali ya hewa
Jinsi pikipiki za umeme zitakavyokuwa suluhisho la uchafuzi wa hali ya hewa

Iliyochapishwa
Mamilioni ya teksi za pikipiki [au bodaboda] ni muhimu kwa kusafirisha watu na bidhaa katika majiji ya Afrika.
Lakini injini za vyombo hivi vya moto vitumiavyo Petroli huongeza viwango vya juu vya uchafuzi wa hewa ambao katika maeneo kama Nairobi mara nyingi huzidi viwango salama.
Suluhisho mojawapo ni kubadili na kutumia pikipiki za umeme. Kuna kampuni kadhaa Kenya zinazoanzisha matumizi ya pikipiki za umeme ambazo ni za bei nafuu na mfumo wake ni rahisi kutumia kwani wahudumu wanaozitumia hawapotezi muda mwingi katika kuzichaji.
Yusuf Jumah na taarifa ifuatayo



