Mikakati ambayo Ukraine inaweza kujaribu kurejesha eneo lililotekwa na Urusi

h

Chanzo cha picha, Reuters

Iliyochapishwa

Kama Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imeelezea wazi, Kyiv haina nia ya kutangaza au kudokeza ni jinsi gani au lini itafanya mashambulizi yake ya muda mrefu ya kujaribu kutwaa tena eneo lililotekwa na Urusi katika kipindi cha miezi 16 iliyopita.

Jumatano hii katibu wa Baraza la Usalama la Kitaifa na Ulinzi la Ukraine Oleksiy Danilov, alitupilia mbali kauli za maafisa wa Urusi ambao walisema kwamba uvamizi huo tayari umeanza.

"Haya yote si ya kweli. Haya yote yakianza, jeshi letu litaamua," Danilov aliliambia shirika hilo katika mahojiano. "Tunapoanza mashambulio ya ulipizaji kisasi, kila mtu atajua, wataona."

Kwa vyovyote vile, harakati za hivi punde za jeshi la Ukraine, ambalo limesonga mbele katika eneo la Bakhmut ambalo, kama ilivyoripotiwa na Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu, limeanzisha operesheni hadi kwenye maeneo matano tofauti ya mapambano, harakati ambazo zinaonyesha kuwa kuna kitu kinachoendelea.

Katika siku za hivi karibuni, askari wa Ukraine wameanzisha mashambulizi kwenye mpaka kati ya mikoa ya Zaporizhia na Donestk, karibu na miji ya Velika Novosilka na Vugledar.

Kulingana na wanablogu wa kijeshi wa Urusi wenyewe, jeshi la Ukraine lilifanikiwa nafasi zake katika eneo hili .

Taasisi ya Uchunguzi wa Vita ilithibitisha kwamba Waukraine walisonga mbele umbali wa kilomita tatu kwa usiku mmoja ndani ya Urusi.

Jinsi shambulio la bwawa la Nova Kakhovka limeathiri

Wachambuzi wanasema kuna uwezekano mkubwa zaidi kuwa mlipuko wa bwawa la Nova Kakhovka Jumanne iliyopita, ambapo Kyiv na Moscow zinatuhumiana na ambao umelazimisha kuhamishwa kwa maelfu ya watu katika kilomita 60 za mwisho za Mto Dnieper, katika hali yoyote, iliathiri mipango ya Ukraine.

Ingawa hatujui ikiwa Kyiv ilipanga kuelekeza nguvu zake katika eneo la Kherson, eneo lililoathiriwa zaidi na maji, ili kuliteka tena eneo lililovamiwa na Urusi, "uharibifu wa bwawa, kwa yeyote aliyeufanya, unasababisha tatizo kuwa kubwa zaidi," anachambua mwandishi wa usalama wa BBC Frank Gardner.

Mshauri wa Wizara ya Ulinzi ya Ukraine, Yuri Sak, aliiambia BBC, "kinachotokea (na bwawa) ni jaribio la linaloonyesha kuwa Urusi imekata tamaa kwa namna fulani kwa kushindwa kuathiri mipango yetu, mashambulizi yetu. Wameingiwa na hofu. kufanya ukatili".

Mambo manne muhimu

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ukraine inaweza kuchagua mambo gani mengine?

Huku eneo la Kherson likiwa limekataliwa na Warusi, kwa sasa angalau, mkakati wa Ukraine unaweza kuwa ni kujaribu kuelekea pande nne zinazowezekana, kulingana na Oleh Chernysh, mwandishi wa BBC wa habari wa masuala ya Ukraine aliyebobea katika uchambuzi wa kijeshi:

1. Kwa upande wa mbele wa Zaporizhia, kuelekea miji ya Tokmak na Melitopol, miji mikubwa zaidi katika sehemu inayomilikiwa na Urusi ya eneo hili.

"Inalindwa vizuri sana na jeshi la Urusi, lakini ikiwa wanajeshi wa Ukraine wangefanikiwa kulikomboa na kusonga mbele hadi Bahari ya Azov, lingepunguza ulinzi wa Urusi kwa nusu," Chernysh anaelezea.

2. Kutoka miji ya Vugledar na Volnovaja kujaribu kufikia Mariupol

Mariupol ni mji mkubwa wa katika bandari ya Azov , uliotekwa na Urusi mwaka mmoja uliopita , na ambako mapigano makali dhidi ya kiwanda cha chuma cha Azovstal yalifanyika. Kukamatwa kwa Mariupol kuliliwezesha jeshi la Urusi kuunganisha maeneo yaliyotwaliwa ya Donbas na Kherson na rasi ya crimea, na hivyo kutengeneza ushoroba.

Kukamatwa tena kwa Mariupol kutakuwa na manufaa ya kimkakati, kwa kugawanya eneo la mapambano la Urusi na kuitenga Crimea.

3. Bakhmut

Wanajeshi wa Urusi na mamluki kutoka Kundi la Wagner walidai kuuteka mji huu katika eneo la Donetsk wiki chache zilizopita.

Mji huo umekuwa uwanja wa mapigano makali katika miezi ya hivi karibuni na na umekumbwa na mapigano ya nchi kwa nchi, na imekumbwa na vita virefu na vya umwagaji damu zaidi katika vita hivi vya Ukraine. Ingawa haina thamani maalum ya kimkakati, ina umuhimu wa ishara, kwa Warusi na kwa Waukraine.

Katika za hivi karibuni, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, Hanna Maliar, alithibitisha kwenye mitandao ya kijamii kwamba "licha ya upinzani mkali na majaribio ya adui kushikilia nyadhifa zao, vitengo vyetu vya kijeshi vimesonga mbele katika mwelekeo tofauti wakati wa mapigano" katika ukanda huo.

Kulingana na Maliar, wanajeshi wa Ukraine waliteka tena miji midogo iliyo kilomita chache kutoka Bakhmut, pande zote za kaskazini mashariki na kusini magharibi, kwa lengo la kuwafunga wanajeshi wa Urusi.

Rais Volodymir Zelensky mwenyewe amewashukuru wanajeshi wa Ukraine kwa kutuma "habari tulizokuwa tukisubiri." "Ikiwa jeshi la Ukraine litafanikiwa kuwazingira Warusi huko Bakhmut, litakuwa pigo kubwa sana kwa Moscow," anasema Oleh Chernysh.

4. Kaskazini mwa mkoa wa Luhansk , katika eneo la Svátove-Kreminná.

Hili ni eneo lenye watu wachache na huenda ndilo lililolindwa zaidi na jeshi la Urusi. Ikiwa Ukraine itaweza kuikomboa miji hii miwili, inaweza, kulingana na wachambuzi, kuharibu ulinzi wa Urusi katika eneo hilo.

Kwa sasa haijulikani ni ipi kati ya njia hizi zinazoweza kupendekezwa na makamanda wa Kiukren.

Kwa hivyo, sehemu ya mapigano ambayo jeshi la Urusi litalazimika kulilinda sasa imepanuliwa katika eneo hili kwa kilomita 200, zile zinazotoka kwenye bwawa hadi jiji la Vasilivka, katika mkoa wa Zaporizhia.

Aliihakikishia BBC Radio 4, mashambulio hayo yanaweza kufanywa kwa njia tatu:

1. Kuna uwezekano kwamba, baada ya mfululizo wa shughuli za kijeshi, vikosi vingi vya Ukrainei, watajikita zaidi kwenye mwelekeo mmoja . Kulingana na Clarke, itakuwa ya kufurahisha kuona kinachotokea katika hali hii kusini mwa Zaporizhia, ambapo wangeweza kuelekea Melitopol.

2. Jambo jingine wanaloweza kulifanya litakuwa ni kujaribu kupitia mitandao tofauti.

3. Uwezekano wa tatu unaweza kuwa kwamba watajaribu akufanya mfululizo wa mashambulizi madogo ambayo baadaye yatageuka na kuwa kitu kikubwa zaidi

Ingawa harakati hizo, kulingana na Clarke, zilianza wiki kadhaa zilizopita, na mashambulio tofauti ya ndege zisizo na rubani kutoka pande zote mbili , hadi sasa hakuna shambulio kubwa limeonekana.

Kutokana na uwezo wa Ukraine, Clarke anakadiria kuwa Kyiv itaweza kujaribu kusonga mbele kwa upana usiozidi kilomita 50.