Kwanini idadi ya wanawake wasioolewa inaongezeka

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

“Nimeona mama yangu alivyopitia maisha magumu tangu utotoni, haiku chini ya mikon yetu kupata au kutopata watoto, sitaki maisha ya namna hiyo, mawazo ya kuolewa hayajawahi kuniingia kichwani, nataka uhuru nataka niwe huru kunywa kikombe cha chai kwa raha baada ya kufanya kazi siku nzima na kufanya kile ninachopenda" , haya ni maneno ya Bharani mwenye umri wa miaka 39, ambaye anafanya kazi ya ualimu.

"Sitaki kuolewa. Nadhani nisiolewe isipokuwa nipate mtu ninayempenda, sijapata mtu anayefaa. Sina wazo la kuolewa na mtu. Maisha haya ya peke yangu ni ya raha, "Anasema Poornima mtaalamu wa IT mwenye umri wa miaka 39.

“Niliolewa nikiwa na umri mdogo, mume wangu alinitesa, nilitoka kwenye uhusiano huo, sijishughulishi tena na ndoa, masomo na kazi yangu yananitosha kwa sasa, pia sipingi ndoa, nikipata mtu ambaye ananielewa, kuolewa tena au kuishi pamoja ni sawa, vyovyote, ni sawa kwangu." Alisema Sharon mwenye umri wa miaka 37.

Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watu wenye fikra  kama hao katika nchni India inaongezeka. Uchunguzi wa hivi karibuni wa serikali uligundua kwamba vijana nchini India wanapendelea kuishi wenyewe kuliko kuolewa.

Katika ripoti ya 'Vijana nchini India 2022' iliyotolewa Julai na Wizara ya Takwimu na Utekelezaji wa Mipango, ilibainika kuwa idadi ya wanaume na wanawake ambao hawajaoa katika makundi yote ya umri inaongezeka.

Jambo la kufurahisha ni kwamba, vijana wenye umri wa miaka 25-29 pia hawako tayari kuolewa, utafiti huo ulisema, kati ya 2011-2019, asilimia ya wanawake ambao hawajaolewa inakaribia kuongezeka maradufu huku ile ya wanaume ikiongezeka kwa asilimia 12.

Kwa mujibu wa 'Sample Registration Survey Report 2019' iliyotolewa Machi mwaka huu, wanaume wasio na wake ni asilimia 1.5 pekee huku wanawake wasio na waume wakiwa asilimia 5.2. Wanawake wasio na waume ni wale waliopata talaka, waliofiwa au walioolewa na wametengana.

Kwa mujibu wa serikali asilimia ya wanawake wasio na waume ni kubwa zaidi Karibu katika majimbo yote kuliko ya wanaume wasio na wake.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

'Vizuizi vingi na vikwazo kwa wanawake katika ndoa'  

Bharani anasema kuwa kuna vikwazo vingi kwa wanawake iwe ni ndoa iliyopangwa na wazee au ndoa ya upendo. Wanasema kuwa kumekuwa na mabadiliko katika miji mikubwa lakini hakuna kilichobadilika katika vijiji.

“Mama na baba walifunga ndoa ya mapenzi yao, walifunga ndoa wakiwa na umri mdogo sana, baba yangu alikuwa ni mtu aliyesoma sana, alikuwa na kazi nzuri, alikuwa akilewa na kumpiga mama kila siku, mama yangu alikuwepo pale kwa ajili ya kupata watoto.Baada ya kuzaliwa kwa wasichana watatu walijaribu tena kupata mtoto wa kiume,” Bharani alieleza uzoefu wake.

"Hatukuweza kuvumilia maumivu haya, sote tulimwacha baba na kwenda nje. Mzigo wa kila kitu uliniangukia tangu ujana. Kwa hiyo, nilichoshwa na ndoa yenyewe," alisema.

Alisema wakati mwingine upweke unaumiza, lakini upweke ni bora kuliko kuolewa na kuteseka.

ggg

“Nahitaji muda kwa ajili yangu mwenyewe, baada ya kufanya kazi natamani kukaa kimya kwa muda, kuimba nyimbo... nataka niweze kufanya kile ninachokipenda, nimeona watu wengi wa rika langu wameolewa. Hisia kwamba sitaki magumu haya imeimarika na haijapungua," Bharani alisema.

“Hata mama yangu hakuwa na uhuru wowote, baba alidhamiria kupata mtoto wa kiume, mama yangu alijifungua watoto 9-10, afya yake ilikuwa mbaya sana, kwa vile mimi ndio nilikuwa mkubwa pale nyumbani, Mama alishindwa hata kupumzika kwa sababu ya mambo makubwa.”

"Lengo langu pekee ni kusoma vizuri, kupata pesa na kumtoa mama na dada zangu kutoka kwenye kifungo. Hili ndilo jambo pekee lililokuwa akilini mwangu. Mbali na unyanyasaji wa majumbani, hakuna haki na uhuru kwa wanawake, uamuzi wa kuzaawatoto au la si katika mikono ya wanawake, kuona mtoto wa kiume kama nasaba.

‘Siwezi kuvumilia maumivu hayo'

 “Kutokana na unyanyasaji wa kijinsia na ukatili wa majumbani niliouona utotoni mwangu, nilipoteza hamu ya mahusiano ya kimwili, mambo niliyoyasikia kutoka kwa marafiki zangu yalikuwa yamejikita ndani ya akili yangu, walikuwa wakiniambia kuwa hakutakuwa na uhuru, kila senti iliyopatikana inapaswa kupewa mume na kwamba hakutakuwa na nafasi ya kuishi kama mtu apendavyo. Kwa hivyo, hakuna hatua niliyofikiria ndoa.

Nahitaji kuoata hisia moyoni. Hakuna zaidi ya hayo. Hata hivyo, ni vigumu kuacha uhuru na kuteseka kwa ajili ya upendo huo. Ni bora kukaa peke yako maisha yako yote. Ulikuwa uamuzi nilioufanya mwenyewe. nfutahia sasa,” anasema Bharani

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

'Nilikuwa kama kipepeo asubuhi'

Hadithi nyingine ni ya Sharon, msichana Dalit aliyeolewa na kuachwa. Sharon mwenye umri wa miaka 37 anafanya kazi kama mwalimu katika shule ya serikali. Aliolewa akiwa na umri wa miaka 17 na mvulana aliyemfuata kwa kumpenda lakini, alifichua kwamba alikuwa akimtesa kiakili na kimwili kila siku. 

Alikuwa na tabia ya kunywa pombe. Alikuwa akinipiga kila usiku. Hakuna siku ambayo sikupigwa hadi michubuko ilionekana kwenye kinyesi changu. Kila mtu alikuwa akitazama na makovu akilini mwangu bado yapo.

Nilikuwa kipepeo hadi shuleni. Ingekunjwa nilipofika nyumbani. Niliteseka sana kiakili. Nilitengana naye kwa sababu sikuweza kuvumilia jeuri aliyonifanyia.

Nilipata kazi ya ualimu nikiwa na umri wa miaka 18 niliondoka kwa ujasiri. Mama na baba waliniunga mkono. Walisema inatosha ndio maana tulitengana,” anasema Sharon.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

'Sio uamuzi wa kujitakia.. ndicho kilichotokea'

Poornima, mtaalamu wa IT, hakuolewa kwa sababu hakuweza kupata mwanamume wa chaguo lake na uhusiano ambao aliona nyumbani haukuweza kumuhamasisha.  

Anasema kwamba watu waliooana na wasiofunga ndoa pia wana misukosuko katika maisha na furaha na huzuni.

“Haukuwa uamuzi wangu mwenyewe kwamba sijaolewa, nikiwa na umri wa miaka 27-28 tu ndipo nilipofikia uamuzi kwamba sitaolewa, hata wale waliokuwa karibu nami waliniwekea wazo hilo kichwani. alisema,

Ingawa sikutaka kuolewa na mtu nilidhani ningeolewa tu ikiwa ningepata mtu ninayempenda. Huo ndio ulikuwa uamuzi wangu.Kwa hiyo ninafurahi kwa hilo. Sikuwahi kuhisi kuwa ndoa au kitu chochote ni maisha mazuri. Kwa sababu niliona marafiki zangu wakifunga ndoa na kuteseka. Kuna watu wanateseka lakini hawawezi kutoka kwenye hiyo ndoa," alisema.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

'Nyumba hazipangishwa kwa wasichana ambao hawajaolewa'

Bharani anasema kuwa kutafuta nyumba za kupangisha kwa wasichana ambao hawajaolewa ni kazi sana, ukiwa hujaoa utapata sura za mashaka na nyumba hautapangishwa. 

“Kama utaenda kwenye nyumba watakuuliza kwanza umeolewa au la?" Ikiwa hujaolewa, watauliza kwa nini na hata kama nyumba utapangishwa, macho yote ya watu wanaozunguka yatakuwa kwangu”

Purnima alisema pia alipitia hali kama hiyo ilimchukua takriban miezi 3-4 kupata nyumba. Poornima alisema katika jiji kubwa namna hii hata maeneo ya kitajiri ukiwa peke yako unaambiwa upange nyumba.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

'Kwa nini usituache tuishi jinsi tulivyo?'

Alisema kuwa kuna watu wengi wanaojifanya kuwa hawajaoa kwenye mitandao ya kijamii na kuwaepuka ni shida nyingine.

"Wakati mmoja sikuweza kupata nyumba hata nilitafuta sana, mwishowe ilinibidi niseme uwongo, walipojua ukweli wakaniomba niihame nyumba hiyo. Ili kuepusha kunyanyaswa kwenye mitandao ya kijamii ilinibidi kuandika uwongo kusema 'ndoa'. Kwa nini niseme uongo? Kwa nini wasiniruhusu niishi maisha yangu?" Anahoji.

Je, sheria ya kutotoka nje ya covid imebadilisha mawazo?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Sharon alisema kuwa hakukumbana na shida yoyote kwa sababu ya kufungiwa ndani kwa sababu ya Covid na kuwa peke yake na mtoto wake, wazazi na dada hakukumdhuru. 

Bharani alisema kuwa sheria ya kutotoka nje ya Covid imemuumiza. Alisema kwamba wakati huo alihisi upweke sana.

"Wakati wa kufungiwa, hakuna haja ya kutoka nje ya nyumba kwa sababu ya madarasa ya mtandaoni. Angalau wakati huo, niliona ni vyema kuwa na mwanamume nyumbani wa kuzungumza naye usiku, niliweza kujiuliza swali nini cha kufanya kama nisipoweza kupumua, walau hakutakuwa na mtu wa kunipa maji safi.” Nilikuwa nikihisi upande wa pili kama nateseka," alisema. 

Poornima alifanya kazi kama mfanyakazi wa kujitolea wa Covid. Kwa kweli, alisema kuwa mtazamo wake umekuwa mzuri na sheria ya kutotoka nje ya Covid.

"Nimeona mengi nikifanya kazi ya kujitolea, watu wengi wamepoteza maisha, sijui kesho kutakuwa na, leo ni muhimu, uzoefu huo umenipa mtazamo chanya, maisha ni moja tu. wameelimika kwamba ni muhimu kuishi jinsi unavyopenda badala ya kufikiria yale wengine wanafikiri na wanayofikiri,” alisema Poornima.

ggg

Chanzo cha picha, AFP VIA GETTY IMAGE

Hadhi ya kutokuwa na mwenza

Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wanawake wasio na waume nchini India imekuwa ikiongezeka katika muongo mmoja uliopita na sasa, kuna zaidi ya wanawake milioni saba wasio na waume nchini humo, idaid kubwa zaidi ya hapo awali.

Pia kuna kundi linaloitwa 'Status Single' kwenye Facebook kwa ajili yao. Iiliundwa 2020 Katika maelezo ya utambulisho wa kundi linatajwa kuwa jukwaa hili limeundwa ili kusikiliza simulizi za wanawake milioni 7.4 wasio na waume.

"Tulianzisha jukwaa hili ili kusimulia hadithi za wanawake wasio na waume, waliotalikiwa au waliotenganishwa, wanawake waliofiwa na waume zao au walioachwa na familia zao na wale walio katika vikundi vya LGBT. Jukwaa hili ni muhimu kujadili matatizo yanayowakabili na kusaidia wanawake wenzangu," aliandika katika sentensi za utangulizi.

Walakini, hili ni kundi binafsi Ni mahususi kwa wanawake wasio na waume pekee. Iina zaidi ya wanachama 2,000.

Purnima alisema kuwa baadhi ya hisia katika jamii ni kuwa wanawake wasio na waume wanakabiliwa na matatizo mbalimbali, jukwaa hili ni muhimu sana kwao kufungua akili zao na kutafuta ufumbuzi wa matatizo.