Clemence Mtenga: Hisia mseto kwenye mahafali ya chuo kikuu alichosomea Mtanzania aliyefariki katika vita vya Israel na Hamas
Clemence Mtenga: Hisia mseto kwenye mahafali ya chuo kikuu alichosomea Mtanzania aliyefariki katika vita vya Israel na Hamas

Iliyochapishwa
Mahafali ya 42 ya chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo mkoani Morogoro Tanzania yamemaliza huku yakigubikwa na hisia mseto kutokana na kifo cha mmoja wa wahitimu kwenye vita vinavyoendelea kati ya Israel na Hamas
Kwenye mahafali hayo hapakua na salamu zozote za pole au muda maalumu wa kumkumbuka licha ya jina lake kuwa kwenye kitabu cha wahitimu.
Wahitimu wenzake wamemwelezea kuwa mtu nyenyekevu na aliyeishika dini huku wazazi wakiwaombea faraja wazazi wa Clemence.
Imeandaliwa na Eagan Salla