'Putin alichukua kila kitu kutoka kwetu, na tukamuachia'

Jina kamili la Nadya Karpova ni - Nadezhda – likimaanisha 'tumaini' katika lugha ya Kirusi. Ana tatuu ndogo yenye maneno ya Kiingereza kwenye sehemu ya mbele ya shingo lake. Aliiweka alipokuwa na umri wa miaka 21, lakini hata hakumbuki ni tumaini gali alilokuwa nalo wakati ule. Lakini kwa sasa neno hilo lina maana halisi.
Tangu Urusi ilipoivamia Ukraine tarehe 24 Februari, ni idadi ndogo tu ya wanamichezo wa Urusi walikuwa wamezungumza kupinga uvamizi huo.
Miongoni mwa wachezaji wa sasa kimataifa wa soka, ni watatu tu waliofanya hivyo.
Kutoka katika timu ya Urusi ya wanaume, Fedor Smolov wa timu ya Dynamo Moscow alituma ujumbe 'No war!' kwenye mtandao wa Instagram Februari . Tangu wakati huo amekuwa kimya. Aleksandr Sobolev kutoka Spartak Moscow pia alituma ujumbe katika siku ya kwanza ya vita lakini akaufuta saa chache baadaye.
Karpova, ambaye anachezea klabu ya Espanyol katika Uhispania ni wa tatu.Ni mwanamke pekee wa timu ya wanawake wa Urusi ambaye ameweza ameelezea kupinga vita hivyo, na alifanya hivyo karibu kila siku. Tangu vita vilipoanza , miezi zaidi ya mitatu iliyopita , amekuwa akituma jumbe kwenye Instagram, ambako ana wafuasi 143,000.
"Siwezi kuangalia tu huu unyama na niendelee kubakia kimya," anasema. "Sijui ni nini kingetokea kama ningekuwa Urusi, sio Uhispania, lakini ninahisi kuwa na wajibu wa kipekee wa kuzungumza wazi."
Mahojiano yetu yalifanyika katika mji wa Barcelona, ambako mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 27 anaishi baada ya kuhamia huko mwaka 2017. Alicheza michezo 24 kwa ajili ya Urusi, iliwemo michuano ya mara ya mwisho ya Kombe la washindi la Ulaya, miaka mitano iliyopita. Michuano ijayo iko karibu tu - katika England kuanzia tarehe 6 hadi 31 Julai- lakini timu ya Urusi haitakuwa pale. Wamewekewa marufuku - kutokana na uvamizi wan chi hiyo wa Ukarine.
Tulikutana katika mghahawa wa Kichina, tangu tulipoanza mazungumzo hakuweza kugusa chakula kila mara tulipoanza kuzungumza kuihusu Ukraine. Aliwasili mapema, akiwa mwenye njaa, na akaagiza chakula cha Kichina ambacho hupakuliwa kweney chungu cha moto ambacho walaji hula wenyewe- wakiongezea mboga, nyama na tambi.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Anachagua maneno yake kwa uangalifu. Lakini sio kwamba anajaribu kujizuia mwenyewe kuzungumza-licha ya kwamba sheria mpya inaweza kumfunga jela miaka 15 mtu ambaye mamlaka za Urusi zitakiangalia kama usambazaji wa ‘’taarifa za uzushi’’ kuhsuu jeshi.
Haogopi kusema kitu ambacho sio sahihi. Bladala yake anaogopa kusahau kitu ambacho ni muhimu. Na anasema pia anajaribu sana kutozungumza matusi tu. Kadri mahojiano yanavyoendelea kuwa marefu ndivyo anavyoendelea kupunguza umakini.
"Propaganda ya Urusi inajaribu kuwashawishi Warusi kwamba ni taifa la kipekee sana na dunia nzima iko dhidi yetu na 'mpango wetu wa kipekee'," anasema.
"Ni mopango gani wa maana unaouzungumzia? Sidhani Warusi ni wa kipekee. Wakati huo huo, siaibiki kuwa Mrusi, kwani Urusi haimaanishi serikali na Vladimir Putin.
"Putini alichukua kila kitu kutoka kwetu, alichukua hali yetu ya baadaye. Wakati huo huo alifanya hivyo bila idhini yetu. Wao, serikali, hawakushuhudia upinzani imara. Watu wengi walikuwa tu wanafunga macho yao ukosefu wa haki, wakifikiria kuwa haiwahusu.
"Nilishiriki katika mikutano miwili ya upinzani, wa mwisho ulikuwa ni wa kuunga mkono kiongozi mkuu wa upinzani wa Urusi Alexei Navalny wakati alipopewa simu na kufungwa, lakini bado, sidhani nimefanya vya kutosha.
"Watu hawa wanaohalalisha vita, ni mateka wa propaganda. Ninawahurumia, na ninaamini tunahitaji kufanya kila kitu kuwaokoa."

Chanzo cha picha, Getty Images
Karpova alikuwa na umri wa miaka 22 alipowasili Uhispania. Valencia ilikuwa imeshuhudia mambo yanayotosha kumpatia mkataba mkataba baada ya Euro 2017, ingawa alicheza kama mchezaji wa ziada kwani Urusi ilishindwa kufika ngazi ya muenguano katika Uholanzi.
Kitu kikubwa kilichohomtia moyo Karpova kuhama kilikuw ani viwango vya soka ya wanawake. Hali ya hewa pia ilikuwa ni sababu pia – haifurahishi sana kucheza soka wakti wa majira ya baridi nchini Urusi. Baada ya kuhamia uhispania, kitu fulani muhimu kilibadilika kwake.
"Niliacha kuogopa baadhi ya mambo kwa mfano kuzungumza wazi," anasema. "Pia nilielewa kwamba mtu angenilaumu kwa kuishi na msichana na kwamba hakuna unyanyapaa hapa kwa wapenzi wa jinsia moja wa kike.
"Kocha wako hapa anaweza kukuuliza : 'Mpenzi wako wa kike anaweza kuja katika mechi ?' Nilifikiria tu nikasema wow. Nchini Urusi, watu huuliza tu kama una mpenzi wa kiume, hapa wanasema 'mwenza' - 'pareja'.
Tangu alipokuwa mtoto, Karprova amekuwa akijaribu kuficha hali yake ya kuwa mpenzi wa jinsia moja, au hata walau sio kuizungumzia katika umma. Anaelezea tu hadithi kuhusu mazungumzo ya kwanza ya mkataba wake wa kazi.
Mmiliki wa klabu , Rossiyanka, alikuwa najaribu kumshawishi baba yake kusiani, akiahidi kwamba "tutamtunza binti yako, mpenzi wa jinsia moja ".
Karpova anasema: " kulingana na watu hawa, wapenzi wa jinsia moja wa kike, walihitaji matunzo maalumu. Wakati huo nilikuwa na umri wa miaka 18. Baba yangu alimwambia mwanaume huyu…nenda zako. Alisema kuwa alikuwa tayari kuzunguza kuhusu soka tu, na sio kuhusu hali yangu ya jinsia .
"Tofauti baina ya hap ana Urusi , kama mtu anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja katika kundi la LGBT, ilikuwa kubwa."
Katika mwaka 2013, 'kueneza mapenzi ya jinsia moja’ miongoni mwa watoto kulitangazwa kuwa ni ukiukaji wa sheria nchini Urusi chini ya wanaounga mkono sheria mpya iliyosemekana kuwa ina lengo lakulinda "maadili ya utamaduni wa Warusi ".
Hakuna mchezaji hata mmoja anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja ambaye yuko wazi kuhusu hali yake nchini Urusi
"Sasa propaganda ya Urusi inajaribu kuwapinga watu wanaoongea wazi dhidi ya vita.
" Kwa mfano wakati , argarita Simonyan [mhariri mkuu wa vyombo vya habari vya taifa RT], alikuwa akizungumzia msimamo wa upinzani wa vita wa (mchekeshani na mtangazaji) Maxim Galkin, akisema: 'Ni mpenzi wa jinsia moja!' Kama kuwa mpenzi wa jinsia moja inamaanisha kwamba wewe ni mbaya, mtu anayeudhi asiye na maadili kitabia .",

Mwezi Machi, Karpova alijiunga na mshambuliaji mwenzake katika Espanyol Tamila Khimych, ambaye ni rai awa Ukraine.
"Nilipokuna nay eye kwa mara ya kwanza, alinitazama kwa tahadhari ," anasema Karpova . "Ni kama hakuw ana uhakika iwapo nilikuwa naunga mkono vita na kuwaona Waukraine kama maadui.
"Nilitaka kulia. Nilikuwa nafikiria kuhusu familia yake na marafiki, na iwapo wako SAWA. Ilikuwa ni hisia za kutisha kama hizo kuelewa kuwa anaweza kuwapoteza wapendwa wake.
" Hisia hizo znanielemea. Siwezi kuamini kwamba wakati mwingine hilo ni jambo halisi na linafanyika ."

Chanzo cha picha, Getty Images
Karpova alifurahi kujua kuwa ndugu wa mchezaji mwenzake mpya katika timu wako salama.Lakini maelfu wameuawa , Waukraine wengi bado wako hatarini wakati vita vinaendelea, na hakuna mtu anayejua vitamalizika lini.
Anakiri kuwa anafurahia kuwa kazi yake ya sasa haina uhusiano wowote na taifa la Urusi kwa vyovyote vile – kinyume na wanamichezo wengi wa kulipwa wa Urusi. Anafikiri kwamba huenda ikawa jambo la busara kuacha safari ya kwenda Urusi kuwatembelea wazazi na marafiki zake msimu huu wa kiangazi.
Lakini bado, ana matumaini ya mabadiliko.
"Ninatamani Warusi wengi zaidi – Wanamichezo wa Urusi wangeongea hivyo wazi kwa watu wengine ambao wanapinga vita nafahamuj kuwa sio wachache " anasema.
"Huwezi kujifanya tu kwamba hakuna kitu kinachofanyika, haiwezi kuwa hivyo tena. Muda wa kukaa kimya unapaswa kuisha.
"Wao [serikali hii] wataondoka siku moja, wote ni wazee. Wakati hili linatokea, tutakuwa bado hai, na tunapaswa kuwa tayari kutatua kila kitu .
"Natumaini itatokea hivi karibuni sana."















