Msaada Gaza: 'Umeme ukipotea watoto hawa watakufa'

Maelezo ya video, Msaada Gaza: 'Umeme ukipotea watoto hawa watakufa'
Msaada Gaza: 'Umeme ukipotea watoto hawa watakufa'
Iliyochapishwa

Madaktari huko Gaza wanasema hospitali zitaishiwa na mafuta hivi karibuni ambapo watoto waliozaliwa kabla ya wakati na wanaotegemea mashine za kuokoa maisha watakufa nadni ya dakika chache.

Israel izuia maji, chakula, mafuta na usambazaji wa umeme huko Gaza tangu shambulio la Hamas tarehe 7 Oktoba.

Ni msaada mdogo tu ambao umeruhusiwa kutoka Misri katika siku za hivi majuzi, chini ya mkataba ulioidhinishwa na Marekani.