Ravil Maganov: Mkuu wa kampuni ya Urusi afariki katika hali ya kutatanisha

G

Chanzo cha picha, KREMLIN

Maelezo ya picha, Ravil Maganov alipewa tuzo la mafanikio na Rais  Vladimir Putin mwaka 2019
Iliyochapishwa

Mwenyekiti wa kampuni kubwa ya mafuta ya Urusi , Lukoil , Ravil Maganov, amefariki baada ya kuanguka kutoka kwenye dirisha la hospitali mjini Moscow, ripoti  imesema.

Kampuni hiyo imethibitisha kifo chake lakini ikasema kuwa  Maganov, mwenye umri wa miaka  67, ali "kufa kufuatia ugonjwa mbaya ".

Vyombo vya habari vya Urusi vinasema kuwa alikuwa anatibiwa katika Kliniki  mjini Moscow na akafariki kutokana na majeraha yake.

 Maganov  ni mmoja wa maafisa wa ngazi ya juu watendaji waliofariki  hivi karibuni katika mazingira hali za kutatanisha.

 Maafisa wa upelelezi wanasema wako katika eneo la tukio la kifo chake kubaini alifariki vipi. Shirika la habari la Tass lilinukuu chanzo cha habari kikisema kuwa alianguka kutoka dirisha la gorofa ya sita mapema Alhamisi asubuhi, na kuongeza kuwa baadaye kuwa alijiua  mwenyewe.

Muda mfupi  baada ya Urusi kuivamia Ukraine bodi ya  Lukoil board ilitoa wito wa kumalizika kwa vita vya Ukraine haraka iwezekanavyo, ikielezea kuwahurumia waathiriwa wa "msiba huu".

 Rais wake ambaye ni bilionea, Vagit Alekperov, alijiuzulu mwezi Aprili baada ya Uingereza kumuwekea vikwazo kujibu uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine. 

Matajiri kadhaa wa Urusi wamefariki katika hali za kutatanisha miezi ya hivi karibuni  :

  • Mwili wa milionea Novatek meneja wa zamani wa Sergei Protosenya ulipatikana pamoja na wa mke wake na binti yao katika jumba la kifahari la  Spanish villa mwezi aprili
  • Makamu rais wa zamani wa kampuni ya  Gazprombank, Vladislav Avayev, alipatikana akiwa amekufa na mke wake na binti yao katika makai yao mjini Moscow,Aprili 
  • Mwezi Mei, mfanyabiashara taji wa zamani wa  Lukoil  Alexander Subbotin alifariki kusimama kwa moyo wake, ambapo iliripotiwa kuwa alitafuta matubabu mbadala kutoka kwa mganga wa kienyeji

Lukoil ni kampuni kubwa zaidi nchini Urusi. Katika taarifa yake ilisema kuwa  kutokana na kipaji cha utawala cha  Maganov  ndio iliweza kukua na kuwa kampuni kubwa zaidi duniani.

 Alianza kufanya kazi katika kampuni hiyo kibinafsi  katika mwaka 1993 na kuwa mwenyekiti wake miaka miwili iliyopita.

Miaka mitatu iliyopita alipewa tuzo ya mafanikio ya maisha na Rais  

President Vladimir Putin.

Maganov amekuwa akitibiwa katka hospitali viungani mwa mji mkuu Moscow, ambayo inafahamika kuwatibu wasomi na matajiri wa Urusi.

 Mikhail Gorbachev alifariki katika hospitali hiyo hiyo - Central Clinical Hospital,  Jumanne na Putin alitembelea eneo la tukio Alhamisi kuweka shada la maua kando ya jeneza lake.