Mvulana aliyepewa jina la 'Utajiri' mwenye nusu ya uzani anaofaa kuwa nao   

g
Maelezo ya picha, Haftom alihangaika kusimama na kung’ang’ania maisha
Iliyochapishwa

Haftom anakaribia kutimiza umri wa miaka mitano   

Jina lake linamaanisha "utajiri" Kwa lugha ya Kitigrinya lakini uzani wake wa mwili ni nusu ya ule anaofaa kuwa nao.

Daktari anapovuta fulana yake na traksuti  kuonyesha mikono yake na miguu  vilivyokonda , mama yake anaonekana  kumtazama bila huruma. Hataki kumpatia jina.   

Hii ndio hali  halisi ya  kila siku ya  njaa na utapiamlo inayoshuhudiwa baada ya miaka miwili ya viyta vya wenyewe kwa wenyewe katika jimbo la kaskazini mwa Ethiopia la  Tigray.  Mkataba wa amani umemaliza vita lakini athari za mzozo bado zipo.

 Mwezi Agosti, Umoja wa Mataifa ulikadiria kuwa karibu mtoto mmoja kati ya watatu walio na umri wa chini ya miaka mitano katika Tigray walikuwa na uta-piamlo.  

 Wakati wanajeshi wa Serikali ya shirikisho na wa vikosi vya Tigray walipokuwa wakipigana, mamlaka za serikali yashirikisho ya Ethiopia walipunguza au kuzuia kabisa misaada kufika katika eneo hilo la Kaskazini, kabla ya kuzuia kabisa misaada.  

'Mikono mitupu'

Makda, ambaye ana umri sawa na mzozo wenyewe, anaonekana kama mtoto mchanga  mikononi mwa mama yake  Hiwot.

Ni mchovu na tumbo lake limevimba. 

Hii ni mara ya pili kwa   Makda kupelekwa hospitalini kwa kuugua
Maelezo ya picha, Hii ni mara ya pili kwa  Makda kupelekwa hospitalini kwa kuugua

"Imekuwa vigumu sana kupata chakula" anasema Hiwot. "Ni viumu sana kula hata mlo mmoja kwa siku."

Lakini tangu alipolazwa hospitalini, hali ya Makda imekuwa ikiendelea kuwa mbaya zaidi.

"Binti yangu yuko katika hali hii kwasabau tuliambiwa hakuna madawa. Hatujaweza kupata chochote," anasema Hiwot.

"Hata wakati tulipokuwa hapa mwaka jana na tatizo sawa na hili, sikuweza kupata chochote na nikaenda nyumbani mikono mitupu ."

Familia ya  Haftom na Makda imekuwa ikitafuta matibabu katika mji mkuu wa jimbo la tigray -Mekelle. BC ilichukua picha zao na kufany amahojiano katika kipindi cha mwezi uliopita.

Baada ya usitishwaji wa mapigano wakati vikosi vya serikali ya shirikisho vilipochukua maeneo zaidi, maafisa wa tigray walikubali kusitisha mapigano. 

Chini ya mkataba wa amani uliosainiwa mwezi uliopita  maafisa katika mji mkuu Addis Ababa, walisema watatuma misaada zaidi 

'kutumiwa kwa siku'

Dkt Kibrom Gebreselassie  amekuwa daktari wa upasuaji katika hospitali ya rufaa ya   Ayder Referral kwa miaka 15.

 Ni hospitali kubwa zaidi ya umma katika jimbo lenye wakazi milioni saba. 

"Kuwaona watoto wadogo na akina mama wakiumia na kulia kila siku, inasikitisha sana," anasema Dkt. Kibrom.

 "Watoto wengi wamekufa katika hospitali yetu kwasababu wakati watoto wanapopatwa na utapiamlo, si  chakula tu unachopaswa kuwapatia. Wanahitaji madawa, ya  antibiotics, na madini… na hatuna hizi."

g
Maelezo ya picha, Dkt Kibrom alihangaika kuendelea kuendelesha hospitali yake wakati wa vita vya miaka miwili

Baadhi ya vile vinavyohitajika vinaonekana kuwasili, lakini havitoshi.

Dkt Kibrom anasema malori mawili yad awa kutoka kwa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (ICRC) yalikuwa ya kwanza kuwasili  mjini Mekelle.

 "Kiwango cha dawa ambazo tulipokea kilikuwa kinawatosha nusu ya wagonjwa wet una kiwango hicho kilidumu tu kwa muda wa siku moja ," anasema

 Kwa siku moja ambayo msaada haufiki hospitalini, wagonjwa zaidi hufariki. 

"kwa mfano wagonjwa wa saratani, hali ni mbaya. Kumekuwa hakuna tiba ya mionzi (chemotherapy) katika Tigray nzima," anasema Dkt  Kibrom.

 "Kila siku, kila wiki , kila mwezi, hatua ya saratani yao inakuwa mbaya zaidi.

"Iwapo ingetibia kabla, lakini sasa haiwezi kutibika. Kwa wale wanaoumwa sana kila siku, kila saa inayopita wanakabiliwa na kifo."

Juhusi za misaada

Kuanzia katikati ya mwezi Novemba hadi kufikia wiki ya kwanza ya Disemba, serikali ya Ethiopia – na mashirika ya misaada wameweza kutuma zaidi ya malori 16 ya chakula , malazi na vifaa vya matibabu, ilisema ofisi ya Umoja wa Mataifa.

 ICRC, ilisema ilituma malori 38 Mekelle tangu katikati ya mwezi Novemba, na mengine zaidi yako njiani. 

 "Juhudi za kutoa misaada zinafanywa na wadau wote wa masuala ya kibinadamu  lakini hazitoshi  ikilinganishwa na mahitaji," anasema Jude Fuhnwi, msemaji wa ICRC nchini  Ethiopia.

g

Chanzo cha picha, ICRC

Maelezo ya picha, Shirika la mpango wa Chakula Duniani linasema limeingilia kati katika juhudi za kupeleka misaada kwa njia ya misafara ya magari inayokwenda Tigray tangu kusainiwa kwa mpango wa amani.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani  (WFP) limelenga kuwapatia misaada ya chakula watu milioni 2.1 katika Tigray kwa kipindi cha miezi sita ijayo.

 "Kuna mafanikio makubwa yaliyofikiwa tangu uliposainiwa mkataba wa amani ," anasema  Claude Jibidar, mwakilishi wa WFP na Mkuruigenzi wake nchini Ethiopia.

 "Baada ya miaka miwili ya mzozo, hatutarajii kurejea katika hali ya kawaida kwa sikuu moja."

Mekelle imesalia kuwa chini ya udhibiti wa serikali ya Tigray ingawa vikosi vya shirikisho bado vinadhibiti maeneo  ya kaskazini karibu na Shire.

Katika idara htofauti ya Hospitali ya  Ayder , Fikadu Jember, mwalimu mstaafu, anaelezea jinsi ambavyo hajaweza kupata matibabu ya ugonjwa wa kisukari kwa miezi mitatu iliyopita.   

 "Tulipokuja hapa kwa ajili ya kupata matibabu, vingi kati yavifaa havikuwa vikifanya kazi. Tulikuwa tunajaribu kila mahali, lakini hapakuwa na kitu kwasababu tulikuwa tumewekewa vikwazo’’, anasema.

watu wengi wanakufa kwasababu ya hili .Baada ya makubaliano kusainiwa, tulikuwa  na matumaini kuwa tutapata dawa lakini bado hakuna chochote kilichowasili."

g
Maelezo ya picha, Fikadu Jember ana matumaini mkataba wa amani utasaidia kuboresha maisha yake   

Madaktari wanakosa vifaa vya kimsingi.

"Hatuna glovu za kutosha kufanya upasuaji. Tunalazimika kuziosha We don't have na kuzitumia tena hadi mara tatu ," anasema Dkt. Kibrom.

 "Hatuwezi kufanya uhamishaji wowote wad amu kutoka kwa mtu mmoja kumuwekea mwingine kwasababu hatuna mifuko ya kutunzia damu. Kwahivyo, iwapo tunajua mgonjwa ambaye atahitaji damu, hatuwezi kumfanyia upasuaji ," anaongeza.

Umeme ulirejeshwa

Daktari mwingine  katika hospitali hiyo ya  Ayder ambaye alipendelea jina lake lisitajwe anasema wanapokea vifaa vichache sana vya matibabu.  

 "Hospitali imejaa majeruhi wanajeshi na raia wagonjwa,"anasema daktari. "Wengi wanasaidiwa."

 Wanasema jambo zuri tu ambalo  maafisa wa  shirikisho  wamelafanya ni kurejesha umeme katika Mekelle.

Hivi karibuni hospitali ilituma ujumbe wa Twitter kwamba dawa za HIV na vipimo vya kupima virusi  hivyo vimeanza kuwasili. 

Lakini waginjwa wasio na uwezo wanalazimika kulipa garama ya juu. 

"Ninataka mwanangu awe na maisha bora yajayo," anasema mama yake  Makda,   Hiwot. "Hilo ndilo ninaloweza kufuikiria pekee."

G