Tetesi za soka Ulaya: Liverpool na Real Madrid wafanya mazungumzo kuhusu mustakbal wa Alexander Arnold

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool na Real Madrid walifanya mazungumzo kuhusu mustakabali wa Alexander-Arnold kabla ya mechi ya wawili hao ya Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Anfield siku ya Jumatano. (Marca - Spanish)
Beki wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 21 kutoka Hungary Milos Kerkez anavutiwa na Manchester United na Liverpool. (Sky Germany via Florian Plettenberg)
Manchester United ina orodha fupi ya mabeki wengine watatu wa kushoto, akiwemo mchezaji wa kimataifa wa Uingereza wa Chelsea mwenye umri wa miaka 27 Ben Chilwell, mchezaji wa kimataifa wa Algeria mwenye umri wa miaka 23 Rayan Ait-Nouri na Mhispania Alvaro Carreras, 21, ambaye anachezea. Benfica. (Rudy Galetti)
Chelsea wanamtaka mshambuliaji wa Ipswich mwenye umri wa miaka 21 Liam Delap, lakini wanaweza kukabiliana na ushindani kutoka kwa klabu ya zamani ya Manchester City. (Football Insider}

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 27, anaweza kujiunga na Liverpool msimu ujao wa joto. (Fichajes - Spanish)
Sevilla wanafikiria kusitisha mkataba wa mkopo wa beki wa Brighton mwenye umri wa miaka 20 kutoka Argentina Valentin Barco mwezi Januari. (Fabrizio Romano)
Aston Villa bado wanavutiwa na mshambuliaji wa Besiktas na Uturuki Semih Kilicsoy, lakini italazimika kupambana na PSG kuwania saini ya kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 mwezi Januari. (Star In Turkish)
Arsenal wamefanya mazungumzo Kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa England Adam Wharton, huku Crystal Palace wakimthamini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kwa takriban euro 65m (£54.1m). (Caught Offside)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amewataja kiungo wa kati wa Real Sociedad Martin Zubimendi, 25, na Kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen naa Ujerumani Florian Wirtz mwenye umri wa miaka 24 na winga wa Sporting wa Uruguay. Kama wachezaji anaolenga kuwasajili katuika dirisha la uhamisho la mwezi Januari (Fichajes - in Spanish, external)
Aston Villa wanavutiwa na kiungo wa kati wa Mainz na Ujerumani Nadiem Amiri, 28. (Bild – in Germany)
Manchester United, Manchester City na Liverpool zote zinamtaka kiungo wa kati wa Atalanta na Brazil Ederson, lakini itahitaji ofa kubwa kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (TeamTalks),
Fiorentina na Napoli wanatazamia mkataba wa mkopo kwa mlinzi wa Arsenal Jakub Kiwior lakini kuna uwezekano meneja Mikel Arteta atamruhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland mwenye umri wa miaka 24 kuondoka the Gunners mwezi Januari. (Tuttomercato – In Italy),
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












