Tshala Muana kutoka kuimba kanisani hadi kuwa nguli wa muziki wa Rhumba Afrika

Chanzo cha picha, Getty Images
Lisabeth Tshala Muana Muidikay, anayejulikana pia kama Tshala Muana, 'Malkia wa Mutuashi' alizaliwa tarehe 13 Machi 1958 huko Lubumbashi.
Alikuwa wa pili katika familia ya watoto kumi.
Mama yake, Alphonsine Bambiwa Tumba alikuwa mjane mwaka wa 1964 baada ya mumewe Muidikay Amadeus kuuawa kama mwanajeshi na wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani na kuuawa Patrice Lumumba.
Tangu utotoni mwake, aliimba katika kanisa la kambi ya jeshi ya Kibembe katika iliyokuwa Elisabethville.
Mnamo 1967, miaka miwili baada ya kifo cha baba yake, mama yake alihama na watoto hadi Kananga na mapema miaka ya 70 aliishi Kinshasa.
Huko alianza taaluma yake mnamo 1976 kama mcheza dansi katika kikundi kipya cha mwimbaji cha M'Pongo Love.
Baadaye, pia alikuwa sehemu ya bendi ya Minzoto Wella Wella na Les Tigresses A'beti Masikini kwa muda.
Mnamo 1978, aliondoka kwenda Afrika Magharibi kwa tafrija mpya ya muziki.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ilianzia Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuishia kupitia Nigeria na Togo nchini Ivory Coast.
Ni katika kipindi hicho hicho ambapo Sam Mangwana na kundi lake waliweka makazi yake Abidjan na kutoka huko waliteka Afrika Magharibi kwa sauti yao nzuri ya kuvutia ya Congo.
Ilikuwa huko Abidjan ambapo msanii na mtayarishaji wa Ivory Coast Jimmy Hyacinthe aligundua kipaji chake cha aina nyingi kama mwimbaji, mcheza dansi na mtunzi wa dansi na kumjumuisha katika bendi yake.
Ilikuwa pia Hyacinthe kwamba alikwenda Paris mnamo 1982 kurekodi wimbo wake wa kwanza wa 12Inch 45rpm, na upande wa a-side wimbo wa pop ulioimbwa kwa Kifaransa 'Amina' na wimbo 'Tshebele', kwa kuzingatia mdundo wa mutuashi wa watu wa Baluba kutoka eneo la kusini la Kasai nchini Congo.
Mnamo 1984 alirudi Paris kwa muda mrefu, ambapo katika kipindi hicho alizidi kuwa kitovu cha muziki wa pop wa Kiafrika.
Huko, pamoja na mpiga besi wa Cameroon, mpangaji na mtayarishaji Aladji Touré, alirekodi albamu kadhaa - Kami', 'Mbanda Matière' and 'M'Pokolo' - kwa ajili ya lebo ya Safari Ambiance.
Siku hizo pia alianza kufanya kazi na mpiga gitaa wa Congo Rigo Bamundele Star.
Tshala aliandika nyimbo zake nyingi yeye mwenyewe tofauti na wasanii wengine wengi wa Congo, hakuishia tu na rumba ya Kikongo inayoimbwa kwa lugha ya Kilingala na soukous.
Katika albamu zake na katika maonyesho yake, alitoa nafasi kubwa kwa nyimbo katika mahadhi ya mutuashi, zilizoimbwa kwa lugha yake ya mama Tshiluba.
Sio kosa kusema kwamba uboreshaji wa mdundo huo na umaarufu uliofuata wa mutuashi ni kwa kiasi kikubwa kutokana na Tshala Muana.
Baada ya Abidjan na Paris, sasa alitaka kushinda nchi yake na muziki wake.
Mnamo 1986, alirudi Kinshasa kwa tamasha kadhaa ili kujitambulisha tena nyumbani.
Ijapokuwa matamasha yake yalipokelewa kwa shauku, ilionekana wazi kuwa uchumi duni ulimfanya msanii huyo asiweze kujikimu kimaisha nchini Congo.
Alirudi Paris kuendelea na kazi yake kutoka huko.
Alifanya hivi kwa kutoa albamu mpya kwa utaratibu wa kila mwaka na kisha kuzuru Ulaya na Afrika.
Pamoja na Mbilia Bel, alikua mmoja wa ‘Wanawake Wanaoongoza wa muziki wa Congo mwishoni mwa miaka ya 1980.
Lebo ya kurekodi ya Marekani, Shanachie pia iliona sifa zake na ilitoa mkusanyo wa nyimbo zake kwenye CD mwaka wa 1991 chini ya jina lililokosewa mahali pengine ‘Soukous Siren’.
Nyimbo nyingi kwenye albamu hiyo zilitegemea mdundo wa mutuashi na hazikuwa na uhusiano wowote na soukous.
Lebo hiyo huenda ilichagua jina hili kwa sababu wasanii wa Congo kama Kanda Bongo Man na Diblo Dibala pamoja na Loketo walikuwa maarufu nchini Marekani wakati huo kwa muziki wao wa dansi wa hali ya juu miongoni mwa mashabiki wa ulimwengu unaoibukia.
Katika miaka ya 90, Tshala Muana aliendelea kujiendeleza kimuziki.
Katika miaka hiyo aliandika nyimbo kadhaa ambazo alifanikiwa kutoka mtindo wa Mutuashi hadi Salsa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Matokeo hayo yanaweza kusikika kwenye baadhi ya nyimbo za CD ‘Mutuashi’, iliyotolewa na lebo ya British Sterns mwaka wa 1996.
Mnamo 1998, alishiriki pia kwenye albamu ya tatu kutoka mfululizo wa ‘Sans Papiers’, iliyotolewa na Ibrahim Sylla.
Katika albamu hii, iliyoandaliwa na Lokassa Ya Mbongo, uteuzi wa wasanii ulishirikiana na medleys ambao walitoa pongezi kwa waimbaji kama vile Mbilia Bel, M'Pongo Love, Oumou Sangare na Nahawa Doumbia.
Wakati mwaka wa 1997 Laurent Désiré Kabila alichukua nafasi kutoka kwa Mobutu Sese Seko kama rais wa Congo, ambako pia kuliathiri maisha na kazi ya muziki ya Tshala Muana.
Miaka hiyo Tshala Muana alizidi kujihusisha na siasa za Congo.
Mnamo 1999 alikua mjumbe wa kitaifa katika Bunge la Mpito la Bunge la Katiba na Sheria.
Hii ilifuatiwa na miaka mitatu ambayo hakuna albamu yake hata moja iliyotolewa.
Kwa bahati nzuri, alianza pale alipoishia mwaka 2002 na albamu ya ‘Dinanga’, ilipotolewa ambayo ina maana ya ‘Mapenzi’.
Mnamo 2006, alitoa albamu mbili yenye jina ‘Mamu Nationale’ ambayo inamaanisha ‘Mama wa Taifa’.
Katika miaka iliyofuata, aliendelea kutoa albamu mara kwa mara.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mnamo 2018, kwa mfano, alitoa albamu ‘Don de Dieu’ pamoja na Mbilia Bel - hadithi nyingine ya kike hai ya muziki wa Congo. Akiwa ametimiza miaka 45, mnamo 2020 ilionekana kana kwamba kazi yake ya muziki ilikuwa imekamilika.
Baada ya kulazwa hospitalini kwa dharura mnamo Juni 2020, ripoti zilienea kwamba ‘Malkia wa Mutuashi’ alikuwa amefariki.
Muda mfupi baadaye, hata hivyo, alitoa taarifa akisema kwamba bado yuko hai na yuko mzima.
Kwamba yeye bado yuko katikati ya maisha ya muziki na kisias. Hili lilithibitishwa miezi michache baadaye mnamo Novemba wakati alitoa wimbo ‘Kutokushukuru’.
Maneno ya wimbo huo yalimuudhi Rais Tshikseki hadi akakamatwa na kuwekwa kizuizini kwa siku kadhaa.
Mwimbaji huyo nguli wa Rhumba Élisabeth Tshala Muana ameaga dunia na taarifa za kifo chake zikithibitishwa na mtayarishaji na mwandani wake, Claude Mashala.













