Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 24.08.2024

Chanzo cha picha, PA Media
Juventus wapo kwenye mazungumzo na Manchester United kuhusu kumnunua winga wa Uingereza Jadon Sancho, 24, ingawa inatarajiwa kuwa vigumu kwa Manchester United kufikia utashi wa kukubali thamani ya United ya £40m . (Athletic - subscription required)
Sancho anaweza kuhamia Italia kwa mkataba wa mkopo, huku United ikiwa tayari kwake kumhamisha bila chaguo la kununua licha ya kuwa wangependelea kumnunua kwa mkataba wa kudumu. (i)

Chanzo cha picha, Getty Images
Napoli wako kwenye mazungumzo na Manchester United kuhusu usajili wa kiungo wa kati wa Uskochi Scott McTominay, 27. (Sky Sports)
Mlinzi wa zamani wa West Ham na Italia Angelo Ogbonna, 36, anatazamiwa kuhamia Watford kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Watford Observer)

Chanzo cha picha, Getty Images
Bournemouth wamemtambua mlinda mlango wa Chelsea Kepa Arrizabalaga, 29, kama shabaha kuu ya uhamisho, huku The Blues wakitaka kumtoa Mhispania huyo. (Athletic - subscription required)
Manchester United wamekubali mkataba wa kumsajili kiungo wa kati Sekou Kone, 18, ambaye aliivutia sana Mali katika michuano ya Kombe la Dunia la Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 mwaka jana, kutoka Guidars FC kwa £1m pamoja na nyongeza kadhaa kulingana na uchezaji wake. (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wanatazamia kukata tamaa katika harakati zao za kumtafuta winga wa Athletic Bilbao Nico Williams, 22, licha ya mshindi huyo wa Euro 2024 wa Uhispania kuwa analengwa zaidi na The Gunners msimu huu wa joto. (Independent)
Southampton wanafikiria kumnunua mlinda lango wa England Aaron Ramsdale, baada ya Arsenal kukataa ombi la mkopo kutoka kwa Ajax kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Porto wamekubali mkataba na Arsenal kumrejesha kiungo wa kati wa Ureno Fabio Vieira, 24, kwa mkopo. Alijiunga na The Gunners kutoka Porto Julai 2022 na yuko chini ya mkataba hadi 2027. (Mail)
Brighton wamekubali ada ya uhamisho ya pauni milioni 30 na Fenerbahce, ambao wamethibitisha kuwa amesafiri kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu, kwa winga wa Uturuki Ferdi Kadioglu, 24. (Ajansspor - in Turkish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Aston Villa wamekubali mkataba na Bologna kumtoa kwa mkopo winga Mwingereza Samuel Iling-Junior, 20, aliyejiunga kutoka Juventus msimu huu wa joto, kurudi Serie A. (Fabrizio Romano)
Mshambulizi wa zamani wa Uingereza Mason Greenwood, 22, anatazamiwa kubadili utiifu wake wa kimataifa kwa Jamaica na kucheza chini ya meneja mpya Steve McClaren. ( Jua)

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool wanamfuatilia kwa karibu mlinzi wa Bayer Leverkusen na Ecuador Piero Hincapie, 22. (Football Insider)
Mshambulizi wa Hull City na Colombia Oscar Estupinan, 27, anasafiri kwa ndege kuelekea Mexico kujiunga na FC Juarez na ataukosa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Millwall . (Hull Daily Mail)
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












