Magumu wanayopitia wazazi wa kiume wanaobaki majumbani

Dad

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Ingawa jukumu la mama kama mlezi wa wakati wote wa watoto linakubaliwa na wengi, akina baba wanaochukua uamuzi kama huo wa kuwa mlezi wa wakati wote wanaweza kuhukumiwa na kutengwa.

Muulize Steven Lange anafanya nini, na atakuambia. Au kwamba anafanya kazi kutoka nyumbani. Au kwamba amestaafu, ingawa anaweza kurejea kazini wakati mtoto wake mdogo atakapohitimu sekondari mwaka ujao.

Kile ambacho anaweza kusema ni kile anachohisi kwamba ni sahihi zaidi.

"Mimi ni baba wa kukaa nyumbani," anasema mkazi wa Ohio, Marekani mwenye umri wa miaka 52, ambaye alifanya kazi ya kutengeneza chapa na ukuzaji wa bidhaa kwa miaka 30 kabla ya kuanza kukaa nyumbani na kulea watoto wake mnamo 2020.

"Lakini sifikirii naweza kumwambia mtu yeyote hivyo, au kujitambulisha hivyo," anaongeza. "Najikuta nikihisi ninahitaji kukueleza kwamba sikunji tu nguo na kupika chakula cha jioni na kwenda kununua mboga. Nina mambo mengine ninayofanya."

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kujitambua huko kunaendelea licha ya kujua jinsi alichokianzisha kimekuwa cha manufaa: ameanzisha uhusiano wa karibu na mwanawe kijana; amekuwa karibu kumsaidia mjukuu wake aliyezaliwa; na mpango huo umemwezesha mke wake kusomea shahada ya uzamili.

Akina baba wa wnaaokaa nyumbani kama Lange wanazidi kuonekana kuwa ni jambo la kawaida. Nchini Marekani, kwa mfano, idadi ya kina baba wanaokaa nyumbani iliongezeka karibu mara mbili kutoka 1989 hadi 2012. Lakini bado si ya kawaida.

Kati ya familia za Marekani zenye jinsia tofauti, wazazi walioolewa, asilimia 5.6% wana mama wanaofanya kazi na baba wasio na kazi, ikilinganishwa na 28.6% na baba wanaofanya kazi na mama wasio na kazi. (Inafaa kukumbuka kuwa hii inajumuisha watu ambao hawana kazi lakini wanaweza kuwa wanatafuta kazi, kwa hivyo ni makadirio tu).

Katika nchi za Umoja wa Ulaya (EU), ni nadra zaidi: takriban mwanaume mmoja kati ya 100 huacha kazi zao kwa angalau miezi sita kwa ajili ya malezi ya watoto, ikilinganishwa na mwanamke mmoja kati ya watatu.

Hili linamaanisha kuwa wanaume wanaofanya chaguo hili wanaweza kujisikia kama watu wasio wa kawaida - na wakati mwingine huhukumiwa vikali. Hata katika tamaduni ambazo akina baba wanatarajiwa kuhusika zaidi kuliko hapo awali, bado wanatarajiwa kuwa walezi wa familia na mara nyingi wanachukuliwa kuwa wasio na malezi au ujuzi wa nyumbani kuliko akina mama.

Haya yote yanamaanisha kwamba, kwa akina baba kama Lange, kukaa nyumbani na watoto kunaweza kuhisi kuwa jambo lisilo la kawaida na la kutengwa - hata kama hawataki iwe hivyo kwa njia nyingine yoyote.

Spencer Bouwhuis)

Chanzo cha picha, Spencer Bouwhuis

Maelezo ya picha, Spencer Bouwhuis na familia yake huko Utah Marekani

'Ninahisi kama wakati mwingine ninatazamwa'

Katika nchi kama Marekani na Australia, baba bora anatarajiwa kujishughulisha zaidi na maisha ya kila siku ya watoto wake kuliko siku zilizopita, anasema Brendan Churchill, mhadhiri mkuu wa Sosholojia katika Chuo Kikuu cha Melbourne nchini Australia, ambaye anatafiti kuhusu 'ubaba' au kuwa baba anayelea.

Hata hivyo, "mtindo wa wanaume kuwa watafuta riziki unadumu. Unaimarishwa kila siku katika utamaduni wetu." Likizo ya uzazi kwa mzazi wa kike au mama, kwa mfano, inasalia kuwa ya ukarimu zaidi katika nchi nyingi kuliko likizo ya uzazi kwa upande wa mzazi wa kiume au baba.

Imani hii ya kitamaduni kwamba akina baba wanapaswa 'ulinzi na kutoa' (kwa familia) inaweza kusalia vichwani mwa akina baba wa nyumbani, hata wale wanaohisi kuwa wanafaa zaidi kuchangia familia zao katika jukumu lao kama mlezi mkuu.

"Nilipokuwa sekondari, sikuwahi kujiona nikienda chuo kikuu na kuwa na kazi ya kifahari. Nilikuwa na furaha sana, kila mara, kuwa baba," anasema Spencer Bouwhuis, 25, huko Utah, Marekani. "Siku zote imekuwa ndoto yangu kuwa baba wa kukaa nyumbani."

Huko Chicago, Eric Taylor, 43, anakaa nyumbani kumtunza mtoto wake wa miaka miwili. Akiwa na PhD katika saikolojia ya kimatibabu, Taylor ana mpangilio rahisi wa kufanya kazi akiwa nyumbani huku mkewe anafanya kazi mbili nje ya nyumbani.

Licha ya mtazamo wake wa usawa kuhusu jinsia na uzazi - moja ya malengo yake makuu ya kazi ni kuwawezesha akina baba kujisikia kuhusika na kuthaminiwa kama mama. Hata hivyo yeye, pia, anajikuta akitilia shaka jukumu lake.

"Ninahisi kama wakati mwingine ninatazamwa, kama vile ninapoosha vyombo, na aina fulani ya kikundi cha wasimamizi wa kiume mahali fulani ambao wananiangalia na kunifuatilia na kusema, 'Kwa nini unasafisha sahani sana?'", Anasema.

Ingawa Taylor huchangia kifedha kwa familia yake, wakati mwingine yeye hukasirika na kujiona ana hatia kwa kutokuwa mlezi mkuu. "Ninatatizika kuhisi kama, 'siisaidii familia yangu'," anasema. "Kwa ndani ninaumia na kujiuliza maswali; 'Je, mimi ni mtu ambaye nabaki tu nyumbani, huyu mtu anahifadhiwa na mke wake anayetoka na kuleta chakula nyumbani?'

Eric Taylor

Chanzo cha picha, Eric Taylor,

Maelezo ya picha, Eric Taylor na binti yake wa miaka miwili huko Chicago Marekani

"Baba wengi hawaelewi hili

Mambo yaliyomo kwenye mioyo yao ama Sauti za ndani zinazowazungumzisha wababaa ni changamoto moja inayowasumbua baadhi ya baba wanaokaa nyumbani kulea watoto. Jambo lingine ni namna gani wanatazamwa ama kuchukuliwa na watu wengine kutokana na majukumu ya nyumbani.

Hakuna ushahidi mzuri kwamba walezi wa kiume hawana ujuzi mzuri kwa ajili ya jukumu hilo kuzidi wanawake. Na utafiti wa hivi majuzi umeonyesha kuwa akina baba, kama akina mama, hukumbana na mabadiliko ya homoni na mitandao ya neva wanapoingia katika malezi ya uzazi - mabadiliko ambayo yanaonekana kuwasaidia kuwa walezi na wenye huruma zaidi.

"Wanawake sio mama wa asili zaidi ama kuliko wanaume walivyo baba wa asili - inahusisha kujifunza, lakini kinachofanya ionekane ulezi wa mtoto ni 'ya asili' ni kwasababu wanawake wanatarajiwa kufanya hivyo," anasema Churchill.

Hata hivyo, baadhi ya wanaume na wanawake wanaendelea kuamini kwamba akina baba hawapaswi kuwa walezi wa wakati wote wa watoo. Kukaa nao wakati wote na kuwalea kuanzia asbuhi mpaka asubuhi nyingine.

Huko Malta, Manrico Bugeja, 36, aliacha kazi yake kama mwalimu wa Kifaransa miaka sita iliyopita na kukaa nyumbani na watoto wake, ambao sasa wana umri wa miaka minne na mwingine sita. Yeye na mke wake walitaka watoto wao wakae na mzazi badala ya kuwapeleka kwenye vituo vya malezi ya watoto. Wkkati huo huo mke wake, mhasibu, alikuwa akipata mshahara mkubwa zaidi.

Uamuzi huo ulionekana rahisi. Lakini si kwa kila mtu. “Tulikuwa na watu wetu wa karibu ambao walisema, ‘Kwa nini usifanye kazi ya muda, ili uingize pesa nyingi kama yeye?’,” anasema Bugeja. "Na kisha kuna wale ambao watasema kwamba mtu huyu mvivu." Lakini angesikia watu wakisema maneno kama, "Sijui inakuwaje wanaume wanavyofanya hivyo, kuwaacha wake zao wafanye kazi".

Kyle Rasmussen

Chanzo cha picha, Kyle Rasmussen

Maelezo ya picha, Kyle Rasmussen na familia yake huko Montana Marekani

Huko Montana, Marekani, Kyle Rasmussen, 38, anawatunza watoto wake wawili kwa muda wote. Anakumbuka akioka keki ndogo za blueberry ili binti yake aende nazo shule ya awali kama vitafunio. "Mmoja wa akina mama alinipongeza sana kwamba niliweza kutengeneza keki," anasema.

Manrico Bugeja

Chanzo cha picha, Manrico Bugeja

Maelezo ya picha, Manrico Bugeja na familia yake huko Malta