Mwalimu aliyepoteza kazi kwa kutuma picha zake Instagram

Iliyochapishwa

Chuo kikuu maarufu binafsi katika mji wa mashariki mwa India wa Kolkata (uliofahamika awali kama Calcutta) kimegubikwa na utata katika miezi ya hivi karibuni.   

Profesa msaidizi wa zamani katika chuo  kikuu cha  Mt Xavier aliiambia BBC kuwa alilazimika kuacha kazi yake kwa kuwa alichapisha picha zake zilizoonesha akiwa amevaa nguo ya ndani aina ya bikini kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.   

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye aliomba jina lake lisitajwe, aliwashutumu maafisa wa chuo hicho  kikuu  kwa  " kumnyanyasa kingono " na anasema "alitishwa, kudhalilishwa na kuchunguzwa maadili."

Pia aliwasilisha  malalamiko kwa polisi na kutuma taarifa ya  kisheria kwa taasisi, ambayo ilijibu kwa kumshutumu kwa kuichafulia jina na kudai ilipwe rupia milioni 990   (takriban dola milioni $2.4) kama fidia.   

   Walinipeleka katika chumba cha upelelezi

Profesa msaidizi anasema kwamba alijiunga na kitivo  tarehe 9 Agosti , 2021 kwa ajili ya kufundisha somo la Kiingereza kwa wanafunzi wanaosomea shahada.

Miezi miwili baadaye, aliitwa katika ofisi ya mkuu wa chuo kwa ajili ya mkutano.    

Aliongozwa "hadi katika chumba cha upelelezi" ambako alihojiwa na kamati inayojumuisha Makamu mkuu wa chuo  Felix Raj, katibu wa chuo Ashish Mitra na wanawake watano.

Alifahamishwa kuwa kulikuwa na malalamiko dhidi yake yaliyotolewa na baba wa mwanafunzi wa kiume anayesomea shahada. 

"Mkuu wa Chuo alisema kwamba baba huyu alimpata mwanaye wa kiume akizitazama picha zangu kwenye Instagram ambapo nilikuwa nimevaa nguo ya ndani. Alisema picha zilikuwa zinaonesha utupu na akakiomba chuo kikuu kimuepushe mwanaye na uchafu wa aina hiyo."

Wajumbe wa bodi walizungusha kipande cha karatasi kilichokuwa na "picha tano- sita " na kumuomba athibitishe kwamba zilikuwa ni zake.  

"Wazazi wako wameona picha hizi?"

“Waliniambia kuwa nilikuwa ninakishushia heshima na kukiaibisha chuo kikuu. Waliniuliza iwapo wazazi wangu wako kwenye Instagram na iwapo waliziona picha hizo. Nilihisi kichefuchefu na nilishituka .”

Aliombwa kurejea siku iliyofuata na ripoti ya maandishi.  

Msamaha na "kulazimishwa kujiuzulu"

Profesa alirejea kwenye ofisi ya Kansela siku iliyofuatia na kuwasilisha msamaha wake " uliokuwa umeandikwa kuhusu ushauri kwa baadhi ya wajumbe wa kitivo ambao walijumuisha mkuu wa kitengo cha jinsia ," mwanafunzi niliyesoma naye na profesa msaidizi ambaye pia alikuwa mjumbe wa jopo ambalo lilikuwa likimhoji.

 "Kama picha zangu zilifasiliwa kwa njia ambayo ingeweza kuchafua sifa ya chuo kikuu, basi ninaomba msamaha," aliandika.

Ni "uzoefu usiofurahisha sana," alisema.

Alitumaini kuwa suala hilo lingeishia hapo. Lakini mkuu wa chuo alimwambia kwamba bodi  "kwa kauli moja imependekeza afutwe kazi ."

 "Anasema kwamba picha tayari zilikuwa zimesambaa sana, kiasi kwamba wengi wa wanafunzi walikuwa wameziona, kwamba wasingenichukulia kama mtu mwenye umakini  na kwamba wazazi wangelalamika. Na kwamba ingekuwa vyema nijiuzulu kwa hiari ."

Kama sitafanya hivyo, aliniambia kwamba "angeenda jela, kwasababu baba wa mwanafunzi aliyeziona picha alitaka kupeleka malalamiko polisi." Iwapo asingeacha kazi, angeweza kukamatwa, aliambiwa na mkuu wa shule.

''Nilihisi nimezingirwa sina jinsi, na nikajiuzulu ", anasisitiza. 

"Lakini pia nilihisi mwenye hasira na kutafuta ushauri wa kisheria. Walipakua picha zangu na kuzisambaza bila idhini yangu. Kwahiyo wakili wangu alipendekeza kwamba niwasilishe kesi ya malalamiko ya unyanyasaji wa kingono na uhalifu wa kimtandao kwa polisi ," anasema.

 

"Hatukuombi ujiuzulu"

Padre Baba Felix Raj, Makamu Chansela, alikataa kuongea kuhusu iwapo kamati ilikuwa imependekeza afutwe kazi, lakini akakanusha madai dhidi yake na Chuo kikuu.    

"Sisi ni taasisi takatifu la masomo na ujuzi. Kama mzee na mkuu wa chuo kikuu, Nilimwambia kwamba asingepaswa kuweka picha hizo."

 Picha hizo, ambapo alikuwa amevaa vipande viwili vya vazi la kuogolewa, zilikuwa ni picha za selfi zilizochukuliwa katika chumba chake, anasema. Alizishirikisha kwenye  Instagram kwenye kitengo cha 'hadithi', akitarajia kwamba zitatoweka saa 24 baadaye. 

 Bodi ya kitivo haikubali maelezo yake: Picha zilichapishwa Juni 13, 2021, takriban miezi miwili baada ya kujiunga na Chuo kikuu na kabla ya kukubali ombi kutoka kwa wanafunzi wake kufuatilia akaunti yake, ambayo ni ya kibinafsi.

Bado anasema,"hakumlazimisha kuacha kazina kwamba aliondoka kwa utashi wake binafsi."

 "Aliwasilisha barua yake ya kuomba msamaha Oktoba  8 (2021). Tulikubali msamaha. Nilidhani ilikuwa ni dalili nzuri. Lakini basi alituma barua yake ya kujiuzulu tarehe 25 Oktoba."

Aliongeza kuwa "hawana kinyongo dhidi yake" na kwamba katika chuo walikuwa "wema sana kwake."

Alipoulizwa kuhusu madai ya profesa kwamba picha hazikuwepo kwenye akaunti yake ya Instagram baada ya kujiunga na chuo kikuu na shutuma kwamba   wajumbe wa bodi walikuwa na hujuma kwake , Padre Feliz Raj alisema "Sidhani kwamba alihujumiwa ."

Kitendo dhidi ya mwalimu amekuwa akikosolewa na wanafunzi wengi wa sasa n awa zamani kwa kuwa cha  "uchokozi."

Taasisi ya  inayotaka mabadiliko- A change.org , lililoanzishwa na mwanafunzi wa zamani wa chuo hicho kikuu  Gaurav Banerjee ombi kwa Wizara ya elimu ya jimbo la kutaka mabadiliko ambalo lilisainiwa na watu  25,000.  

Banerjee aliiambia  BBC kwamba anataka chuo kuomba msamaha kwa profesa na kuitaka serikali ichukue hatua za kinidhamu dhidi ya kamati kwa jinsi walivyoshughulikia suala la mwalimu.   

"Ninafurahi kwamba, sawa na mimi, watu wengi wamesikitishwa na kwamba chuo kinaweza kufanya kitu fulani kama hiki ," alisema.

Hivi karibuni, makumi kadhaa ya wanafunzi walifanya maandamano ya kukaa kimya. 

"Haikubaliki ikabisa. Kwanini mtu ajali kuhusu kile ninachokifanya faraghani? Eneo letu halipaswi kukiukwa," alisema. "Inatisha kwamba wajumbe wa kamati , ambayo inajumuisha wanawake watano, hawakufikiria kwamba huu ulikuwa ni ulinzi wa maadili," aliongeza.

Mwalimu alisema kuwa "amefurahishwa na uungaji mkono ."alioupata.

"Baada ya miezi kadhaa ya kujihisi vibaya, ninahisi kama watu wanaona yaliyonitokea ni kichekesho. "

Haki ya faragha na ya kujieleza, alisisitiza,haipaswi kukiukwa na tunapewa na Katiba ya India na   huu "upelelezi " umevuka nje yae neo la kazi.

"Imani yangu ni kwamba sijafanya kosa lolote. Huenda nisishinde hili, lakini kwangu mimi ni muhimu kupambana," alisema.