Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 15.08.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Napoli wanamtaka kiungo wa kati wa Manchester United, Scott McTominay na pia wanavutiwa na mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Scotland, Billy Gilmour, huku West Ham wakimlenga Tammy Abraham wa Roma.
Napoli wameanza mazungumzo na Manchester United kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Scotland Scott McTominay, 27, na wangependelea mkataba wa mkopo. (Times - usajili unahitajika)
Manchester United wanatarajia ombi rasmi kwa kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 32, ambaye amesalia na mwaka mmoja kwenye mkataba wake. (Sky Sports)
Napoli pia wanakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Scotland Billy Gilmour mwenye umri wa miaka 23 kutoka Brighton . (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea wamerejea kwenye mazungumzo na Napoli kuhusu kumnunua mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 25.(Talksport)
Paris St-Germain wanapunguza nia yao ya kumnunua winga wa England na Manchester United Jadon Sancho , 24, na pia wanafikiria kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kumnunua Osimhen. (i)
West Ham wana nia ya kumnunua mchezaji wa Roma Tammy Abraham huku klabu hiyo ya Serie A ikiwa tayari kumuuza mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 26 kwa £25m. (Gazzetta dello Sport kupitia Football Italia)
Ipswich iko tayari kumsajili kiungo wa kati wa Uswidi Jens Cajuste kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Napoli baada ya Brentford kujiondoa katika harakati za kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Gianluca Di Marzio - kwa Kiitaliano),

Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham wako tayari kuuza wachezaji zaidi kabla ya dirisha la usajili kufungwa huku kocha mkuu Ange Postecoglou akilenga kusalia na kikosi cha wale wanaolingana na mtindo wake wa soka. (Telegraph - usajili unahitajika)
Klabu ya Saudi Pro League Al-Qadsiah imempa mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney, 28, mshahara wa mwaka wa £15.4m na mkataba wa miaka mitatu ili kumshawishi kuondoka Brentford . (Footmercato - kwa Kifaransa)
Ofa ya Arsenal ya kumnunua kiungo wa kati wa Real Sociedad Mikel Merino, 28, ambaye amekubali masharti ya kibinafsi ya kuhamia London, imekataliwa. (Times - usajili unahitajika)

Chanzo cha picha, Getty Images
Klabu ya Bologna ya Serie A inavutiwa na beki wa Chelsea Trevoh Chalobah. Wanataka mkataba wa mkopo kwa Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 25. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Wolves wanamtazama mshambuliaji wa Brentford na Kongo Yoanne Wissa mwenye umri wa miaka 27 kama mchezaji anayeweza kuimarisha mashambulizi. (Telegraph)
Aston Villa inashughulikia mpango wa kumsajili beki wa Colombia Yeimar Mosquera, 19, kutoka Orsomarso SC katika ligi kuu ya nchi yake. (Athletic-Usajili unahitajika)
Imetafsiriwa na Yusuf Jumah












