''Mume wangu alinichoma moto nikahisi ngozi yangu inayeyuka mithili ya plastiki''
''Mume wangu alinichoma moto nikahisi ngozi yangu inayeyuka mithili ya plastiki''
Iliyochapishwa
Wazazi wake waliposhindwa kutimiza ombi la kuongeza mahari Desemba 2000, mume wa Sneha Jawale alimchoma moto kwa mafuta ya taa.
Baadaye mume wake alimuacha na kuondoka na mtoto wao. Lakini Sneha aliazimia kujenga upya maisha yake.
Aliombwa kushiriki katika katika mchezo wa kuigiza, Nirbhaya, uliopewa jina la mwathiriwa wa ubakaji wa magenge huko Delhi 2012 kama mmoja wa walionusurika kwenye vurugu.



