Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 30.09.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wanamfikiria kocha wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri kama uwezekano wa kuchukua nafasi ya meneja Erik ten Hag. (Caught Offside),
Manchester United wanafikiria kumsajili mlinda lango wa Sunderland Muingereza Anthony Patterson, 24, kuwa mwanafunzi wa Andre Onana. (Sun),
Manchester City wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi, 25, katika dirisha la uhamisho la Januari. (Football Insider),
Bayern Munich wanafuatilia matukio kuhusu mlinda lango wa Liverpool na Brazil Alisson Becker, 31, ambaye amekuwa akihusishwa na uhamisho wa Saudi Arabia. {Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle inaweza kuwapa changamoto Inter Milan na Juventus kwa ajili ya kumsajili fowadi wa Lille kutoka Canada Jonathan David, 24. (Calciomercato – In Italy).
Liverpool ni moja ya vilabu kadhaa za ligi ya Premier League vinavyofuatilia hali ya winga wa Sevilla raia wa Uhispania Juanlu Sanchez, 21. (Caught Offside).
Manchester City wameambiwa watalazimika kulipa angalau pauni milioni 70 ili kumsajili kiungo wa kati wa Italia Nicolo Barella, 27, kutoka Inter Milan. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea itahimiza ombi la Januari la kumuuza beki wa kushoto wa Uingereza Ben Chilwell - licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kurejea kwenye kikosi chao cha kwanza. (Mirror)
Liverpool hawana wasiwasi na madai kuwa mshambuliaji mpya wa Misri Mohamed Salah, 32, tayari amekubali kujiunga na klabu ya Saudi Arabia mkataba wake utakapokamilika msimu ujao. (Football Insider)
Barcelona wamepewa ruhusa na La Liga kumsajili mchezaji huru Wojciech Szczesny, 34 - kipa wa zamani wa Poland, Arsenal na Juventus - kama mbadala wa kipa wa Ujerumani aliyejeruhiwa Marc-Andre ter Stegen, 32. (Mundo Deportivo – In Spanish)
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












