BBC Africa Eye: Mzozo mbaya uliozuka Nigeria ulivyogharimu maisha ya maelfu ya watu
BBC Africa Eye: Mzozo mbaya uliozuka Nigeria ulivyogharimu maisha ya maelfu ya watu
Iliyochapishwa
Onyo: Baadhi ya picha zilizomo ni za kuogofya
Mzozo mbaya uliozuka kaskazini-magharibi mwa Nigeria umegharimu maisha ya maelfu ya watu tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Magenge ya majambazi waliojihami kwa silaha nzito yanatishia usalama wa eneo hilo - kuvamia vijiji, kushambulia wasafiri barabarani, na kuwateka nyara.
Miaka ya awali, karibu wasichana 300 wa shule walitekwa nyara. BBC Africa Eye ilitumia miezi kadhaa kufuatilia magenge yenye silaha nyuma ya mashambulizi hayo na kukutana na waathiriwa wa ghasia hizo.



