'Tunabadili dhana potofu kwamba wanawake hukutana ili kusengenya'

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya 2022 ilionyesha kuwa waandishi wa habari wanawake wa Somalia wanakabiliwa na viwango vya juu vya ubaguzi wa kijinsia na unyanyasaji sio tu katika jamii bali katika sehemu za kazi.
Wanahabari wengi wa kike waliripoti kunyimwa nafasi za mafunzo, kupandishwa vyeo na kuhujumiwa wanapokuwa katika uongozi.
Katika jitihada za kupambana na changamoto hizi, Bilan ilibuniwa.
Bilan ni kitengo cha kwanza na pekee cha vyombo vya habari vya wanawake nchini Somalia.
Waendeshaji hutetea hadithi za wanawake na wale walio hatarini na waliotengwa katika jamii.
Wanatumai kwa kusimulia zaidi hadithi hizi, sio tu kwamba watabadilisha mitazamo, bali pia sura ya uandishi wa habari nchini Somalia.
Mtayarishaji/mwanahabari-Esther Akello Ogola
Picha imechangiwa na Mohamud Abdisamad
Imeandaliwa na Jeff Sauke



