Vita vya Ukraine: Kwa nini Warusi wanabadilisha mbinu zao za kushambulia?

Chanzo cha picha, VALENTYN OGIRENKO/REUTERS
Katika siku za hivi karibuni, Warusi wameongeza kwa kiasi kikubwa kasi na ukubwa wa mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani huko Kyiv na miji mingine ya Ukraine.
Takriban kila usiku makumi ya makombora na ndege zisizo na rubani za kamikaze ziliruka katika mji mkuu na vituo muhimu vya kijeshi kote nchini. Mashambulio yanaendelea hadi usiku wa manane, na wakazi wa Kyiv wanashuhudia vita halisi ya "angani".
Makombora mengi na ndege zisizo na rubani yamgonga mwamba, lakini kuna machache ambayo yameleta uchungu kwa Ukraine, kama vile lile lililoshambulia kwenye kambi ya kijeshi karibu na Zhytomyr na Khmelnytskyi.
Na mnamo Mei 29, Urusi ilirudi kwenye utaratibu wa zamani ambao haujatokea kabisa katika miezi ya hivi karibuni - kufanya shambulio kubwa la kombora la mchana kwenye mji mkuu.
Je, haya mashambulio yanayoongezeka ya ndege zisizo na rubani na makombora yanamaanisha nini? Kwa nini wanaanza kushambulia mchana kweupe na je, haya ni mabadiliko makubwa ya kimbinu katika usiku wa mashambulizi ya Kiukreni? Jeshi la anga la Ukraine lilijifunza hili kutoka kwa wataalam wa ulinzi wa anga.

Chanzo cha picha, Reuters
Mbinu mpya
Mnamo Mei, Warusi walifanya mashambulizi makubwa katika jiji la Kyiv na miji mingine kwa kutumia ndege zisizo na rubani 'drones' za kamikaze na makombora mengine marefu karibu kila siku.
Katika siku za hivi karibuni, mashambulizi yamekuwa mikubwa zaidi. Ilifikia hatua kwamba Jumapili usiku, ndege zisizo na rubani 54 za Shaheda ziliruka juu ya anga ya Ukraine kwa mara moja, na Jumatatu usiku - zilikuwa 35 pamoja na makombora 40 ya anga.
Ikiwa karibu mwezi mzima wa Mei mashambulizi hayo yalikuwa yakifanyika usiku pekee (kuanzia hasa saa 7 usiku hadi saa 11 alfajiri), lakini Mei 29, kwa mara ya kwanza kwa muda mrefu, makombora ya cruise na ballistiki yalirushwa kwenye mji mkuu mchana kweupe.

Chanzo cha picha, ANDRII NEBYTOV, TELEGRAM
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Msemaji wa Jeshi la Anga Yuriy Ignat alielezea mabadiliko hayo ya mashambulizi ya Urusi yanatokana na kile Jeshi la Anga la Ukraine linafanya: Warusi inabidi wabadilike na kuendana na hali ya vita na wanatafuta namna mpya. Anasema kwamba Warusi wana ndege nyingi zisizo na rubani nyingi zaidi, ndiyo maana wanazitumia zaidi.
"Katika masuala ya kijeshi, jambo muhimu zaidi ni kuwapotosha adui, kuwafanya waamini katika jambo fulani. Urusi ilifanya shambulio kubwa kwa kutumia ndege zisizo na rubani na makombora ya masafa marefu katika mkoa wa Kyiv usiku huo. Warusi wangeweza kutarajia kwamba baada ya mashambulizi hayo ya usiku kwamba tungekuwa bado hatujajiandaa, na wangeweza kutushangaza. Ni kizuri kwamba hawakweza kufanya hivyo, "anaelezea mashambulizi hayo ya siku.
Utawala wa kijeshi wa Kyiv unaonyesha kuwa kuanza tena kwa mashambulizi ya mchana kwenye mji mkuu ni mbinu dhidi ya raia.
"Kwa namna hii, adui amebadilisha mbinu - baada ya mashambulizi ya muda mrefu, ya usiku pekee, sasa anashambulia jiji la amani wakati wa mchana, wakati wakazi wengi walikuwa kazini na mitaani. Warusi wanaonyesha wazi kwamba wanalenga kuwaathiri raia," mkuu wa KMVA, Serhiy Popko alisema.
Ingawa wataalamu waliohojiwa na BBC Ukraine wanaonyesha kuwa lengo kuu la Warusi sasa ni maeneo ya kijeshi na yenye vifaa na silaha za kijeshi za Ukraine kabla ya Ukraine kutekeleza mashambulizi yao ya nguvu yanayotarajiwa wakati wowote.
Mtaalamu wa ulinzi wa anga Ihor Romanenko anasisitiza kuwa mkakati wa Warusi katika wiki za hivi karibuni unatokana na ukweli kwamba wana wasiwasi sana kabla ya kuanza kwa mashambulizi ya Ukraine.
"Wanalenga kila sehemu ili kuzuia mashambulizi yetu na kudhoofisha uwezo wetu. Bila shaka, serikali yetu inaonyesha uharibifu wa miundombinu na kuuawa kwa raia, lakini Warusi kimsingi wanashambulia vituo vya kijeshi ili kudhoofisha uwezo wetu waa Wanajeshi." , - anaamini Ihor Romanenko.
Anasema kuwa Vikosi vya Wanajeshi sasa vinafanya kazi kikamilifu kwenye kambi za kukabiliana na Urusi, maeneo ya mawasiliano, njia za usambazaji na maghala ya silaha. Warusi wanajaribu kufanya vivyo hivyo pia.
"Ikiwa wana taarifa za kijasusi kuhusu mashambulizi tunayoweza kuyafanya dhidi yao siku hadi siku, basi wanazidisha mashambulizi yao," mtaalamu huyo anasisitiza.

Chanzo cha picha, Getty Images
Awali kama walishambulia mara moja kwa wiki au mara moja kila baada ya siku kadhaa, leo ni tofauti wanashambila kila siku na mara nyingi zaidi.
"Mashambulizi ya usiku na yale ya mchana yana athari tofauti za kisaikolojia kwa wananchi kwa ujumla na hasa wa Kyiv, kwa kuwa Kyiv ni kitivo cha maamuzi," - anaamini Ihor Romanenko.
Warusi wanatafuta kila fursa mpya, kwa hivyo wanatafuta mbinu mpya na kurudia hata za zamani, mtaalam huyo anasema.
Jde lengo ni kudhoofisha mifumo ya anga ya Ukraine?
Valery Romanenko, mtafiti mkuu katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Anga, ambaye ni mtaalamu wa makombora na mifumo ya ulinzi wa anga, anaamini kwamba lengo kuu la mashambulizi ya sasa ya Warusi ni kudhoofisha ulinzi wa anga wa Ukraine. Kabla ya mashambulizi ya kupinga.
Anakumbusha kwamba kulivuja taarifa kwamba Ukraine itakuwa na uhaba wa makombora ya kuzuia ndege kwa mifumo ya ulinzi wa anga ya Soviet na Magharibi.
"Ndio maana Warusi waliona hii nafasi ya kuchokoza mfumo wetu wa ulinzi wa anga haraka iwezekanavyo, ili baada ya hapo waweze kushambulia kwa njia zingine," anasema Valery Romanenko.
Ingawa mtaalam mwenyewe anashangaa kwa nini Warusi hawashambulii sana miundombinu ya usafiri, zaidi wanashambulia mji wa Kyiv na miji mingine mikubwa.
Kwa upande mwingine, anakiri kwamba mashambulizi karibu na Zhytomyr na Khmelnytskyi yanaweza kudhoofisha uwezo wa Vikosi vya Wanajeshi wa ardhi na wa anga.
Valery Romanenko aliona mabadiliko makubwa katika mbinu ya Warusi katika matumizi ya "Shakheds" - katika usiku wa hivi karibuni, waliingia Kyiv kutoka upande wa magharibi. Hapo awali, hawakufanya hivyo. Anasema kuwa utafutaji wa fursa na mbinu mpya unaendelea.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Lengo lao ni kutulazimisha kurusha makombora zaidi. Kombora la cruise na Shahed ni rahisi kuyatungua wakati wa mchana," Valery Romanenko anaamini hivyo.
"Wanaweza kutarajia kwamba angalau kombora moja kati ya kumi yatafanikiwa, lakini sio lengo kuu. Gharama ya "Shahedu" ni karibu dola elfu 20. Na gharama ya kombora la kawaida ni kuanzia dola elfu 200-300," Valery Romanenko anasema.
Lakini haijalishi ni wakati gani wa kurusha makombora ya balestiki - mchana au usiku, kuna mwongozo wa rada tu katika mifumo ya kiotomatiki. Kwa hivyo, kama wataalam wanasema, Warusi hawajali wakati gani wa kushambulia kwa makombora hayo.












