Ni njia gani bora ya kusuluhisha mzozo kati ya DR Congo na Rwanda?

Maelezo ya video, Ni njia gani bora ya kusuluhisha mzozo kati ya DR Congo na Rwanda?
Ni njia gani bora ya kusuluhisha mzozo kati ya DR Congo na Rwanda?
Iliyochapishwa

Kuna mgawanyiko wa maoni kuhusu hatua ya kutuma kikosi cha kijeshi jumuishi kutoka Afrika Mashariki katika lengo la kumaliza ghasia katika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

 Aidha, ghasia zinazoendelea katika eneno hilo zimeweka doa mahusiano ya kidiplomasia kati ya DR Congo na nchi Jirani  Rwanda, ambao wote ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Jumuiya hiyo ina mataifa saba ikiwemo Kenya, Tanzania, Uganda, Burundi, na Sudan Kusini; na huenda mvutano huo ukaleta athari za kiuchumi, usafiri huru wa watu na bidhaa katika mipaka.

Mwandishi wa kitengo cha biashara wa BBC, Jewel Kiriungi, anachanganua mtafaruku huo.