Davido azungumza kwa mara ya kwanza kuhusu kifo cha mwanawe

Chanzo cha picha, Davido
Mwanamuziki maarufu Nigeria , David Adekele, anayejulikana na wengi kama Davido , amesema kwamba anaendelea kumuomboleza mwanawe Ifeanyi Adekele kila siku.
Davido alizungumza wakati wa mahojiano kwa jina "Million Dollaz Worth of Game."
Anasema kwamba haikuwa rahisi kwake yeye kutoa albamu kwa jina Timeless baada ya kifo cha mwanawe
Kulingana na mahojiano hayo , mashabiki wake wengi walitarajia kwamba angetunga wimbo wa huzuni katika albamu hiyo lakini badala yake aliamua kutunga wimbo ambao ungewafurahisha badala ya kuomboleza
‘’Sikumbuki hata siku moja kukaa bila kutoa machozi ‘’
Katika Taarifa yake , mwanamuziki huyo anasema kwamba anaamini kwamba mamake na mwanawe wako mbinguni wakifurahia mziko anaofanya na kwamba haruhusu kuvunjika moyo.
Aliongezea kusema kwamba: Ninapojiangalia katika kioo, najua kwamba watu wengi wanaweka matumaini yao kwangu mimi.
‘’Kila siku machozi yanabubujika mahoni mwangu kwasababu ya kifo cha mwanagu lakini watu hawajui hilo’’.
‘’Najua kwamba mwanangu ananitazama kutoka mbinguni, mbali na hilo mwanangu hangependa nimvunje moyo kwasababu ya mama yake, lazima niwe mwangalifu kutokana na wapenzi wangu wa muziki kote duniani’’.
Ifeanyi alifariki tarehe mosi mwezi wa kumi na moja mwaka 2022 baada ya kuanguka katika bwawa la kuogelea ndani ya nyumba yao huko Banana Island , Mjini Lagos.

Chanzo cha picha, Davido












