Mfahamu Mama Jumapili‚'Mother Theresa' wa Burundi

Maelezo ya video, Christine Ntahe mwanamke anayewalisha watoto yatima kwa mafao yake ya uzeeni
Mfahamu Mama Jumapili‚'Mother Theresa' wa Burundi
g
Iliyochapishwa

Unapofika nyumbani kwa Bi Christine Ntahe mjini Bujumbura Burundi saa za mchana, utadhani ni makazi ya watoto wa mitaani.

Watoto kutoka wa mitaani na wenye wazazi masikini wasio na uwezo wa kupata chakula hukusanyika nyumbani kwake kupata chakula cha bure.

Bi Ntahe ambaye ni mwandishi wa zamani wa habari amepokea tuzo mbali mbali kutokana ajili ya ukarimu wake huku baadhi wakimlinganisha na ‘Mother Theresa’.

Watoto anaowalisha wamempatia jina ‘’Mama dimanche’ au ‘Mama Jumapili’ kwa kuwa huwalisha chakula siku ‘’muhimu’’ ya Jumapili.

Alianza kutoa chakula kwa watoto wa mitaani mwaka 1994 na mpaka sasa ameweza kuwasaidia watoto 10,000 kuishi. Katika Mazungumzo na Idhaa ya Kiswahili ya BBC , Bi Ntahe anaelezea ni kwanini aliamua kuchukua jukumu la kuwalisha watoto yatima na masikini, changamoto na vilevile anatoa wito kwa serikali na wazazi kuhusu watoto hao