Eneo ambalo panya ni bei ghali kuliko Kuku

.

Chanzo cha picha, Grant Singleton Internationa Mice Research Institute

Maelezo ya picha, Panya
Iliyochapishwa

Kabla ya kulala usiku, ikiwa kuna chakula kilichobaki jikoni, tunakificha kwenye jokovu au makopo. Kwa sababu ikiwa tutakiacha kwenye meza, wageni wasiotarajiwa kama panya watakimbilia jikoni mwetu.

Watu wengine huchukia panya wanapowaona.

Kwa mfano, mji wa New York hivi karibuni umeanzisha kanuni mpya za kuondokana na janga la panya. lakini, haimaanishi kwamba panya huonekana kuwa hivi kila mahali.

Katika baadhi ya maeneo panya huchukuliwa kuwa kitoweo muhimu na kitamu sana. Kila mwaka mnamo Machi 7, tamasha linaloitwa "Yunang Aaran" hufanyika katika kijiji cha mbali huko Kaskazini-mashariki mwa India.

Huwa sherehe ya kukata na shoka. Panya hupikwa  kama chakula cha wageni wanaokuja nyumbani . Wakazi hapa pia hutengeneza sahani inayoitwa 'Bole Balak Uing' – ambapo  Utumbo wa panya, maini yake , korodani zake , miguu, mkia hupikwa na chumvi, pilipili na tangawizi.

Wakaazi hapa hula kila aina ya panya. Wanakula kila kitu kuanzia panya wanaopatikana majumbani mwetu hadi panya mwitu.

Mkia wa panya na miguu ni mitamu sana, anasema Viktor Benno Meyer wa Chuo Kikuu cha Oulu nchini Finland. Kama sehemu ya utafiti wake, alizungumza na wakazi wengi. Anafanya utafiti juu ya panya kama chakula.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Panya

Je ni chakula kizuri?

Victor alijifunza mambo mengi mapya katika utafiti huo. "Nyama ya panya ni bora kuliko nyama zote," baadhi ya wakazi walimwambia.

"Hatutaki sherehe, hatuna haja ya kuombaomba. Hatuhitaji hata kusubiri wakati maalum. Tunapika nyama hii wakati wowote tunataka. "Tutafanya hii kama karamu kwa wageni wanaokuja. nyumbani,” walisema .

Panya sio tu sehemu ya lishe ya makabila haya lakini pia hutolewa kama zawadi.

Hapa watu wengine wanatoa panya kama mahari katika ndoa.

Panya pia hupewa binti-mkwe anapopelekwa nyumbani kwa mama mkwe wake.

Panya pia hutolewa kama zawadi kwa watoto siku ya Yunung Aran. Panya hutolewa kwa watoto kama vile zawadi hutolewa kwa watoto siku ya Krismas. Wanacheza na panya kama wanavyocheza  na vinyago.

.

Chanzo cha picha, MEYER -ROCHOW and MEGU

Je nani anayepika?

Hakuna anayejua kwanini wenyeji asilia wa eneo hili walikua wakipenda sana panya. lakini, Victor anasema kwamba wamekuwa wakitumia nyama ya panya kama chakula tangu zamani.

"Kuna wanyama wengi kama kulungu, mbuzi na mafahali wanaozurura msituni. Lakini wanapenda panya zaidi," alieleza.

Victor kwa kweli ni mtu asiyekula nyama . Hata hivyo, alikula nyama ya panya ili kujua ladha yake. Kando na harufu hiyo, ina ladha kama ya nyama nyingine, anasema.

Ulaji wa panya kama chakula hauko katika maeneo fulani ya India. Mtangazaji wa TV ya Uingereza Stephen Gates alifanya kipindi maalum na baadhi ya watu duniani kote ambao wanakula vyakula visivyo vya kawaida.

Kama sehemu ya hili, alitembelea kituo kidogo cha ufugaji wa panya nje kidogo ya mji mkuu wa Younde, nchini Cameroon.

''Panya hawa ni maalum sana. Kwa sababu ni ghali zaidi kuliko nyama ya kuku na mboga hapa," Gates alisema.

.

Chanzo cha picha, GRANT SINGLETON

Je nyama ya panya ni tamu?

Watu walipouliza kuhusu ladha yake , Gates alisema, "Hii ndiyo nyama tamu zaidi ambayo nimewahi kula."

Nyama ya panya hupikwa na nyanya. ''Ilihisi kama nyama ya nguruwe,'' Gates alieleza.

"Nyama ilikuwa na ladha  tamu na mafuta yake yaliyeyuka mdomoni ," alisema.

PROF SR BELMAIN, UNIVERSITY OF GREENWICH

Chanzo cha picha, PROFE SR BELMAIN < UNIVERSITY OF GREEWICH