Zelensky aishutumu Urusi kwa 'unyama' juu ya shambulio la Odesa

Maelezo ya video, Tazama: Bandari kuu ya Ukraine ilivyolipuliwa
Iliyochapishwa

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameishutumu Urusi kwa ‘’unyama’’ baada ya shambulio la kombora kwenye bandari ya Odesa.

Mkataba wa kihistoria wa kuanza tena mauzo ya nafaka nchini Ukraine - uliotiwa saini saa chache kabla ya shambulio - sasa uko kwenye hatihati.

Moscow haijatoa maoni yoyote kuhusu shambulio hilo na Kyiv imesema maandalizi bado yanaendelea ili kuanza tena mauzo ya nafaka licha ya ukiukwaji huo.

Lakini Jumamosi Rais Zelensky alisema inaonyesha jinsi Moscow haiwezi kuaminiwa katika kukumbatia mpango huo.

Aliapa kufanya kila liwezekanalo kupata mifumo ya ulinzi wa anga inayoweza kuangusha makombora kama hayo katika siku zijazo.

Ukraine ni muuzaji mkubwa wa nafaka nje ya nchi1, lakini kwa sababu ya vita, takriban tani 20 za nafaka zimenaswa katika bandari zake, haziwezi kuondoka kwa sababu ya vikosi vya Urusi.

Hii imesababisha uhaba wa chakula na kupanda kwa bei barani Afrika, ambayo kwa kawaida inategemea Ukraine na Urusi kwa ngano.

Chini ya makubaliano ya Ijumaa, Urusi ilikubali kutolenga bandari katika mashambulizi yake wakati usafirishaji wa nafaka unaendelea.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

 Lakini saa chache baada ya makubaliano hayo kutiwa saini, makombora mawili ya Kalibr yalipiga bandari ya Odesa, kulingana na kituo cha kamandi cha jeshi la kusini la jeshi la Ukraine.

Makombora mengine mawili yaliangushwa na mifumo ya ulinzi wa anga, iliongeza.

Shambulizi hilo halikusababisha uharibifu mkubwa kwa bandari, kituo cha jeshi kilisema.

Shambulio hilo limelaaniwa vikali.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken aliishutumu Urusi kwa kuzidisha mzozo wa chakula duniani, na kusema shambulio hilo lilitia shaka juu ya uaminifu wa kujitolea kwa Urusi kwa mapatano hayo.

"Urusi lazima ikomeshe uchokozi wake na kutekeleza kikamilifu makubaliano ya nafaka ambayo imekubali," alisema Jumamosi.

Ikulu ya Urusi hadi sasa haijatoa maoni yoyote kwa umma kuhusu shambulio hilo, hata hivyo serikali ya Uturuki, iliyosimamia makubaliano hayo, ilisema maafisa wa Urusi wamekana kuhusika.

"Katika mawasiliano yetu na Urusi, Warusi walituambia kwamba hawakuhusika kabisa na shambulio hili na kwamba walikuwa wakichunguza suala hilo kwa karibu sana na kwa undani," Waziri wa Ulinzi Hulusai Akar alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban alisema Ukraine haiwezi kushinda dhidi ya Urusi.

Akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa wahafidhina, alisema vita vinaweza tu kumalizwa na mazungumzo ya amani kati ya Marekani na Urusi.

Mkakati mpya unahitajika, ambao unapaswa kuzingatia mazungumzo ya amani badala ya kujaribu kushinda vita," alisema Bw Orban, ambaye maoni yake kuhusu mzozo huo mara nyingi yanakinzana na ya viongozi wengine wa Umoja wa Ulaya.

Siku ya Ijumaa, maafisa kutoka Kyiv na Moscow walitia saini mkataba wa kuruhusu mamilioni ya tani za nafaka zilizonaswa nchini Ukraine kusafirishwa nje ya nchi.

Makubaliano hayo yalisifiwa kama "msingi wa matumaini" na Umoja wa Mataifa baada ya miezi kadhaa ya mapigano.

Mpango huo - ambao ulichukua miezi miwili kufikiwa - unatazamiwa kudumu kwa siku 120, na kituo cha uratibu na ufuatiliaji kitakachoanzishwa mjini Istanbul, chenye wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, Uturuki, Urusi na Ukraine.

Makubaliano hayo yanaweza kupitiwa upya ikiwa pande zote mbili zitakubali.

Wazima moto kwenye eneo kulipotokea shambulio la kombora huko Odesa

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wazima moto kwenye eneo kulipotokea shambulio la kombora huko Odesa

Mkuu wa maswala ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell alisema shambulio dhidi ya Odesa limeonyesha "kutozingatia kabisa

"Kufikia lengo muhimu kwa mauzo ya nafaka siku moja baada ya kutiwa saini kwa mikataba ya Istanbul ni jambo la kulaumiwa," aliandika kwenye Twitter, akiongeza kuwa EU "inalaani vikali" shambulio hilo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres bila shaka amelaani shambulizi hilo, akisema kwamba utekelezaji kamili wa makubaliano ya nafaka ni muhimu.

Mwandishi wa BBC Paul Adams aliyeko Kyiv anasema inajaribu kuonesha shambulio la Odesa kama jaribio la kuharibu mpango wa nafaka.

Lakini mwandishi wetu anasema hilo linaonekana kupingana na matamshi ya Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu kwamba majukumu ya Urusi yamewekwa wazi.

Katika mapigano ya hivi punde ya ardhini, maafisa wa ulinzi wa Uingereza walisema kuwa wanajeshi wa Urusi katika eneo la Kherson walihatarisha kukatwa kutoka kwa njia zao za usambazaji na vikosi vya Ukraine.

Vikosi vya Ukraine vimetumia mifumo mipya ya makombora ya masafa marefu iliyotolewa na Marekani kulenga daraja la Antonovsky huko Kherson.

Ikiwa daraja lingeharibiwa, njia za usambazaji wa Urusi zingenyooshwa kabisa.