Tetesi za soka Ulaya Jumapili tarehe 07.07.2024

,

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Joshua Zirkzee
Iliyochapishwa

Manchester United wanakaribia kumsajili Joshua Zirkzee, Arsenal bado hawajafikia bei ya Riccardo Calafiori na Pascal Gross anatarajiwa kujiunga na Borussia Dortmund.

Manchester United wamekubaliana masharti ya kibinafsi na mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee na wako kwenye mazungumzo na Bologna kuhusu jinsi klabu hiyo ya Italia inataka kima cha ya kuachiliwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 cha £34m ilipwe. (CaughtOffside)

Chelsea wako tayari kuwatoa mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 31, na kiungo wa kati wa Italia Cesare Casadei, 21, kwa Napoli ili kusaidia kupunguza bei ya mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 25. (Teamtalk)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Riccardo Calafiori

Arsenal bado hawajafikia bei ya Bologna ya pauni milioni 42.3 kwa ajili ya kumnunua mlinzi wa Italia Riccardo Calafiori, 22, na mazungumzo kati ya klabu hizo mbili yanaendelea. (Football Italia)

AC Milan wametoa ofa ya awali kwa beki wa kulia wa Tottenham na Brazil Emerson Royal lakini kuna pengo kati ya tathmini ya vilabu kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Sky Sports Italia)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pascal Gross

Kiungo wa kati wa Ujerumani Pascal Gross amekubali masharti ya kibinafsi na Borussia Dortmund, ambao wako kwenye mazungumzo ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 kutoka Brighton kwa kati ya £6m na £8.5m. (Sky Sports Germany)

Tottenham wamehusishwa na kiungo wa kati wa Chelsea Conor Gallagher, 24, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza hana uwezekano wa kuhamia Spurs msimu huu wa joto kwani biashara ya uhamisho iliyofanywa na The Blues imewasaidia kufikia kanuni za faida na endelevu. (Football Insider)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Winga wa Newcastle United Miguel Almiron yuko kwenye mazungumzo na mwakilishi wake kuhusu mustakabali wake huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Paraguay mwenye umri wa miaka 30 akihusishwa na kuhamia Saudi Arabia na Magpies wanaaminika kuwa tayari kumuuza. (Chronicle)

Mshambulizi wa Uhispania Alvaro Morata anatafakari iwapo ataondoka Atletico Madrid na kujiunga na AC Milan, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 akisema atasalia katika klabu hiyo ya Uhispania hadi ashinde kitu nao. (Corriere dello Sport - in Italian)

Florian Wirtz

Chanzo cha picha, Joosep Martinson

Maelezo ya picha, Florian Wirtz

Real Madrid wana imani kuwa wanaweza kuwashinda wapinzani wao wa Uhispania Barcelona katika kumsajili kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Florian Wirtz, 21 . (Sport - in Spanish)

Wakala wa mlinda mlango wa Argentina Emiliano Martinez, 31, anasema Manchester United walikuwa karibu kumsajili kutoka Aston Villa msimu uliopita wa joto lakini mkufunzi wa Old Trafford Erik ten Hag aliamua kumnunua Andre Onana wa Cameroon, 28, badala yake. (ESPN)

Imetafsiriwa na Asha Juma