Uchaguzi Kenya 2022: Changamoto za wanasiasa wenye ulemavu
Uchaguzi Kenya 2022: Changamoto za wanasiasa wenye ulemavu
Iliyochapishwa
Zikisalia siku 14 kabla ya wakenya 22mil kupiga kura katika Uchaguzi mkuu wa Agost 9, baadhi ya wagombea wanaendelea na kampeni za lala salama. Miongoni mwao ni Damaris Caroli ambaye ni mlemavu wa viungo. Licha ya ulemavu wake hakujamzuia mgombea huyu huru kutumia njia ya kampeni za mlango kwa mlango akitembea kwa magongo kuomba kura nyumba kwa nyumba
Mwanahabari wetu @judith_wambare amekutana naye katika Kaunti ya Nakuru, eneo linaloongozwa na kutawaliwa kwa muda mrefu na wagombea wengi wanaume.



