Maelezo ya video, Alipokuwa akikua, Emem Thomas anasema mwili wake wenye nguvu haukuwa unapendwa katika jiji la Uyo, kusini mwa Nigeria. Matamshi hayo ya kejeli yalitikisa imani yake lakini siku moja mwaka wa 2018, alipata nafasi ambayo inathamini kile ambacho Thomas sasa anakielezea kwa fahari kama aina ya mwili wake wa "ukubwa zaidi"Dragon Squad Limited, timu ya mabaunsa wanawake ambao wanavunja imani potofu kuhusu wanawake kuwa mabaunsa. Anawaajiri wanawake tu walio na mwili mkubwa wakibaunsa, na kutengeneza usalama wa wanawake wenye nguvu, na mwili mkubwa katika jamii inayotawaliwa kitamaduni na wanaume. Nchi hiyo , karibu mwanamke mmoja kati ya watatu, wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wamepitia ukatili wa kimwili, kwa mujibu wa Unicef. Tazama video.