Tazama wakati barafu ilipoporomoka katika milima ya Italia
Tazama wakati barafu ilipoporomoka katika milima ya Italia

Chanzo cha picha, AFP
Iliyochapishwa
Picha ya video inaonesha wakati barafu ilipoanguka kwenye miteremko ya Marmolada, kaskazini mwa Milima ya Alps ya Italia.
Takribani watu watano wamepoteza maisha baada ya kunaswa kwenye maporomoko ya theluji yaliyosababishwa na kuporomoka kwa barafu katika mlima mrefu zaidi eneo hilo.
Maafisa wa dharura walisema wengine wanane walijeruhiwa katika ajali hiyo, huku watu wawili wakiuguza majeraha mabaya.



