Tetesi za soka Jumapili: Man United imearifiwa gharama ya kumsajili Jean-Philippe Mateta

Mateta

Chanzo cha picha, Reuters

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester United imearifiwa kuwa itawagharimu pauni milioni 40 kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Jean-Philippe Mateta, 27, kutoka Crystal Palace. (Mirror)

Fulham pia itatafakari ofa za zaidi ya pauni milioni 40 kumuuza beki wa kushoto wa Marekani Antonee Robinson, ambaye anawindwa na Liverpool na Manchester United. (Football Insider)

Huenda Roma ikamuuza Tammy Abraham katika msimu wa joto wakati AC Milan ikiwa haina mpango kumsajili mchezaji huyo wa mkopo kwa msimu ujao na Abraham hatarajiwi kuichezea timu yake msimu huo ujao. (Nicolo Schira)

West Ham, Wolves na Everton zinamtaka Abraham, huku Hammers ikiwa tayari imeshaanzisha mazungumzo na wawakilishi wake kuhusu uwezekano wa kuhama. (Calciomercato)

Semenyo

Chanzo cha picha, Getty Images

Tottenham iko tayari kuwasilisha ombi la takriban pauni milioni 33.6 kumsajili winga wa Bournemouth raia wa Ghana Antoine Semenyo, mwenye umri wa miaka 25. (CaughtOffside)

Chelsea inamwinda mchezaji wa Feyenoord - David Hancko, huku Tottenham ikiwa ni miongoni kwa vilabu vingine walio na hamu ya kumsajili mlinzi huyo wa Slovakia mwenye umri wa miaka 27. (Teamtalk)

Manchester United ina nafasi ya kuongeza mkataba wa Kobbie Mainoo kwa miezi 12 hadi mwaka 2028, licha ya kuwa mchezaji huyo wa kiungo cha kati wa Uingereza mwenye miaka 19 analipwa mshahara mdogo katika kikosi cha wachezaji wakubwa. (Sun)

Norgaard

Chanzo cha picha, Getty Images

Everton itashinikiza kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati raia wa Denmark Christian Norgaard, 30, wakati mkataba wake na Brentford ukimalizika katika majira ya joto. (Football Insider)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Juventus na Brazil Douglas Luiz, 26, huenda akabadilishwa na mchezaji wa Newcastle Sandro Tonali, 24, katika majira ya joto. (Calciomercato)

Newcastle ina hamu ya kumsajili winga Assane Diao 19 kutoka Como katika majira ya joto. (Football Insider)

Inter Milan inataka kufanya majadiliano ya mkataba mpya wa Marcus Thuram wakati mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akihitajika kulipiwa pauni milioni 71.3 ili aweze kuachiwa. (Gazzetta dello Sport)

Eintracht Frankfurt wanaangalia kwa makini hali ya winga mwenye miaka 20 raia wa Uturuki Arda Guler akiwa Real Madrid. (Sky Sports Germany)

Aliyekuwa msimamizi wa Barcelona Xavi, 45, anasema anataka kurudi katika usimamizi na atakubali nafasi ya ajira katika klabu nyingine ya La Liga. (France Football, kupitia AS)

Imetafsiriwa na Maryam Dodo Abdalla