Shauku ya kuwa na mahusiano yasiyo na masharti yazidi kuongezeka duniani

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuwa na mchumba wa ziada ambaye unashiriki naye tendo la ngono wakati tayari uko katika uhusiano wa kudumu kwa kipindi kirefu imekuwa mwiko.
Na ingawa hadi kufikia sasa halijakuwa jambo la kawaida, bado kuna shauku kubwa ya kuwa na mahusiano ya namna hii yanayoendelea kuongezeka.
Dedeker Winston amekuwa katika mahusiano na mke zaidi ya mmoja kwa zaidi ya muongo mmoja, lakini hajawahi kuona shauku kubwa katika mahusiano ya wazi kama ilivyo sasa.
Tangu jadi hili limekuwa mwiko sana katika maeneo mengi, ikiwa ni pamoja na Marekani, ambako Winston anaishi.
Mnamo mwaka 2014, alipoanzisha matangazo ya sauti yaani podikasti ya Multiamory, yeye na watayarishaji wenzake walilazimika kuamua kama watatumia majina yao halisi kwenye kipindi kimoja kilichokuwa kinaangazia kuwa na ndoa zaidi ya moja.
"Wakati huo, kulikuwa na podikasti moja au mbili tu zinazozungumzia suala hili," anasema mtaalam wa masuala ya uchumba.
"Na watu ambao walikuwa wakitengeneza na kukaribisha podikasti hizo walitumia majina bandia."
Lakini mambo yamebadilika.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mnamo mwaka wa 2016, Winston aligundua "mlipuko wa shauku katika uhusiano zaidi ya mke mmoja", kama mwaka mmoja baada ya kuanza kazi kama mtaalam wa masuala ya mambo ya uchumba aliyebobea katika mahusiano.
"Hapo ndipo nilipohisi kama niliona mabadiliko makubwa zaidi, kwa ghafla watu wengi mtandaoni kuwa tayari kuzungumza juu ya kutokuwa na mke mmoja," anasema, "na kueleza ukweli kwamba wanapendezwa na aina hii ya mambo.”
Sarah Levinson, mshauri katika Tiba ya Saikolojia inayohusiana na ubunifu katika Jiji la New York, ambaye anajishughulisha na masuala ya kujamiiana na mienendo ya uhusiano, pia amegundua shauku inayoongezeka katika mahusiano ya wazi ndani ya muongo mmoja uliopita.
"Ilikuwa kitu ambacho hakijulikani sana miaka 10 iliyopita, na sasa ni jambo la kawaida kabisa," anasema.
Hayo pamoja na baadhi ya data zinaonyesha shauku inayoongezeka katika mahusiano yasiyo ya mke mmoja, ikiwa ni pamoja na mahusiano ya wazi.
Wataalamu wanasema mambo mengi ya kijamii na kitamaduni ambayo yamesababisha kukumbatia kwa mitindo isiyo ya kitamaduni katika mahusiano, pamoja na janga la corona kuna uwezekano yamechangia katika hali ilivyo sasa.
Lakini ingawa hamu ya mahusiano ya wazi inaweza kuongezeka, mawazo ya wataalam yametofautiana kuhusiana na jinsi inavyoweza kutekelezwa - pengine kwa sasa.
Uhusiano wa wazi ukoje?
Kuna njia nyingi za kushiriki katika kutokuwa na mke mmoja, anasema Levinson.
"Inaweza kuwa chochote kuanzia kuishi na wapenzi wengi na kugawana fedha, au inaweza kuwa kusaidia mpenzi wako mara moja kwa mwaka au kumpa tiketi ya kuingia kwenye mkutano wa kazi ili upate fursa ya kuwa naye."
Mahusiano ya wazi yako chini ya uhusiano unaohusisha kuwa na zaidi ya mke mmoja, lakini wengi huwa na tofauti kati ya aina hizo za mipangilio na aina nyingine za uhusiano kama vile uhusiano wa zaidi ya mtu mmoja lakini wahusika wote wanajua ilhali mahusiano ya wazi mara nyingi huhusishwa na watu wanaojihusisha kimsingi na mahusiano ya kimapenzi nje ya ubia wao uliopewa kipaumbele, wa watu wawili.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa wengine, hii inamaanisha kwenda nje pamoja kama kawaida tu na kuwa na uhusiano wa aina ya 'marafiki-wenye-manufaa' na watu wengine mbali na wenzi wao wa halali.
Kwa wengine, uhusiano wa wazi unamaanisha tu kwamba kuna wakati pengine mutatoka kama mara moja tu kwenda mahali kusherehekea pamoja au kwa ajili ya kushiriki mapenzi kwa kipindi kifupi tu. Na kwa wengine bado, mpangilio huo unaweza kuonekana zaidi kwenye kushiriki mapenzi na wengine kama wanandoa, lakini si kwenda kujivinjari pamoja.
Winston pia anazungumzia uhusiano wa “usiulize wala kuseme kitu”- mtindo wa mahusiano ya wazi, ambapo wanandoa wote wanamruhusu mwingine kushiriki ngono na watu wengine – bila kujadili matukio hayo pamoja.
Pia kuna mahusiano mengine, kama vile "monogamish", ambayo mwandishi wa habari aliyebobea katika mahusiano wa Marekani Dan Savage aliyapatia umaarufu miaka kadhaa iliyopita, yanaweza kuingiliana baadhi ya mipangilio ya mahusiano ya wazi.
Savage amezungumzia uhusiano wake wa kuwa na mke mmoja kwenye podcast yake, ambapo yeye na mpenzi wake wamejitolea kwa kila mmoja wao, lakini bado wanashiriki ngono katika uhusiano mwingine ambao sio wa kujitolea na watu wengine.
Miongoni mwa wateja wa Winston, wasikilizaji wa podikasti na watembeleaji wa tovuti, amepata wengi wanaovutiwa au kushiriki katika mahusiano ya wazi huwa wanaonekana kuwa wadogo - kati ya umri wa miaka 25 na 45.
Hata hivyo, katika kazi yake, ameshirikiana na wateja wanaopenda au wanaoshiriki mahusiano ya wazi ambao wana umri wa miaka 19 na pia wwenye umri wa miaka 70.
'Shauku inayoongezeka'
Programu za kuchumbiana husaidia kuangazia ongezeko la shauku ya mahusiano ya wazi.
Kwanza, kumeibuka majukwaa yanayolenga hasa kutokuwa na mke mmoja, ikiwa ni pamoja na mahusiano ya wazi, ili kushughulikia shauku inayoongezeka.
Lakini hata programu za kitamaduni za kuchumbiana, kama vile OkCupid, zimeshuhudia ongezeko la nia katika mahusiano ya wazi.
Zaidi ya hayo, data ya 2022 kutoka kwa programu ya kuchumbiana Hinge ilionyesha mtumiaji mmoja kati ya watano wa Hinge "angezingatia" kujaribu uhusiano a wazi, wakati mmoja kati ya 10 tayari amejihusisha na mahusiano hayo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Hinge Logan Ury anasema kunaweza kuwa na athari ya janga la corona, kwani anaamini ilikuwa "fursa nzuri ya kutulia na kufikiria zaidi juu ya kile tunachotaka."
Washauri na wataalamu ikiwa ni pamoja na Levinson na Winston pia wameshuhudia ongezeko la shauku juu ya uhusiano wa wazi.
Winston anasema kwamba mambo mengi ya hivi majuzi ambayo ameyaona katika mahusiano ya wazi yanatoka kwa watu wa milenia ambao "wanahoji tu jinsi walivyolelewa" - mara nyingi, kuamini kwamba ndoa ya muda mrefu, ndoa ya mke mmoja ni lengo la mwisho la mahusiano ya karibu.
Kijamii, sote tuko wazi zaidi kwa kila aina ya utambulisho ambao si wa kawaida ... watu wako tayari zaidi kupinga miundo ya jamii kwa njia ya jumla."
"Hii imefungua mlango kwa watu kuhoji matamanio yao wenyewe, pia.
"Wakati unaendelea kuchagua ndoa ya mke mmoja na haifanyi kazi ... unaanza kuwa na hamu kuhusu [kama] kuna njia nyingine," Levinson anasema.
Na kwa wale ambao wana shauku, kuna rasilimali zaidi kuliko hapo awali.
Pamoja na "mlipuko wa hamu au nia" katika mahusiano ya wazi, anaongeza Winston, kuna "mlipuko katika watengenezaji maudhui na watu wanaoandika kuhusu mahusiano hayo kwenye vyombo vya habari… katika programu na hata katika mikutano ya jumuiya".
Hii ina maana kwamba taarifa kuhusu kutokuwa na mke mmoja hupatikana kwa wingi - si katika "[majarida ya kibinafsi ya mtandaoni] pembezoni", ambapo Winston anasema alihitaji kutafuta habari zaidi ya muongo mmoja uliopita.
Mahusiano hayo yanaonekana kuwa ndoto zaidi kuliko uhalisia wa maisha?
Licha ya watu wengi kukumbatia mipango isiyo ya mke mmoja, na kuongezeka kwa shauku kuhusu mahusiano ya wazi, mtazamo wa jumla bado kwa kiasi kikubwa ni hasi.
"Kura za uchunguzi na maoni ya umma zinaonyesha kuwa mitazamo kuhusu kuwa na mke zaidi ya mmoja kwa kawaida ni mbaya kwa jumla, ingawa inaonekana kuwa na mwelekeo mzuri zaidi katika miaka ya hivi karibuni," anasema Dk Justin Lehmiller, mtafiti mwenza wa Taasisi ya Kinsey na mwenyeji wa kipindi cha Sex and Psychology kupitia Podcast.
Ingawa mitazamo hiyo hasi haiwezi kuwazuia watu kufikiria kuwa katika mahusiano ya wazi, inaweza kuwazuia kujihusisha nayo.
Katika utafiti wake kuhusu mawazo ya mapenzi, kwa mfano, Lehmiller amegundua kwamba "watu wengi wamefikiria kuhusu kutokuwa na mke mmoja kwa njia fulani hapo awali, kama vile kuwa na uhusiano mwingine".
Hata hivyo, anaongeza, "ni wachache wanaoshiriki mahuasiano ya wazi katika maisha halisi".
Ingawa hakuna data ya baada ya janga la corona inayoonesha jinsi watu wengi wako katika mipango hii, utafiti wa Canada kutoka 2019 unaweka takwimu hiyo karibu 4%, na takwimu kama hiyo ikiibuka katika utafiti wa 2018 wa Marekani.
Levinson anaamini kuwa hii inaweza kwa kiasi fulani kutokana na mtazamo ulioimarishwa kwamba mahusiano ya wazi yanaonekana kwa ujumla kuwa 'yasiofaa'.
Anaongeza kuwa imani za kidini pia zinaweza kuzuia watu kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na/au kuchumbiana na zaidi ya mtu mmoja kwa wakati mmoja, kama vile kanuni za kitamaduni za jamii fulani zinavyoweza.
Ingawa Levinson anakubali kutakuwa na ongezeko linaloendelea la "miundo bunifu ya uhusiano huu", hafikirii kuwa itakuwa janga duniani.
Tamaduni nyingi sana ulimwenguni huleta changamoto kwa watu wanaotarajia kuanzisha uhusiano wa wazi na mwiko unasalia kuwepo kwa kiasi kikubwa ulimwenguni.















