Trevor Jacob: Akiri kuangusha ndege makusudi kwa ajili ya kupata wafuasi YouTube

Chanzo cha picha, TREVOR JACOB
Mwana YouTube ambaye aliangusha ndege kimakusudi ili kutazamwa na wafuasi wake mtandaoni ataingia kwenye hatia ya shtaka la kuzuia uchunguzi wa serikali kwa kusafisha eneo la ajali, waendesha mashtaka wa Marekani wanasema.
Trevor Jacob, 29, alichapisha video ya ajali ya ndege kwenye YouTube mnamo Desemba 2021, Imetazamwa na zaidi ya watu milioni 2.9 hadi sasa.
Katika makubaliano yake na waendesha mashtaka kuhusu kukukiri makosa, alisema alirekodi video kama sehemu ya mpango wake wa udhamini wa moja ya bidhaa.
Anaweza kufungwa jela hadi miaka 20.
Rubani huyo mwenye umri wa miaka 29 amekubali kukiri kosa moja la uharibifu na kuficha kwa nia ya kuzuia uchunguzi wa serikali, idara ya haki ya Marekani ilisema katika taarifa yake siku ya Alhamisi.
Mnamo Novemba 2021, Bw Jacob aliondoka kwenye uwanja wa ndege wa Santa Barbara, California kwa ndege ya mtu mmoja huku kamera zikiwa zimepachikwa kwenye ndege yake. Pamoja na kamera, Bw Jacob alikuwa na parachuti, pamoja na fimbo ya kuchukulia picha za 'selfie'.
"Hakuwa na nia ya kufika alikoenda, lakini badala yake alipanga kuidondosha ndege yake wakati wa safari na kupiga picha za video akiruka kwa parachuti chini kabla ya ndege yake kuanguka", Ofisi ya Mwanasheria wa Marekani katika Wilaya ya Kati ya California ilisema.

Chanzo cha picha, TREVOR JACOB
Ndege hiyo ilianguka kwenye Msitu wa Kitaifa wa Los Padres dakika 35 baada ya kupaa. Kabla ya kurudi eneo la tukio la kuchukua picha.
Baadhi ya watazamaji wa YouTube walikuwa na mashaka kuhusu ajali hiyo, wakibaini kuwa Bw Jacob alikuwa tayari amevalia parachuti na hakujaribu kutua kwa usalama.
Aliripoti ajali hiyo kwa Bodi ya Kitaifa ya Usalama wa Uchukuzi, ambaye alisema alikuwa na jukumu la kuhifadhi mabaki hayo. Kulingana na makubaliano yake na waendesha mashtaka, Bw Jacob baadaye alidai kuwa hakujua eneo la tukio.
Alikuwa anajua, alirudi kwa helikopta akiondoka na mabaki, ambayo baadaye aliyaharibu, taarifa inasema.
Bw Jacob anatarajiwa kufika Mahakamni kwa mara ya kwanza wiki chache zijazo.
Leseni yake ya urubani ilifutwa mwaka jana.
Wakili wa Bw Jacob hajajibu ombi la BBC la kutaka maoni yake.

Chanzo cha picha, TREVOR JACOB












