Pardon Modest: Mtengeneza gitaa wa kipekee Tanzania

Maelezo ya video, Pardon Modest: Mtengeneza gitaa wa kipekee Tanzania
Pardon Modest: Mtengeneza gitaa wa kipekee Tanzania
Iliyochapishwa

Mjasiriamali mmoja nchini Tanzania, Pardon Modest amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na kipaji alichonacho cha kuunda magitaa ya umeme kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini humo ikiwemo mbao, nyaya na vipuri mbalimbali.

Sambamba ameweza kutengeneza fursa kwa vijana kwa kuwafundisha stadi hiyo lakini pia jinsi ya kuvitumia.

Mwandishi wa BBC, Alfred Lasteck alimtembelea mtaalamu huyo.