Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi: Klabu tatu za Saudia zinasubiri kwa hamu kumchukua kwa mkopo Rashford

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rashford
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester United wanafikiria kuidhinisha kuondoka kwa mkopo kwa mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, mwezi Januari. (Sun)

Klabu tatu za Saudi Arabia, Al Ahli , Al Ittihad na Al Qadsiah , zote zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili Rashford. (Sport)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Dele Alli

Kiungo wa kati wa Uingereza Dele Alli, 28, anatumai kufufua soka lake nchini Italia na klabu ya Serie A ya Como baada ya kutangaza kuondoka Everton. (Telegraph)

Chelsea wana nia ya kumsajili mlindalango wa Uswizi Gregor Kobel, 27, kutoka Borussia Dortmund . (Florian Plettenberg)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Franco Mastantuono

Manchester United inamfuatilia kiungo wa kati wa River Plate Muargentina Franco Mastantuono, 17, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa katika mkataba wake cha takriban £38m. (Give Me Sport)

Mchezaji wa kimataifa wa Newcastle na Brazil Bruno Guimaraes, 27, na Real Sociedad na kiungo mwenza wa Uhispania Martin Zubimendi, 25, ndio walengwa wakuu wa Manchester City Januari. (Team Talk)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tijjani Reijnders

Kiungo wa kati wa Uholanzi Tijjani Reijnders, 26, ambaye amekuwa akihusishwa na taarifa za kuhamia Manchester City, anakaribia kuafiki mkataba mpya AC Milan . (Football Insider)

Beki wa kushoto wa Paraguay Diego Leon, 17, atajiunga na Manchester United wakati Cerro Porteno atakapofikisha umri wa miaka 18 mwezi Julai. (Fabrizio Romano)

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Virgil van Dijk

Real Madrid wameorodhesha mlinzi wa kati wa Liverpool na Uholanzi Virgil van Dijk, 33, kama mmoja wa wanaoweza kuchukua nafasi ya beki wa Austria David Alaba, 32, na mlinzi wa kati wa Brazil Eder Militao, 26. (Football Transfers)

Beki wa kushoto wa Bayern Munich na Canada Alphonso Davies, 24, ambaye amewavutia Manchester United na Real Madrid, yuko tayari kuhama kutoka klabu hiyo ya Ujerumani kwenda Liverpool. (Caughtoffside)

Paris St-Germain wanavutiwa na mlinzi wa kimataifa wa Ukraine wa Bournemouth Illia Zabarnyi, 22. (L'Equipe - in French)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Dominic Calvert-Lewin

Mshambuliaji wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 27, ambaye mkataba wake na Everton unamalizika Juni 2025, analengwa na Fiorentina Januari. (Gianluca Di Marzio)

Klabu ya Brazil Palmeiras imetuma pendekezo la awali kwa Fulham kuhusu usajili wa kiungo wa kati wa Brazil Andreas Pereira, 28. (Fabrizio Romano)

Meneja wa Chelsea Enzo Maresca anataka kumbakisha mshambuliaji wa Uhispania Marc Guiu mwezi ujao lakini itategemea iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 anataka kuhama kwa mkopo. (Standard)

Kiungo wa kati Muitalia Cesare Casadei, 21, anapanga kuondoka Chelsea mweziJanuari, akitarajiwa zaidi kuelekea Serie A . (Fabrizio Romano)

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi