Uchaguzi Kenya: Familia ya Afisa wa Tume aliyeuawa wataka wahusika wakamatwe
Uchaguzi Kenya: Familia ya Afisa wa Tume aliyeuawa wataka wahusika wakamatwe
Iliyochapishwa
Familia ya Afisa Msimamizi wa Uchaguzi wa tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC aliyeuawa, Daniel Musyoka wanataka serikali iwakamate na kuwafungulia mashtaka waliomuua.
Musyoka alitoweka asubuhi ya Agosti 11 katika kituo cha kuhesabia kura cha Embakasi Mashariki baada ya kuripotiwa kujiepusha kupiga simu ya faragha.
Mwandishi wetu Regina Mziwanda amezungumza na msemaji wa familia hiyo ya Daniel Musyoka, Jackson Muimi ambaye ni shemeji wa marehemu.