Kwanini watoto wanaua kuku shuleni Kenya?
Na Evelyne Musambi
BBC News, Nairobi

Chanzo cha picha, Getty Images
Picha ya video iliyosambaa inawaonyesha wanafunzi wa shule ya msingi wakiwachinja kuku nchini nchini Kenya imesababisha malalamiko na baadhi ya mizaha ya kuchekesha kuhusu mtaala mpya wa nchi hiyo ambao unaangazia zaidi ujuzi halisi kivitendo.
Wakati wa somo la nje ya darasa kwa ajili ya wanafunzi wa miaka 11kuhusu jinsi ya kumchinja na kumpika kuku, mvulana mmoja anaonekana akimkandamiza chini jogoo chini huku mwingine aliyeshikilia kisu kwenye shingo ya kuku akionekana mwenye hofu.
Baadhi ya wanafunzi wenzake waliokuwa makini wakitazama huku mwalimu, ambaye anachukua picha za tukio kwa simu, akimsifia mvulana kwa kukata kichwa na halafu akamuelekeza mwingine, ambaye anashikilia kiwili wili cha kuku, ili kukiweka katika sururia ya maji yanayochemka.
Lakini wakati mtoto alipokuwa akielekea kwenye chungu, kuku asiyekuwa na kichwa alianga kupiga mabawa yake na kutoroka.
Video ya sekunde 19 inaishia kwa kicheko cha mwalimu wakati kuku asiye na kichwa akiendelea kukimbia huku watoto wakipiga kelele wakimkimbiza.
Wakati kichwa cha kuku kinapokatwa, kuku anaweza kukimbia kwa dakika kadhaa kwa muda ambao uti wake wa mgongo unakua bado una hewa ya oksijeni. Ni kitu ambacho wanafunzi wa darasa la sita huenda wasisahau
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Video hiyo iliibua malalamiko kwenye mitandao ya kijamii huku watu wengi wakihofia usalama wa watoto, ingawa hakuna yeyote aliyezungumzia kuhusu kuumia kwa kuku, kwani katika maeno ya vijijini nchini Kenya ni jambo la kawaida kuona kuku wakichinjwa.
Tangu waanze shule ya msingi, wamekuwa wakitumika kufanyiwa utafiti kwa ajili ya mtaala mpya, na wamepitia mitradi mbali mbali ya kivitendo kwa kipindi cha miaka michache iliyopita – kuanzia kutengeneza sanamu za kuwatisha ndege wanaoharibu mimea hadi kuuza bidhaa kwenye masoko .
Wanaounga mkono mtaala wenye msingi wa ujuzi - Competency Based Curriculum (CBC) wanawaona zaidi kama waanzilishi, wakisema ni uboreshaji wa nadharia za zamani – na mfumo wenye msingi wa mtihani kwani unawaandaa zaidi kwa ajili ya maisha na kupata ajira katika karne ya 21.
Pia walidai kuwa kwasababu kuna tathmini inayoendelea itapunguza udanganyifu katika mitihani, ambao umekuwa ni tatizo kubwa kwa serikali.
Takriban wanafunzi milioni 1.25 wa darasa la sita watafanya mtihani karibuni kama sehemu ya kupata cheti cha kumaliza shule ya msingi ambacho kinatoa fursa ya mwanafunzi kujiunga na shule ya sekondari.
Kwa mara ya kwanza, mtihani utachangia 40% ya maksi za mtihani wao wa mwisho kwani alama za mitihani ya tathmini waliyoifanya tangu darasa la kwanza itachangia 60% zilizosalia.
'Karamu kwa ‘gharama’ ya wazazi
Lakini baadhi ya wazazi hawafurahishwi na gharama ya mtaala mpya kwani shule huwategemea kuchangia zana na fedha kwa ajili ya vitu kama – kuku – wanaohitajika kwa ajili ya kujifunza kwa vitendo.
Mwalimu wa sayansi kimu katika Shule ya Msingi ya Kangundo mashariki mwa Kenya anasema wale wanaotoka katika familia zenye kipato cha chini wakati mwingine wanalazimishwa kuwatazama wenzao wakijifunza kwa vitendo.
"Wanafunzi wangu wa darasa la tano, kwa mfano, walikuwa wakishona leso kwa ajili ya mradi na baadhi hawakuwa na uwezo wa kununua kitambaa, kwahiyo tuliishia kutumia vichache ambavyo vilinunuliwa na baadhi ya wanafunzi," Jemimah Gitari aliiambia BBC.

Anahisi baadhi ya waalimu wenzake hutumia fursa ya mtaala mpya – kuwaambia wanafunzi walete nyama, lakini anasema hii kusema kweli sio lazima kuleta nyama kwa ajili ya mradi wa kupiga supu ya nyama.
"Shule yangu iko kijijini ambako baadhi ya familia haziwezi hata kumudu mlo kutokana na kupanda kwa gharama ya chakula kwahiyo nisingewataka walete nyama," alisema.
Kufuatia somo la vitendo la kuku – lililofanywa na wanafunzi wa darasa la sita kote nchini mwezi Septemba – picha zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii ambazo zionyesha waalimu wakionekana kula kuku katika ofisi za waalimu.
Mbunge kutoka magharibi mwa Kenya, Didmus Barasa, aliwashutumu kwa kufanya karamu kwa chakula kilicholipiwa na wazazi ambao hawana uwezo wa kukinunua.
"Sasa hakuna kuku kwenye nyumba za watu" alisema katika kauli iliyokasirisha muungano wa waalimu.
Mjadala mkali wa kuku hata uliyafikia masikio ya rais mpya wa Kenya Rais William Ruto, ambaye ameweka kamati ya kikosi kazi cha wajumbe 49, kitakachotathmini mtaala mpya, ambao ulikuwa mradi mdogo wwa mtangulizi wake, Uhuru Kenyatta.
Wajumbe wa kamati hiyo wana hadi kufikia mwisho wa mwaka huu kutoa mapendekezo kuhusu iwapo mtaala wa CBC unaweza kuendelea kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la sita kuweza kuendelea katika elimu ya sekondari, ambao wanatarajia kuanza mwezi Januari.
"Vitabu na mtaala vilivyotayarishwa viko tayari lakini tunasubiri ushauri kabla ya kuvisambaza," Profesa Charles Ong'ondo, ambaye anaongoza Taasisi ya Kenya ya maendeleo ya mtaala (The Kenya Institute of Curriculum Development), aliiambia BBC.
Baadhi ya wazazi hawana tatizo na suala la wanafunzi kujifunza kwa vitendo, lakini wanasema mtaala unakosa uwiano kwani kazi za vitabuni ni kidogo.
"Mwanangu, ambaye yuko darasa la nee, anafanya masomo 12 na kila somo lina mradi wa kufanya. Walitumia muda wao mwingi wa masomo katika muhula uliopita wakifanya miradi na kwahiyo kazi za darasani hazikufanywa ," Rozina Kisilu, mama wa watoto wawili anayeishi Nairobi, aliiambia BBC.
Lengo la masomo kwa vitendo linaifanya kazi ya mwalimu kumaliza mtaala kwa muda uliopangwa kuwa ngumu, anaongeza Bi Gitari – akielezea kuvurugwa kwa masomo kwa wiki mbili kulikotokea muhula uliopita kwasababu ya uchaguzi mkuu.
Miaka miwili iliyopita kusema kweli imekuwa sio ya kawaida, huku wanafunzi wakisoma kwa mihula mitatu badala ya minne ili kusoma masomo yaliyositishwa kutokana na janga la Covid.
Wengine wanasai kuwa itachukua muda kwa waalimu kuzowea mtaala mpya.
Hii pia inakuja wakati hivi karibuni kukiwa na ukosoaji wa video kadhaa zilizosambazwa mitandaoni za watoto wa shuke katika maeneo ya vijijini wakionekana wamelala chini wakijifanya wanaogelea kwasababu hawakuwa na dimbwi la kuogolea.
Lakini mwalimu mjini Nairobi Marion Muthoni anasema miradi ya masomo ya shughuli za mwili inawapatia uhuru waalimu wa kuchagua: wanafunzi wanaweza kuogelea au kuruka kwa kutumia kamba kulingana vifaa walivyo navyo.
"Baadhi ya waalimu wenzangu wanazidisha tu vitu vingine. Vitu ambavyo nimekuwa nikiviona kwenye mitandao ya kijamii ni tofauti sana na mwongozo tulionao. Kadri muta utakavyokwenda waalimu watagundua kuwa sio kila kitu kinahitaji kufanwa kwa vitendo " Bi Muthoni aliiambia BBC.

Waalimu wanasema wanasema kuwa wanahitaji muda zaidi kutekeleza mtaala mpya.
Pendekezo lililotolewa na Chama cha waalimu nchini Kenya (KNUT) baada ya majaribio ya miaka miwili ya mtaala mpya ni kwamba CBC haupaswi kuanzishwa kote hadi walimu watakapopewa mafuzo yanayofaa.
Baadhi ya wataalamu wa elimu walipendekeza kwamba wanafunzi waliofanyiwa majaribio ya mtaala huu wanapaswa kumaliza mzungumo kabla ya kuanzishwa kwa mfumo kamili kote nchini ili marekebisho yaweze kufanyika.
Sophia Mbevi, mkurugenzi wa shule za kibinafsi mjini Nairobi, anaafiki, akisema kuwa japokuwa CBC ilikuwa na malengo mazuri, iutekelezwaji wake uliharakishwa.
Shule yake hutoa mtaala mbadala – ambapo chini ya sheria ya Kenya inaruhusiwa kwa kwa taasisi za kibinafsi ili mradi uwe umeidhinishwa na idara ya elimu.
Baadhi ya wazazi wenye uwezo wanachagua kuwapeleka watoto wao katika shule binafsi zenye mitaala iliyodumu, sawa na shule anayoiongoza Bi mbevi, kwasababu hawataki hali ya baadaye ya watoto wao iwe ya kufanyiwa majaribio.















