Je, ni umri gani sahihi wa kuwa mama na madaktari wanasema nini kuhusu hili?

w

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Baadhi ya maswali hayana majibu ya uhakika. Yana majibu mengi. Hutofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Hata hivyo, maswali hayaishi na hivyo kufanya majibu yake kuwa mengi pia.

Mojawapo ya maswali hayo muhimu ni umri gani unaofaa wa kuwa mama?

Pooja Khade Pathak anaishi katika Pune. Anafanya kazi katika sekta ya usimamizi wa wafanyakazi. Aliamua kuwa mwanamke akiwa na umri wa miaka 23 anatosha kuwa mama .

Leo ana umri wa miaka 33 na binti yake ana umri wa miaka 10. Alisema uamuzi huo umechukuliwa kwa umakini. Kulingana naye, "Kuna ushindani katika kila sekta, kuna ngazi za uongozi. Kazi yangu haikuwa na ugumu sana na kisha nilifikiri kwamba ikiwa nitapumzika katika kazi yangu, nitapata fursa zaidi za kusonga mbele.

Ni afadhali kuwa mama kwanza kuliko kupata uraibu wa kufanya kazi na kuiachia katikati." Nilikuwa nafikiri hivyo."

"Kitu cha pili nilichofikiria ni afya. Katika umri wa miaka 23, afya yangu ilikuwa katika hali nzuri. Nilihisi kwamba ningeweza kushughulikia mafadhaiko yote na uvumilivu vizuri sana.

Wazo lingine lilikuwa kwamba sikutaka pengo la kizazi kati ya watoto wangu na mimi. Uamuzi huo ulichukuliwa.

Je, kuna umri sahihi wa kuwa mama?

Kitaalam, hili ni suala la kibinafsi sana. Lakini ukizungumzia suala la kimatibabu, kuna vita tofauti. Kulingana na Daktari bingwa wa magonjwa ya akili Dkt. Nandini Palshetkar, umri wa kati ya miaka 25-35 ni umri bora wa kuwa mama.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Anasema, "Kuna matatizo mengi ya kuwa mama baada ya miaka 35. Kwa hiyo, miaka 25 hadi 35 ni miaka 10 inayofaa.

Ikiwa unajaribu kupata ujauzito baada ya miaka 35, ni vigumu sana. Siku hizi, ndoa zinachelewa.

Baada ya hapo, wakati mwingine uamuzi huchukuliwa wa kuwa mama. Lakini kwa kuzingatia hali ya sasa, wasichana wanapaswa kuwa makini sana. Wanapaswa kufanya uchunguzi wa uwazi wa uzazi.

Kuna kipimo kinachoitwa AMH (homoni ya Anti Mullerian) ambapo Idadi ya mayai ya uzazi ya mwanamke inajulikana iwapo inaweza kutapungua, au kuna hatari kuyahusu. Kwa hiyo, wasichana wanapaswa kuwa makini."

Dr Chaitanya Shembekar ni mtaalamu maarufu wa magonjwa ya wanawake huko Nagpur ambaye anasema , umri bora wa kuwa mama ni 25 hadi 30.

"Wagonjwa wanaokuja kwetu kwa ajili ya kupata hudumua ya uzazi wa kusaidiwa (IVF) huwa wamepungukiwa na hifadhi ya ovari (mfuko wa mayai ya uzazi) wanapofikia umri wa miaka 30," anasema.

Katika umri wa miaka 32, huwa wamepungukiwa sana na mayai ya uzazi . Kwa sasa tunafuata mtindo wa Magharibi ambapo , msisitizo umewekwa kwenye kazi zaidi

Kwa hiyo, ni tatizo kubwa. Nina maoni thabiti kwamba bila kujali ni watoto wangapi wanataka, mtu anapaswa kujifungua katika kipindi hiki."

h

Chanzo cha picha, POOJA PATHAK

Dr Palshetkar anaendelea, "Uzee wa ovari ni tatizo kubwa siku hizi. Asilimia 30 ya wasichana wanaokuja kliniki yangu wana tatizo hili.

Kuna ndoa za marehemu. Baadaye aliamua kuzaa mtoto. Siku hizi, chaguo la kufungia mayai pia linapatikana.

Chaguo hili pia linakubaliwa na wasichana wengi. Lakini kuna ubaguzi. Lakini nadhani umri wa miaka 25 hadi 35 ni umri sahihi wa kuwa mama."

Dr. ni ya maoni kwamba chaguo la kufungia mayai haifai sana. Schembaker inaonyesha. Kumekuwa na wimbi la hivi karibuni la kufungia yai.

Makampuni mengi makubwa pia hutoa bima kwa ajili yake. Lakini sio tu ovari lakini pia umri wa mwanamke unapaswa kuzingatiwa hapa.

Unapokuwa na umri, mwili wako una mapungufu.

Uvumilivu ni mkubwa zaidi katika umri mdogo. Uwezo wa kimwili ni wa juu.

Inasemekana kuwa kuzaa ni kuzaliwa kwa pili kwa mwanamke. Kwa sababu matatizo kama kisukari, shinikizo la damu mara nyingi hutokea wakati wa ujauzito. Kwa hivyo ukiolewa mapema na kujifungua mtoto mapema, matatizo haya yataepukwa, anasema Dk. Shembaker.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Dk Palshetkar anaendelea kusema kuwa , "Uzee wa ovari ni tatizo kubwa siku hizi. Asilimia 30 ya wasichana wanaokuja kliniki yangu wakiwa na tatizo hili.

Kuna ndoa za marehemu, ambapo watu huamua kuzaa mtoto kwa kutumia mbegu za uzazi za watu waliofariki. Siku hizi, chaguo la kutunza mayai ya uzazu pia linapatikana.

Chaguo hili pia linakubaliwa na wasichana wengi, lakini nadhani umri wa miaka 25 hadi 35 ni umri sahihi wa kuwa mama."

Kwa maoni ya Dk. Ni kwamba chaguo la kuhifadhi mayai ya uzazi halifai sana.

Makampuni mengi makubwa pia hutoa bima kwa ajili yake. Lakini sio tu ovari lakini pia umri wa mwanamke unapaswa kuzingatiwa hapa.

Kadri unapovyokuwa na umri mkubwa, mwili wako unakuwa na mapungufu. Uvumilivu ni mkubwa zaidi katika umri mdogo. Uwezo wa kimwili pia ni wa juu.

Inasemekana kuwa kuzaa ni kuzaliwa kwa pili kwa mwanamke. Kwa sababu matatizo kama kisukari, shinikizo la damu mara nyingi hutokea wakati wa ujauzito. Kwa hivyo ukiolewa mapema na kujifungua mtoto mapema, matatizo haya yataepukwa, anasema Dk. Shembaker.

Kuchelewa kupata mtoto...

Rita Joshi ni mzaliwa wa Mumbai. Anafanya kazi katika sekta ya teknolojia ya mawasiliano ,IT. Alikuwa na shughuli nyingi katika kazi yake katika umri ambao kijamii ni umri wa kuolewa.

Mara nyingi walilazimika kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kufanya kazi. Alifunga ndoa akiwa na umri wa miaka 35 kutokana na sababu nyingi. Baada ya kufunga ndoa, walijaribu sana kupata mtoto kwa njia ya kawaida, lakini hawakufanikiwa.

w

Chanzo cha picha, Getty Images

Baadaye, alijaribu kutumia njia ya IUI, IVF, lakini hakuwa na wakati wa kufanya hivyo kwa sababu ya kazi yake.

Hatimaye mnamo Oktoba 2020 alibeba mimba kwa njia ya IVF. Kwa kuongezea, kwa sababu ya kufanya kazi wakat iwa sheria za corona za kufanyia kazi nyumbani, aliweza kutumia muda unaohitajika kwa matibabu haya na mwishowe akawa mama wa msichana mzuri.

Hadithi ya Rita Joshi ya ndoa ya kuchelewa kutokana na kazi na hivyo basi kuchelewa kupata mtoto sio ya kipekee kwa Rita Joshi.

Kwa nini umri wa wanawake ni muhimu?

Umri wa wanawake ni muhimu kwa sababu ya idadi ya mayai ya uzazi aliyonayo. Kwa miongo kadhaa iliyopita, wanasayansi wamegundua kuwa idadi ya mayai katika mfuko wa uzazi wa wanawake hupungua kadri umri unaoongezeka.

Mamilioni ya mbegu za kiume huzalishwa kwa wanaume kila siku. Wanawake wanapozaliwa huwa na mayai milioni 1.

Kufikia wakati wa hedhi , idadi hiyo hufikia 3,000,000. Kwa umri wa miaka 37 idadi hii inakuwa 25,000 na kwa umri wa miaka 51 idadi hii hufikia 1000. Kati ya hayo mayai yenye uwezo wa kuzalisha huwa ni 300 hadi 400 tu.

Kadiri idadi ya mayai inavyopungua umri unavyoongezeka, ubora wa jeni za urithi na ubora wa vinasaba-DNA katika mayai pia hupungua.

Wasichana huanza hedhi wakiwa na umri wa miaka 13. Katika mwaka wa kwanza au miwili, yai huwa halina uwezo mkubwa wa kukomaa.

Uzazi wa wanawake wengi huishia miaka minane kabla ya ukomo wa hedhi.

Iligundulika kuwa idadi ya mayai katika ovari inategemea hali ya maumbile, anasema Andrea Jurisikova daktari wa uzazi ambaye amefanya utafiti.

Lakini idadi ya mayai pia inategemea kuongezeka kwa maisha ya wanawake. Idadi ya mayai pia inategemea yatokanayo na kemikali zenye sumu, mafadhaiko.

Pamoja na wingi, ubora wa mayai pia ni suala muhimu. Ubora huu pia hupungua kwa umri unaoongezeka.

Umuhimu wa Chromosomes (Jeni za urithi)

Chromosomes pia ina jukumu muhimu katika uzazi. Kulingana na watafiti, hata kama kuna shida katika kromosomu, kuna vikwazo katika uzazi. Kwa kweli, kuna baadhi ya kasoro katika chromosomes. Wanawake wengi wana kasoro zao.

Kwa kawaida tatizo hili ni la kiwango cha chini kwa kwa wanawake vijana. Lakini uwezekano kufeli kwa utendaji wake huongezeka kadri umri unavyoendelea kuongezeka.

Upungufu wa Chromosom haimaanishi kuwa wanawake hawawezi kupata watoto. Hata hivyo, uwezekano wa mtoto mwenye afya kuzaliwa kutokana na yai linalozalishwa wakati wa hedhi ni mdogo.

Upande wa kijamii

Akizungumzia hali ya sasa ya kijamii kuhusu kuzaa watoto, Dk anasema, "Siku hizi, hakuna mtu anayefikiria ndoa akiwa na umri wa miaka 25.

Mwanamke anaolewa na kisha anafikiri kwamba tutakuwa na mtoto wakati wowote tunapotaka. Wanafikiri kuwa kwa umri wa miaka 30 bado ni ni vijana sana.

Lakini hawajui kabisa kwamba kwa wakati huo hifadhi ya homoni imepungua kabisa. Wasichana huzingatia kazi zao, kisha kuchelewesha ndoa na kisha tatizo linalofuata linatokea."

Mume wa Pooja Khade-Pathak alifariki miaka michache iliyopita. Kwa sasa ni mzazi mmoja. Kwa sababu ya uzazi wa mapema, binti yake amekuwa na ana utunzaji mdogo kwa binti yake.

Rita, kwa upande mwingine, ameupokea kwa furaha uzazi wa mapema.

Uamuzi wa kuwa mama ni mkubwa, unaobadilisha maisha. Ikiwa ni kuchukuliwa kwa wakati sahihi, maisha yanaweza kuwa mazuri kabisa.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi