"Wakiona ninaanza kuwasha injini wanashangaa"- Mwanamke nahodha wa boti
"Wakiona ninaanza kuwasha injini wanashangaa"- Mwanamke nahodha wa boti

Iliyochapishwa
Si jambo la kawaida kukutana na mwanamke akifanya kazi zinazodaiwa na kuaminika kwamba ni za wanaume tu. Kazi hizo ni kama vile udereva,urubani,ufundi na kazi nyingine.
Katika hali inayokwenda kinyume kabisa na dhana hiyo huko visiwani zanzibar Bi. Bahati Suleiman ni nahodha wa boti ya kutembeza watalii na amekuwa akifanya kazi hiyo kwa takribani miaka 25 hadi sasa.
Mwandishi wa BBC Esther Namuhisa alifika visiwani humo ili kuweza kujua ni kwa namna gani mwanamke huyu alithubutu kujitumbukiza katika kazi hiyo:
Video ;Eagan Salla



