Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kufunguliwa kwa mikutano ya hadhara ya siasa Tanzania: 'Tumepokea kwa tahadhari' - Wapinzani
Iliyochapishwa
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu ameruhusu mikutano ya vyama vya siasa baada ya marufuku ya miaka zaidi ya 6 iliyowekwa na mtangulizi wake, hayati John Magufuli. Lakini wapinzani wamepokea kwa tahadhari hatua hiyo, kama walivyozungumza na BBC Ikulu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya mkutano wa Rais Samia na viongozi wa vyama vyote 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu nchini humo.