Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kundi la kwanza la familia 27 waliokuwa wakiishi hifadhini Ngorongoro limeondoka leo
Kundi la kwanza la wananchi waliokuwa wakiishi ndani ya hifadhi ya Ngorongoro nchini Tanzania limepewa fidia na kuondoka rasmi leo kuelekea Tanga kuanza maisha mapya.
Kundi hilo la familia 27 kati ya 103 zilizokubali kuondoka kwa hiyari kwenye hifadhi hiyo, lilitoka jana hifadhini na kufikia mji wa Karatu, Arusha kabla ya kuanza safari alfajiri ya leo kuelekea kwenye makazi yaliyoandaliwa na serikali katika kijiji cha Msomera, wilaya ya Handeni.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongella, aliyeongoza zoezi la kuwapa hundi za fidia wananchi hao wa jamii ya kimasai, mbali na kusifia zoezi hilo kuwa ni la kihistoria, amesema ni endelevu litakalohusisha familia zingine zinazoendelea kujiorodhesha.