Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Katika kipindi cha miezi miwili, mapadri wawili wamepoteza maisha kwa vifo vyenye utata
Kanisa Katoliki nchini Tanzania linakiri kukumbwa na mgagaziko kuhusu kuuawa kwa mapadri wake wawili wa kigeni vilivyotokea katika kipindi kifupi cha miezi miwili.
Hapo jana Polisi mkoani Mbeya ilithibitisha kifo cha Padri wa Kanisa hilo jimbo kuu la Mbeya wa Shirika la wamishionari wa Afrika (White Father), Michael Samson baada ya mwili wake kuokotwa mtoni, ukionekana kukatwatwaka na kutenganishwa viungo vyake. Mwezi April mwaka huu pia, Padri Francis Kangwa wa Parokia ya Mbezi, jijini Dar es Salaamm, alikuta amekufa kwenye tanki la maji kwenye makazi ya mapadri jijini humo. Uchunguzi wa awali wa Polisi unasema mauaji ya Padri huko Mbeya ni ya makusudi, na sasa inaendelea na uchunguzi zaidi.
Vifo hivi ‘tata’ vimeibua mjadala kuhusu namna vinavyotokea, nini kinaendelea ama mapadri wa kigeni wa Kanisa hilo wanawindwa na nani ni muhusika? Mwandishi wwetu Yusuph Mazimu amezungumza na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa hilo nchini Tanzania, Padri Charles Kitima.