Mzozo wa Ukraine: Kwa nini Ukraine haishambulii ardhi ya Urusi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Zimepita siku zaidi ya 100 tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi wake nchini Ukraine na mapambano ya ardhini yanasalia kuwa magumu na yanayofanyika kwa haraka.
Vikosi vya Moscow vimerudishwa nyuma kutoka Kyiv, mji mkuu, na wanajeshi waliotumwa na Vladimir Putin hadi mji wa pili, Kharkiv, wamelazimika kuvuka mpaka na kurudi Urusi - lakini mapigano makali yanaendelea.
Waandishi wetu katika uwanja huo walijibu maswali yako kuhusu mageuzi ya vita na uwezo wa Ukraine kunusurika mashambulizi ya Urusi.
Waandishi hao ni:
- Sarah Rainsford, mwandishi wetu wa Ulaya Mashariki, akiripoti vita vya Ukraine baada ya zaidi ya miongo miwili ya kuripoti nchini Urusi.
- Steve Rosenberg ni mhariri wetu huko Moscow na mtaalamu wa Urusi ambaye ameishi huko tangu mwisho wa Vita Baridi.
- Mwanahabari wetu wa kidiplomasia Paul Adams, ambaye ameripoti kutoka maeneo yenye migogoro duniani kote, ikiwa ni pamoja na Ukraine.
1: Nini kitakachofuata kwa Urusi?
Steve Rosenberg, Mhariri, Moscow
Baada ya upinzani wa awali, wanajeshi wa Urusi wanaonekana kusonga mbele katika eneo la mashariki mwa Ukraine. Lakini lengo la Moscow ni nini? Ikiwa Urusi inamiliki maeneo yote ya Donetsk na Luhansk, je Kremlin itasimama au itaendelea kusonga mbele kuelekea maeneo mengine?
Hata kama Urusi itaamua kuacha, hakuna uhakika kwamba itakuwa ni kukomesha kwa kudumu kwa uhasama. Wanasema chui habadilishi madoa yake...nashuku hata rais wa Urusi hangebadilisha.
Katika hotuba na makala zake, Vladimir Putin aliweka wazi kwamba haoni Ukraine kama taifa huru, bali ni eneo ambalo kihistoria ni mali ya mzunguko wa Moscow. Alitoa wito kwa jeshi la Ukraine kuisimama na kupindua uongozi wa Ukraine. Hili halifanyiki. Lakini hiyo haimaanishi kuwa Vladimir Putin amekata tamaa ya kuilazimisha Ukraine kurejea katika nyanja ya ushawishi ya Moscow, hata katika kukabiliana na vikwazo vya Magharibi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine yalianza muda mfupi baada ya uvamizi wa Urusi. Kulikuwa na raundi kadhaa za mazungumzo, lakini hayakusababisha makubaliano yoyote.
Kwa sasa, majadiliano yamekwisha. Pande zote mbili zinalaumiana kwa hili. Lakini kumbuka kwamba ikiwa majeshi ya Urusi hayangeshambulia Ukrainia, kusingekuwa na haja ya kusitisha mapigano!
Kuna uwezekano kwamba maendeleo kwenye uwanja wa vita yataamuru ni lini, vipi na kwa namna gani mazungumzo yataanza tena.
2: Kwanini Ukraine haishambulii Urusi?
Sarah Rainsford, mwandishi Ulaya Mashariki
Ni vita ambayo Ukraine haikuchagua na haikuanza. Kwa asili yenyewe inajihami: nchi inapigania haki yake ya kuwepo dhidi ya mashambulizi ya Kirusi.
Sidhani kama unaweza kudharau gharama ya Ukraine kuzuia Urusi kuchukua Kyiv, na sasa kujaribu kuzuia kusonga mbele kwa wanajeshi wa Urusi kwenye eneo la Donbas.
Kuishambulia Urusi itajiweka kwenye wakati mgumu zaidi wakati huu Ukraine ikikalia kuti kavu

Chanzo cha picha, Getty Images
Je ni kweli baadhi ya wanajeshi wa Urusi wanagoma kupigana?
Ni kweli, ila ni ngumu kujua ukubwa wake. Ukweli ni kwamba Urusi haijatangaza rasmi vita: Vladimir Putin anasisitiza kuita uvamizi wake "operesheni maalum", ambayo ina maana kwamba askari wa kitaaluma wanaweza kukataa kushiriki. Wanaweza kufukuzwa kazi, lakini hawawezi - au hawapaswi - kufunguliwa mashitaka.
Kutokana na taarifa yangu mwenyewe nchini Ukraine, najua kwamba askari wengi wa Kirusi waliotumwa mwanzoni mwa uvamizi huu walikuwa vijana na wasio na uzoefu; wengine hawakujua wangeenda vitani, wengine walidhani wangeiteka Kyiv katika siku chache, bila upinzani.
Lakini ushahidi wa vita vikali na athari kubwa kila mahali, ikiwa ni pamoja na katika mabehewa ya treni ambayo nimeona yakiwa na askari wa Kirusi waliokufa. Kwa hiyo sishangai kwamba wengine wanakataa kupigana, hasa sasa kwa kuwa wamejionea wenyewe kwamba Ukraine haitaki "kukombolewa". Lakini hatuoni ripoti za kuondoka kwa watu wengi.
Je! Nchi za Magharibi zinazoiunga mkono Ukraine zinaogopa ama zinachukua hatua kwa tahadhari?
Paul Adams, Mwanahabari wetu wa kidiplomasia

Chanzo cha picha, Getty Images
Baadhi, kama Jamhuri za Baltic, wameelezea kuchanganyikiwa kwa kile wanachokiona kama kutokuwa tayari kwa nchi za Magharibi kuipa Ukraine kila kitu inachohitaji.
Lakini kwa mapungufu yote ya kijeshi ya Urusi - ambayo yamefichuliwa sana katika miezi hii zaidi ya miezi mitatu ya mapambano - bado ina safu kubwa ya silaha za nyuklia ambayo imedokeza kwamba inaweza kutumia.
Maafisa wa Magharibi wanaendelea kuamini kwamba hakuna uwezekano wa Moscow kuamua chaguzi kama hizo za siku ya mwisho, lakini hawawezi tu kupuuza hatari hizi.
Na wakati baadhi, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Liz Truss, wanaonekana kuwa na furaha kuzungumza juu ya kufukuzwa kwa majeshi ya Kirusi kutoka Ukraine yote, wengine wanaona kuwa kurejea kwa hali iliyokuwa asubuhi ya Februari 24 ni hali inayowezekana na kufikiwa.
Je mazungumzo ya amani yameishia wapi?
Steve Rosenberg, Mhariri, Moscow
Mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine yalianza muda mfupi baada ya uvamizi wa Urusi. Kulikuwa na raundi kadhaa za mazungumzo, lakini hayasaidia kufikiawa kwa makubaliano yoyote. Kwa sasa, majadiliano yamekwisha. Pande zote mbili zinalaumiana kwa hili. Lakini kumbuka kwamba ikiwa majeshi ya Urusi hayangeshambulia Ukraine, kusingekuwa na haja ya kusitisha mapigano!
Kuna uwezekano kwamba maendeleo kwenye uwanja wa vita yataamuru ni lini, vipi na kwa namna gani mazungumzo yataanza tena.












