Mzozo wa Ukraine: Bilionea wa Urusi Oleg Tinkov ajipata mashakani kwa kumkashifu Rais Putin na uvamizi wa UKraine

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Baada ya kupaza sauti yake dhidi ya uvamizi wa Ukraine na kupoteza mamilioni.

Oleg Tinkov, oligarch wa Urusi ambaye mwezi uliopita alikosoa "mauaji" ambayo nchi yake inatekeleza huko Ukraine, anahakikishia kwamba alilazimika kuuza hisa alizomiliki katika TCS Group Holding, ambayo inadhibiti Benki ya Tinkoff, akikabiliana na vitisho kutoka kwa Kremlin vya kutaifisha taasisi hiyo.

"Sikuweza kujadili bei. Ilikuwa kama mateka, unachukua kile wanachokupa. Sikuweza kujadili," tajiri huyo aliliambia The New York Times kuhusu uuzaji huo.

Mfuko huo ambao unawakilisha 35% ya hisa za TCS - ambazo seti ya makampuni chini ya chapa ya Tinkoff inashughulikia sekta kuanzia benki na bima hadi huduma za simu - ilinunuliwa na kampuni inayomilikiwa na mfanyabiashara mkubwa wa madini Vladimir Potanin, anayejulikana kwa uhusiano wake na Vladimir Putin.

Kwa mujibu wa Tinkov, siku moja baada ya ujumbe wake wa Instagram ukitoa wito wa kusitisha "vita vya kichaa" nchini Ukraine, maafisa wa Kremlin waliwasiliana na watendaji wa benki ya Tinkoff kuwaonya kwamba ikiwa hawatakata uhusiano naye, basi benki hiyo itataifishwa.

Taasisi ya kifedha ambayo Alhamisi iliyopita iliripoti juu ya uuzaji wa hisa, ilikanusha kwa New York Times kwamba shughuli hiyo ilifanyika chini ya shinikizo. "Hakujawa na vitisho vya aina yoyote dhidi ya uongozi wa benki hiyo," alibainisha.

Kupoteza thamani

Tangu mwanzilishi wake alipokosoa uvamizi wa Urusi wa Ukraine, benki imefanya jitihada za umma kujitenga naye.

"Oleg hajawahi kuwa huko Moscow kwa miaka mingi, hakuhusika katika maisha ya kampuni na hakuhusika katika mambo yoyote," benki hiyo ilisema katika taarifa.

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Hakika, Tinkov ameishi nje ya Urusi tangu mwaka 2019, alipoondoka kwenda kupata matibabu ya saratani ya damu. Baadaye, alijiuzulu huku akiendelea kuhifadhi hisa zake.

Mwishoni mwa mwaka jana, bei kwenye Soko la Hisa la London ilikuwa karibu dola za Marekani milioni 20,000, ingawa kulingana na jarida la Forbes tangu mwanzo wa vita ilipungua kwa zaidi ya 90%.

Kulingana na uchapishaji huo, wakati utajiri wa Tinkov ulikuwa na thamani ya dola bilioni 7.7.

Ingawa haijafichuliwa ni kiasi gani cha pesa alichopokea sasa kwa mauzo ya hisa zake, makadirio yaliyochapishwa na gazeti la Kommersant huko Moscow yanakadiria kwamba shughuli hiyo ilifanywa kwa takriban 15,000,000,000, ambayo ni sawa na takriban dola milioni 210 za kimarekani.

Lakini alisema nini kuleta matokeo haya?

Maneno makali ya Tinkov

Onyo: Hadithi hii ina lugha ambayo wengine wanaweza kuiona kuwa ya kuudhi.

Katika chapisho la Instagram lililokuwa na maneno makali, Tinkov alisema kuwa haoni "mnufaika yeyote" katika mzozo wa Ukraine.

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Mbali na kuanzisha benki ya kimataifa ya mtandao ya Tinkoff Bank, mjasiriamali huyo alimiliki timu ya waendesha baiskeli ya Tinkoff-Saxo.

Yeye pia ni mmoja wa Warusi mashuhuri zaidi kulaani hadharani vitendo vya Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Matajiri wengine wawili wa oligarchs nchini humo, Mikhail Fridman na Oleg Deripaska, wametoa wito wao pia wa kutaka amani, lakini hawakumkosoa Putin moja kwa moja.

Unaweza pia kusoma

Tinkov hapo awali alikana kuwa na uhusiano wa karibu na Rais Putin na, kwa hakika, alijipatia utajiri katika sekta nyingine isipokuwa madini na nishati, ambako wafanyabiashara wengi wanaohusishwa na Kremlin wanatokea.

Katika chapisho lake la Instagram, Tinkov alidai kuwa 90% ya Warusi wanapinga vita vya Ukraine, na kuongeza kuwa "wajinga ni 10% katika nchi yoyote" .

"Sioni mnufaika MMOJA MMOJA katika vita hivi vya kichaa! Watu wasio na hatia na askari wanakufa," aliongeza.

"Na je, jeshi litakuwa jema ikiwa kila kitu kingine nchini ni upuuzi na msingi wa upendeleo, kubembeleza na utumishi?" aliendelea.

Kabla ya Urusi kuivamia Ukraine mwishoni mwa Februari, utajiri wa Tinkov ulikadiriwa kuwa zaidi ya dola bilioni 4.4.

Lakini tangu wakati huo amepoteza hadhi yake ya bilionea, kwani hisa katika benki yake zimeporomoka, Forbes iliripoti mwezi Machi.

Tinkov aliandika katika chapisho lake, wakati huu kwa Kiingereza: "Dear 'Collective West,' tafadhali mpe Bw. Putin njia wazi ya kuokoa uso wake na kukomesha mauaji haya. Tafadhali kuwa na busara zaidi na utu."

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Mfanyabiashara huyo wa Urusi ametajwa kuwa "mjasiriamali " ambaye taaluma yake imeanzia kwenye mashindano ya baiskeli hadi kuagiza bidhaa za kielektroniki, kuuza vyakula vilivyogandishwa, kutengeneza bia, kutoa kadi za mkopo na kisha mpya hadi magurudumu mawili kama mmiliki wa timu ya baiskeli ya Tinkoff-Saxo.

Ukosoaji kutoka kwa oligarchs wengine

Fridman, bilionea benki, amesema kuwa maoni yoyote ya kibinafsi yanaweza kuwa hatari sio kwake tu bali pia kwa wakurugenzi na wafanyakazi wa biashara zake.

Wakati huo huo, mfanyabiashara Boris Mints, ambaye alifanya kazi na serikali ya Urusi katika miaka ya 1990 lakini alifutwa kazi yake ya kisiasa siku nne baada ya Putin kuchukua madaraka, aliungana na Tinkov kumkosoa rais moja kwa moja.

Mints, ambaye anaishi nchini Uingereza, kwa sasa anachukuliwa hatua za kisheria na Kremlin. Aliambia BBC kwamba "kila mtu mwenye akili timamu ana wajibu wa kushutumu vita hivi vya kutisha na kuongezeka kwa ubabe wa Vladimir Putin."

"Lazima sote tufanye tuwezavyo kusaidia raia wa Ukraine wanaoteseka kutokana na shambulio hili la kikatili, iwe Ukraine au kama wakimbizi nje ya mipaka yake," aliongeza.

Serikali ya Uingereza imemuwekea vikwazo Tinkov na Warusi wengine wengi waliotambuliwa kuwa na uhusiano wa karibu na Kremlin.