Wanajeshi wa Urusi wameshindwa kupiga hatua yeyote kubwa katika saa 24 zilizopita -Intelijensia

"Licha ya kuongezeka kwa shughuli mbalimbali, vikosi vya jeshi la Urusi havijafanikio kwa kiasi kikubwa katika saa 24 zilizopita huku mashambulizi ya kukabiliana na Ukraine yakiendelea kuzuia juhudi zao," Idara ya Ujasusi ya Ulinzi (DI) ya wizara ya ulinzi ya Uingereza ilisema katika taarifa yake ya hivi karibuni.
Taarifa hiyo inasema vikosi vya anga na majini vya Urusi "havijaweka udhibiti katika eneo lolote kutokana na jitihada za ulinzi wa anga na bahari wa Ukraine kupunguza uwezo wao wa kufanya mashambulizi makubwa".
Pamoja na ushindi uliotajwa wa Mariupol [kusini-mashariki mwa Ukraine], mapigano makali yanaendelea kutokea na kukatisha tamaa majaribio ya Warusi ya kuuteka mji huo".
Hii "inapunguza kasi ya jitihada za Urusi" katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine, DI anaongeza.

Chanzo cha picha, Reuters
Mapema wiki hii, Urusi ilitangaza hatua ya pili ya "operesheni yake maalum ya kijeshi" nchini Ukraine, ikisema sasa itazingatia kuchukua udhibiti wa Donbas.
Haya yanajiri baada ya wanajeshi wa Urusi kujiondoa kutoka kaskazini-mashariki mwa Ukraine, baada ya kushindwa kuchukua miji mikubwa - ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Kyiv - huko.

Urusi ina malengo ya kuchukua udhibiti kamili wa kusini mwa Ukraine na pia eneo la mashariki la Donbas, kamanda mkuu wa Urusi anasema.
Meja Jenerali Rustam Minnekayev alinukuliwa katika vyombo vya habari vya serikali akisema lengo hilo lingeruhusu Moscow kuunda daraja la ardhini kuelekea Crimea, ambalo ililinyakua mnamo 2014.
Pia alisema itaipa Moscow ufikiaji wa eneo la kujitenga linaloungwa mkono na Urusi la Transnistria huko Moldova.
Transnistria ni eneo dogo linalopakana na magharibi mwa Ukraine.

Chanzo cha picha, Getty Images
Haijawekwa wazi kama maoni ya Jenerali Minnekayev yaliidhinishwa rasmi na Kremlin, lakini yalinukuliwa sana katika vyombo vya habari vya serikali ya Urusi ikiwa ni pamoja na mashirika ya habari ya Interfax na Tass.
Maafisa wa ulinzi wa Urusi walimwambia mwandishi wa BBC Steve Rosenberg kwamba "wanachunguza" maoni ya jenerali huyo, ambayo - ikiwa yatathibitishwa - yanatoa ufahamu wa kwanza kuhusu mipango inayoweza kutekelezwa na Urusi katika wiki zijazo.
Unaweza pia kusoma
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine














