Wabunge wa Tanzania wamekataa kupokea ripoti ya Mto Mara wakidai haina mashiko

Iliyochapishwa

Wabunge wa Tanzania wamekataa kupokea ripoti ya Mto Mara iliyoandaliwa na Waziri wa Mazingira, Suleiman Jafo.

Timu hiyo ilikuwa imepewa jukumu la kuchunguza sababu ya uchafuzi wa mazingira ambao umezua wasiwasi kufuatia vifo vya baadhi ya viumbe hai hasa samaki.Rangi ya maji katika mto Mara ilibadilika.

Kutokana na hatua hiyo iliyochukuliwa na wabunge hao awali mwandishi wa BBC Regina Mziwanda amezungumza na katibu wa wabunge wa Chama tawala cha Tanzania CCM, ambaye pia ni mbunge wa Mlalo Rashid Abdallah Shangazi na kwanza ametaka kufahamu juu ya ushauri ama mapendekezo yaliyotolewa katika kikao cha wabunge, kuhusiana na ripoti hiyo inayopingwa na kwamba isichapishwe popote na kujua ushauri huo umezingatia nini hasa?