Sweden: Wafahamu viongozi waliodumu madarakani kwa muda mfupi zaidi duniani, wengine mpaka dakika 15

Iliyochapishwa

Magdalena Anderson ameandika historia katika siasa za Sweden na duniani mara mbili kwa siku moja. Kwanza, mapema asubuhi kuelekea mchana, alipata uungwaji mkono mkubwa bungeni kwa kuteuliwa kuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke nchini humo, kabla ya kujiuzulu wadhifa huo mchana na kuweka historia ya kiongozi mkuu aliyekaa madarakani muda mchache zaidi Sweden.

Sweden ndio nchi pekee ya Scandinavia ambayo haijawahi kuongozwa na mwanamke kama kiongozi mkuu wa serikali. Alijiuzulu kwa sababu mshirika wa muungano wa chama chake alijiondoa serikalini na bajeti iliyopendekezwa haikupitishwa. Badala yake, bunge lilipigia kura bajeti iliyopendekezwa na upinzani, ambayo inajumuisha mrengo wa kulia.

"Nilimwambia spika wa bunge kwamba nilitaka kujiuzulu," Anderson, 54, aliwaambia waandishi wa habari. Aliongeza kuwa ana matumaini ya kujaribu kuwa waziri mkuu tena wakati ujao, lakini tu kwa kuungwa mkono na chama chake.

"Kuna utaratibu wa kikatiba kwamba serikali ya mseto inapaswa kujiuzulu chama kimoja kinapoondoka. "Sitaki kuongoza serikali ambayo uhalali wake utatiliwa shaka," alisema kiongozi huyo wa chama cha Social Democrats.

Huyu ni mmoja tu, wako viongozi wengine waliowahi kukaa madarakani muda mfupi zaidi kutokana na sababu mbalimbali.

Christopher Elnathan Okoro Cole - Sierra Leone

Okoro Cole alikuwa rais wa Sierra Leonean kwa siku mbili. Alihudumu kama gavana mkuu na raia wa nchi hiyo kwa siku mbili tu mwaka 1971.

Wakati huo miaka ya 1960's na mwanzoni mwa 1970 kulikua na utata wa mabadiliko ya katiba baada ya utawala wa kiflame kuwekwa kando mwaka 1971.

Ilikuwa wazi Bwana Siaka Stevens, waziri mkuu wa wakati huo, angekuwa Rais. Cole, ambaye alikuwa ameteuliwa kama mkuu Machi 31, alitumikia uraia kwa siku moja, siku ya pili akjakabidhi nchi.

Baada ya kukabidhi nchi akarejea kwenye nafasi yake ya ujaji mkuu wa Sierra Leone mpaka mwaka 1978.

Siaka Stevens- Sierra Leone

Stevens ni mmoja wa viongozi na wanasiasa waliokuwa na nguvu kubwa Sierra Leone akitokea chama cha mrengo wa kushoto cha All People Congress in Sierra Leone.

Katika uchaguzi wa mwaka 1967 e, chama chake kilipata ushindi kiduchu sana wa viti vya uwakilishi, kuwafanya kuongoza serikali.

Waziri mkuu aliyekuwa anaondoka madarakani hakufurahishwa na kutaka jeshi liingilie kati, Machi 21, dakika chache baada ya kuapishwa, kama waziri mkuu, jeshi lilimvamia kwenye makazi yake na kumuweka kizuizini.

Bahati nzuri kwak , Sierra Leone ilimrejesha madarakani mwaka 1968.

Pedro Lascuráin - Mexico

Mwanasiasa wa Mexico Pedro Lascuráin ambaye alikuwa rais wa 34 wa Mexico kwa muda mfupi unaokadiriwa kuwa kati ya dakika 15 na 56 kabla ya kuachia ngazi kwenye mapinduzi ambaye yalimfanya jenerali Victoriano Huerta kuwa rais anayefuata.

Anatajwa kama rais aliyehudumu kwa muda mfupi zaidi Mexico, licha ya kukubalika kwake na wanasiasa mashuhuri na watu waliomuona kama mungwana.

Louis XIX wa Ufaransa

Huyu anatajwa kama mfalme wa muda wote aliyeongoza kwa muda mfupi zaidi duniani.

Baada ya kutekwa nyara kwa baba yake wakati wa Mapinduzi ya Julai mnamo Agosti 2, 1830, alichukua kiti cha enzi, lakini alijiuzulu kama dakika 20 baadaye.

Utawala huu unabishaniwa, kwani baadhi ya wanahistoria wanaamini utawala huu ni mfupi sana kuwahi kutokea.

William Henry Harrison - Marekani

William Henry Harrison alikuhudumu kwa muda mfupi zaidi kwneye nafasi ya urais. Baada ya mwezi mmoja ofisini, rais wa 9 wa Marekani, William Henry Harrison, alifariki mwaka 1841.

Kiongozi huyo alikuwa rais mkongwe zaidi katika historia ya Marekani akiwa na miaka 68 kabka ya muongo mmoja baadae Ronald Reagan akimpiku kwa kuwa rais akiwa na miaka 69.

Anachokumbukwa zaidi Harrison ni kwamba alitoa hotuba ndefu zaidi katika wakati ambao kulikuwa na baridi na barafu nyingi bila kuwa na vikinga baridi kama koti ama nguo ziko, ikamsababishia kupata nimonia na kufariki muda mfupi baadae. Ingawa kwa sasa watu wanafikiria tofauti.

Mfalme Dipendra wa Nepal:

King Dipendra alitawala kwa siku 3 tu katika utawala tata uliogusa familia. Aliposhika hatamu ya ufalme, Dipendra uhusiano na wazazi wake ulikuwa na misuko suko kufuatia nia yake kumuoa mrembo Devyani Rana, ambaye alikuwa anatokea familia adui iliyokuwa na uhusiano usioa sawa na familia yake ya kifalme.

Alikuwa mlevi wa kupindukia akawauwa kwa risasi wazazi wake na ndugu zake katika tukio lilioshangaza dunia. Haifahamiki kama alitaka kuuawa na walinzi wa ufalme ama alitaka kujiua mwenyewe, lakini alipona ila alikuwa hoi, akaja kufariki siku tatu baadae.