Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mahakama ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda iliopo Tanzania yageuzwa kuwa makumbusho ya kihistoria
Dunia bado ina kumbukumbu ya yale yaliyotokea katika mauaji ya Kimbari yaliyotekelezwa huko nchini Rwanda miaka mingi iliyopita na wahusika kukamatwa na kuhukimiwa vifungo mbalimbali na wengine kuachwa huru kutokana na Mahakama kujiridhisha kuwa hawakuwa na hatia.
Sasa Mahakama iliyokuwa ikitumika kuendesha kesi hizo nchini Tanzania katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC imegeuzwa kuwa sehemu ya Makumbusho kwa ajili ya wanafunzi na wafuatiliaji wa historia hii toka pande zote ulimwenguni kujifunza mengi zaidi.
Mwandishi wa BBC @frankmavura alipata wasaha wa kuitembelea Mahakama hii.